Friday, February 27, 2009

Swala la KAMA huna PAPARA usihofie TUSI!

Lakini,...
....LABDA KAMA HUNA papara, TUSI utukanwalo kama KWELI ni tusi na sio sifa, TUSI utukanwalo HUNUNA zaidi.

Swali:

  • BADO unamshangaa APAPARIKAYE na TUSI wakati nyuma ya tusi kuna SIFA ya mtu?


WIkienDI NJema!
Tutulie na Aaliyah- At Ur Best.


Au ngojea Inner Circle wazungumzie - Sweat

Thursday, February 26, 2009

Wakati UNAENDELEA kupenda sehemu za SIRI za mwenzio!

TATIZO ...
...... la afanyaye SIRI ni kufikiri au KUDHANIA kifikiriwacho ni siri ni kweli NI SIRI, au labda NI SIRI.

WAKATI....
.... unaficha siri, KUMBUKA unawaficha wasio na JUHUDI za kutaka kujua SIRI yako ni, NI nini, au TU unajaribu kuficha ambacho si siri kwako ili kiwe kwa wengine SIRI.

KUNAUWEZEKANO,...
... siri yako wanajua ambao HAWAJUI unafikiria kuwa HIYO ni SIRI.


LABDA,...
... siri yako si SIRI ndio maana wewe MWENYEWE umeistukia na kuipa jina SIRI au kufikiria LABDA KWELI ni SIRI.

WAKATI...
.....unaficha SEHEMU za siri , kumbuka kuwa ni ukweli asilimia kubwa YA ambao hujui sehemu zao za siri unajua WANAZAA au KUZALISHA na labda unajua watoto wao , NA si SIRI.
Swali:

  • Ukiona watoto wa MWENYE siri ,SI unajua kuna MTU anajua sehemu zake za SIRI?
  • Unauhakika una siri au hujui ajuaye yako SIRI?

Naacha!
Hebu twende tena GABON kwa Oliver N'goma katika - BANE

AU ngojea tu Will Smith azungumzie - Miami..

Photobucket


Photobucket


Photobucket


Nipo na kama upo Stockholm labda tutakutana.
Nipo kama baadhi za picha zisemavyo....

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Nipo na usafiri upo kama wewe sio MNENE.
Photobucket

Wednesday, February 25, 2009

LINI Tanzania kutakuwa na CHAMA CHA MAPINDUZI?

Inasemekana TANZANIA ina WANAMAPINDUZI!

Na,...
....TANZANIA kuna WANAMAPINDUZI.
Swali:

  • Unajua chama CHAO?
  • Unauhakika wanamapinduzi wanahitaji CHAMA?


NAACHA!
Tulia twende Brazil kutulia na Zé Renato na Milton Nascimento

Au ngojea BUGLE aseme- WHAT WE GONNA DO...

Tuesday, February 24, 2009

Kama kuna BUSARA za KUJILAUMU!

Labda,....
.... kama bado unakumbuka kujilaumu kuna uwezekano una UTU!

Kama,....
..... unajilaumu , si lazima lakini kuwa ni wewe wa KULAUMU.
Lakini wakati UNALAUMIWA labda ni kweli kuna kilichofanyika.

Swali:

  • Tokea uzaliwe unafikiri umesahau kujilaumu mara ngapi?
  • Wakati unalaumiwa ni mara ngapi unajua ukweli si wewe ustahilie lawama?


Siku Njema!

Au kama una muda tulia na Faya Tess katika kibao -GINA

Monday, February 23, 2009

Labda BASHA ni MSENGE!

LABDA,...
....basha MSENGE kwa sababu anakula unacho ONJA!.


Lakini,...
.... kumbuka ukionja maana yake UMEKULA.

Inawezekana unakumbuka bado BASHA na MSENGE wanakula UGALI kama tu asiye TALIBANI.

Wakati....
.... unafikiria kwanini Msenge hajaoa BASHA ,kuna uwezekano unafikiri unajua ndoa.

Na,...
....kunauwezekano kama umefikia kujua ndoa NI nini ,....

.....basi....
....ndoa YAKO imeanza kuharibika au imeshaharibika ndio maana una utaalamu wa ndoa.
Swali:
  • AU?

Lakini,...
.... kabla basha hajaonja bado ni BASHA.

Msenge anapendwa kulalamikiwa kwa sababu ya roho nzuri ya kutoa , ila ukweli ni kwamba hakuna basha kama msenge hayupo.
Swali:
  • Si unakumbuka kuna watu wanahangaikia sana KITU wakati LABDA wahangaikiacho kama hakijaoshwa labda kinanuka Mkojo au mavi?
  • Unakumbuka PADRE, Shekhe na MSENGE ni watu ambao wamebobea kwenye ZAO wafikiriazo waziweza fani?
  • AU?

NAACHA!
Kumbuka NAWAZA tu!
siKU NJema!


Tumtembelee mtoto wa Bob Marley kwa jina Steve Marley azungumzie.. - Rebel In Disguise

Au Ngojea Snoop Dogg na Butchy Cassidy wamalizie kwa kusema - Loosen Control..

ASANTENI WADAU WOTE!
Asante pia kwa wadau ambao tulikuwa wote JUZI ya JANA na kamera yangu ilibahatika kuwadaka kama hawa.....

Photobucket
Papaa Ray a.k.a Raymond Mutafungwa , a.k.a Mkuu wa kikao, ASANTE!


Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket



Photobucket



Photobucket






Photobucket







Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Papaa Ronaldo, ASANTE!

Photobucket





Photobucket

Photobucket

Friday, February 20, 2009

INASEMEKANA kuna siri ya KUJUA kama UGALI UMEIVA kabla ya KUUTOMASATOMASA, kuubonyeza au KUUONJA!

LABDA,....
......binadamu ni MALIMBUKENI!:-(

Baada ya binadamu kugundua kuna uwezekano wa kupika, wamesahau kuwa MBICHI NYINGI hulika.:-(


Lakini,...
.. ....inasemekana UGALI hujisikia vizuri ukiliwa kwa mkono , na maswala ya kula kwa UMMA au KIJIKO yana uparura tu ugali na kuutia majeruhi ya dondoshayo njiaani utamu, katika safari ya utamu wa ugali kutoka kwenye sinia kwenda mdomoni.

Na....
.....wakati unajiandaa kufinyanga TONGE la UGALI ni muhimu ujue UNAUNYEMELEA ugali wa aina gani.

Kila aina ya ugali, kuanzia wa mahindi, muhogo, ulezi , BILA KUUSAHAU ugali wa unga wa magimbi, kumbuka UNAHITAJI mbinu tofauti ya mashambulizi hata katika KUUTOMASATOMASA, kuushikashika au tu katika KUUTUMBULIA MACHO ugali, hata KAMA safari hii ni katika kutaka kujua tu kama ugali umeiva au bado bila KUUONJA!

Swali:

  • AU?

Lakini,...
...... nisikudanganye kwa kukataa kuwa hakuna WAZOEFU wa ugali hata wa Mbatata ambao wanajua UGALI WA MBATATA umeiva bila KUUSHIKASHIKA, KUUTOMASA au hata KUUONJA. Na sina uhakika kama hawa WAZOEFU huwa wanatumia harufu au ni mbinu gani zaidi katika utaalamu ,na labda hiyo ndio siri ya UZOEFU katika taaluma.

NA TATIZO....
.... la wote wahangaikiao staili za kutaka kujua IMEIVA au BADO, mara nyingi WAMESAHAU tu kuwa WAHANGAIKIAVYO vinalika vikiwa VIBICHI.

Ni kweli kabisa nakwambia kuwa kuanzia;
  • Nyama
  • Nyanya mshumaa
  • Mchele
  • Wali
  • Unga wa mahindi
  • Ugali

AU
  • Nakadhalika kadhaaa,.....
......VYOTE huweza kulika vibichi hata kama huna ujazo wa njaa WAKUTOSHA.

Swali:
  • Si kuna uwezekano bikira mdogo yuko tayari ingawa mkubwa ndio inaaminika kaandaliwa na yuko tayari ingawa naye hayuko tayari ingawa yuko tayari?
  • Unakumbuka kuna mpaka wataalamu wajawazito walao mpaka UDONGO?


SIKUKATAZI!

Endelea tu KUTOMASATOMASA , kubonyeza au KUONJA kama ni kweli HUZIJUI MBIVU HIZI kuwa ni MBIVU hata ukiwa kona ya saba KULE katika mkao wa KUNYEMELEA huku ukiwa na wasiwasi labda ni MBICHI!

Kumbuka kijiweni kuna KIPINDUPINDU lakini, kabla hujafinyanga tonge !

Na nimesikia kuna wenye busara wadaio ukinawa mikono kabla, INASAIDIA hata kwa kuonyesha umejaribu kujiandaa angalau kwa kunawa kabla ya mashambulizi ya tonge.

Labda,...
..... tutumie tu kijiko!
Swali:
  • SI labda ni kweli ukila vibichi utaumwa tumbo?
  • Hivi sijui tutumie tu kijiko?
  • Si utaumwa tu tumbo au kuharisha kama vibichi vinakuumiza hata ukitumia kijiko?

Lakini,....
... Labda endelea kula vibichi kama vilivyoiva hujazoea, USIJEUMWA TUMBO buuure!

Mimi simo!

NAACHA!
Kumbuka NAWAZA tu hapa!



wiKIENdi njEMa!
Twende kidogo kwa Wakyuba kukutana na Orishas wakidai - 537 CUBA



Au tu tupitie tena Jamaica kwa Admiral Tibet, Shabba Ranks & Ninja man enzi hizo , watupunguzie spidi kwa kitu - Serious times

JINSI ya kumbembeleza WAZIRI mkuu AKILIA!

Wakati katibu MKUU au mtoto analia,.....
...... kumbuka KUFARIJIKA kwa kujua kwa vyovyote vile hawawezi kulia DAIMA hata kama hawatapewa nyonyo.

Tukumbuke pia,....
...... kuna watu wako kimya ila wanalia KWA NDANI!:-(

Pamoja na mwiko wa jamii usababishao kubwa zima kuogopa kulia hadharani, KULIA NI MUHIMU.

Na USIDANGANYIKE....
... kuwa sababu za watu kulia MSIBANI ni kweli wanasikitika marehemu katutoka.

Kuna watu walikuwa wanatembea na KILIO tokea jana na MSIBA wa leo umewawezesha kuangua kilio HADHARANI au nyuma ya mbuyu, na wala walikuwa hawamjui marehemu na kama walikuwa wanamjua MAREHEMU, ...
......WALIKUWA HAWAMPENDI.:-(




Swali:

  • Unafikiri kubwa zima wakati linalia msibani ni dakika ngapi wakati linalia ndani ya dakika linafikiria jambo jingine lisilo husiana na kilio msibani?

  • Unafikiri toto wakati linalilia pipi likiona lawalawa nyama halianzi kufikiria labda ligeuze kilio cha pipi kielekee kwenye lawalawa nyama?
  • Unafikiri wakati mtu ANALIA anakuwa ameshaanza kufikiria jinsi atakavyo malizia gia ya KULIA?


Kumbuka wakati KATIBU MKUU analia, bado kunyonya kidole ni RUKSA.

Na, ....
.... DAIMA kumbuka watu wanatembea na VISIRANI vyao na wanaonekana wanatembea kwa maringo tu na VILIO vyao ingawa unaweza usistukie na ukiwapa sababu ya KUKULILIA WEWE wanaweza wakachukua nafasi hiyo KUJILILIA WAO na YA KWAO.

Na usipoangalia UNAWEZA kupigwa kibao kwa kumchekea mtu halafu usielewe KWA NINI , kumbe mwenzio alikuwa anavisirani vyake anavifuga tokea MWAKA JUZI na SIKU HIZI kwake KUTABASAMU kwa wengine na KUNG'ONG'A ni saresare MAUA.

Swali:
  • AU?
  • Hivi unafikiri hakuna kitu ambacho wewe ni Rais au angalau ni Waziri MKUU kabla hujalia?
JARIBU.....
........ kujipa ruhusa KULIA leo kama unachakulia LEO, utafaidika kwa kulenga kulilia kilichokuliza na kinachohusika katika ULIZI leo. Ukitunza kilio cha leo unaweza kujikuta UNACHANGANYA VILIO na unalia ya marehemu wa leo na yakuaibishwa mwaka juzi ,wakati sasa hivi unatakiwa ulie kwa sababu ya utamu wa penzi.

Na ikibidi kukasirika leo ,.....
.......KASIRIKA leo yaishe leo!
Usije ukaanza kutukasirikia na sisi leo wakati hasira zako zilipewa ujauzito na bosi wako juzi na pia na LIMPENZI lako mwaka JUZI na sisi hatuhusiki:-(

Na ni kweli,...
....Mila , Desturi na Miiko mingine mingi hata ya kijinga inatusaidia kusababisha tunatunza maumivu na vilio mpaka inakuwa vigumu, mambo yakiwa magumu kujua tulilie lipi.

Wakati unamalizia kulia,....
..... jaribu kukumbuka kujiangalia kama ulifanikiwa kutoa KAMASI ili ulifute kamasi kama lilikutoka katika miondoko yako ya kulia.

NAACHA!
Topiki imenishinda!:-(

Hebu tubadili hali ya hewa kwa kukutana na Michael Leahy labda na kwa mbaaali Mtaalamu RON JEREMY, ili kuuliza-How did you get hooked on Porn?...


Au turudi tu Congo na kukutana na Tshala Muana atukumbushe - Mbombo..

Thursday, February 19, 2009

Katika kutembelea SHULE ya VIDUDU!

Shikamooo Watoto!

Swali kwa wakubwa:

  • Hivi kwenye SHULE YA VIDUDU umeshawahi kuona WATU?
  • Hivi kwenye shule ya watu kukiwa na VIDUDU Mwalimu MKUU atatoa UAMUZI gani?

Naacha!

Leo nimebanwa kidogo kujazia muda ndani ya siku iliojaa mambo mengi kwa kuandika kirefu-kifupi UjingaBUSARA kama kawaida!:-)

Kesho Basi kama Hatujafa!

Ngojea tupumzike kwa kupata mtazamo na swali katika fantasi ya Mwanadada katika....-Woman's fantasy(Tahadhari kama mtoto au mtoto mkubwa na utakwazika katika topiki)

Au ngojea FAYA TESS atukumbushe kwenda Kenya katika kibao -Nairobi.....

Wednesday, February 18, 2009

STAILI ya kuongea IMSAIDIAYO mhubiri wa dini , labda INA MSAADA pia kwa mtongozaji!

Katika kila fani wanafani wanastaili zao za kuongea au kushusha kauli KATIKA FANI.

Kama wewe Mkristu, Mkristo ,Mlokole, Muislamu,......., au unatumia tu Waganga wa kienyeji , nafikiri unajua staili ya WAHESHIMIWA WASIKILIZWA katika kumwagia wafuasi KAULI zao hasa za vitisho kabla ya KUAHIDI tamutamu katika FANI.

Mimi binafsi napenda staili ya uongeaji wa kitakatifu wa MAPAPA wa kikatoliki ndani ya fani , na nakiri kuwa huwa wananifanya nijaribu kusikiliza wasemacho ingawa sielewi Kilatini , Kiitali au hata lugha yoyote watumiayo katika kumwaga KAULI kutokana na staili za kumwaga neno kitakatifu zitumikazo katika fani .

Na,...
......katika staili ya kumfanya msichana ajikute anavuta majani au anajikanyaga katika mkao wa nataka-sitaki wa kusikilizia kauli TAMU anazopatiwa na Mtongozaji, inasemekana ukimrekodi anayetongoza utastukia haongei kwa sauti yake ya kawaida.Yuko katika fani.

Na katika fani, hata ukiwa mbali lazima utajua nini kinaendelea watu wawili wakiwa wanapeana kauli hata kama mara hii ni Kijeba anacheza mchezo wa nataka-sitaki wakati MWANADADA anamwaga kauli ya mtongozo ndani ya fani.

Lakini,...
....... binadamu tuko tofauti!:-(


Wengine tumezaliwa tunapenda MDUNDIKO wakati wengine wamezaliwa wanasikia kelele tu kwenye MDUNDIKO.

Nawasiwasi staili ya wahubiri wa kilokole, hata kabla ya KUSIKIA WANAONGELEA NINI kuna watu inawatuliza roho na hao kuna uwezekano wakaokoka kirahisi labda kwa kuogopeshwa zaidi kutokana na staili ya mzungumzaji iwaingiavyo au kwa kuelewa zaidi kutokana na mhubiri kuto waboa kwa staili na kabla ya kwa neno, na kwa hilo labda mhubiri anakuna kipele kwa KAULI kwenye fani.

Kuna wengine ni staili ya mashekhe ya kushusha neno a.k.a KAULI iongezayo uelewa wao wa Kitabu Kitakatifu na ya ALLAH.


Tukirudi kwa mganga wa kienyeji au hata mtongozaji , staili yake inaweza kumfanya mtu akubali jambo ingawa aliyepewa KAULI wakati amejilaza kwenye kitanda chake cha teremka tukaze BAADAYE, atakuwa bado haelewi ni kwanini mambo kama; ya mtongozaji ya;Aisee dada nakupenda sana na kila nikikuona nabanwa mkojo AU ya mganga ya;Lete kijambio cha njiwa jike msenge na mzizi wa jiwe, vilikuwa vinaleta maana sana wakati anapokea kauli.

Bado tatizo ni;...
....tunaamini STAILI ya ashushavyo kauli Mmarekani ni tofauti na ya ashushavyo Mfaransa, na labda ni KWELI ! Lakini ukweli ni kuwa kuna Mgogo wa DODOMA anayeweza akawa anakuna Mfaransa kwa STAILI na kauli za Kigogo kuliko Mfaransa akunavyo Mfaransa mwenzake, kama tu Mmarekani awezavyo kuvutia Mpare wa Mwanga kwa Msuya , kwa staili na UNG'ENG'E labda kuliko awezavyo kulainisha Mmarekani mwenzake mtaa wa jirani kwa kauli , kisa anaongea na ana STAILI za Mmarekani mweusi katika kumwaga KAULI ya fani.

Swali:

  • Ushastukia hata mjinga akiwa anaongea kwa sauti au staili uioanishayo na mwerevu, mjinga haonekani mjinga sana ingawa unajua pointi zake zote hazikuni pointi ingawa anamwaga KAULI?

  • Ushawahi kutofautisha staili na sauti yako ya kuombea msamaha ilivyotofauti na ya kutongozea ingawa zote ni za utulivu na zinamwaga kauli?
  • Si unajua kutongoza maana yake kuomba kwa kubembeleza na sio lazima uwe unaomba nanihii?
Labda ni kweli ,.....
.... staili ya kuongea imsaidiayo MGANGA WAKIENYEJI, ina msaada kwa mtongozaji!
Na labda,....
... Staili ya muhubiri huyu UAMINIYE anahubiri ya nabii wa UONGO haiwezi kutumika kukuokoa kwa kutumiwa na muhubiri mwingine kukuokoa WEWE hata kama inashusha ya NABII wa kweli yenye UKWELI katika staili ya kukugawia KAULI.

Lakini,....
......HATA kama hutaki , ukweli ni kwamba Mtongozaji na Mtongozwaji wapo na staili za kumwaga kauli ZIPO na zina afya kama MNYOO na binamu yake FINYOFINYO!:-(
NAACHA!
Kumbuka nawaza tu hapa!:-(
siKU Njema!


Tulia na Harry Belafonte katika -Man Smart, Woman Smarter....



Au ngojea turudi tena Guadeloupe kukutana na FUCKLY katika kibao -Doudou....

SINA MAJIBU!

Katika hali halisi ya kuumbwa kibinadamu Simon Kitururu kama Chakubanga tu , bado ni MTU.


CHAKUSIKITISHA....
......katika ubinadamu wa baadhi ya binadamu kutafuta mkao wa kuheshimika katika jamii ya kibinadamu, MHESHIMIWA MTU huweza hata KUAHIDI MAJIBU yawezwayo na MALAIKA kama si MUNGU PEKEE.

Mie sina majibu ingawa napenda kuuliza!:-(

Swali:

  • Hivi Mungu kama yuko pekee na hapendi dhambi, unafikiri sio mpweke sana kwa kuwa pekee na labda kwa miaka milioni kadhaa KANUNA kutokana na kujua ataumba binadamu halafu watafanya dhambi?
  • Hivi wewe unajua mangapi kama mjuaji yaliyokufanya uweHAI jana?
  • Sina majibu lakini si kuuliza RUKSA?
NAACHA!
BAADAYE!
Hebu tubadili hali ya hewa kwa kucheki uhusiano wa binadamu katika kufuatilia
Mapping migration with genes katika -phonecian gene.


Au ngojea tena Billy Taylor, Duke Ellington and Willie the Lion waJAZZfai katika kibao -Perdido..

Tuesday, February 17, 2009

KAMA wewe huandiki historia yako kama uijuavyo wewe!

Labda...
.... hatujui hata USAHIHI wa historia ya juhudi za binadamu kugundua choo cha shimo ,hata baada ya miaka yote hii baada ya baadhi ya BIN-ADAMU kuchoshwa na safari za kwenda kichakani ambako ukikosea unaweza kujikuta kichaka kimoja na Mama Mkwe mnachimba DAWA.


Na historia yako kama si wewe uiandikayo, inaweza kusimuliwa na ajuaye CHEMBE kuhusu wewe akiwa katika mkao wa kudai anajua mwili wako mzima hata ile chunusi yako KUNAKO.

Tatizo pia ni kwamba chochote kisemwacho juu yako hukutana MPAKA na masikio yenye UDHAIFU wa kuvumilia UONGO uliopo kwa kutopenda kuhangaikia ukweli mpaka UJITOKEZE kuhusu hata ubikira wa Bikira Maria baada ya kujifungua Yesu.

NAACHA!
Kumbuka Nawaza tu hapa MKUU!

SIku Njema!

Tulia na moja ya bendi nizipendazo sana kwa jina NUTTIN but STRINGZ katika kibao -Thunder..

AU ngojea wamalizie na Broken Sorrow

MBWA MWITU aliyeshiba kaonekana akicheza na MBUZI! (hadithi ya KIJINGA- kisogo cha pili)

Hapo zamani kulikuwa na MBUZI aitwaye KIBEZI DUME, na mbwa mwitu aitwaye BINTI TITI!

Kibezi na Titi walikuwa marafiki wakubwa wapendao kucheza katika kijiwe cha jamii bila viatu.Lakini jamiii iliishi na hofu ya ukweli kuwa Binti Titi anaweza kumla Kibezi Dume.

Hofu ya jamii ilizidi kukua hasa mbwa mwitu- BINTI TITI alivyo kuwa anazidi kukua na mbuzi- KIBEZI DUME alivyozidi kunawili katika safari ya kukua pamoja na ilivyozidi kuwa vigumu kuwatenganisha wasicheze pamoja bila viatu.

Jamii ilikuwa roho juujuu kwa kuamini mbuzi wa jamii ataliwa tu akiachiwa aendelee kucheza na mbwa.

Swali:

  • Hivi chui si huwinda akiwa na njaa tu?

Lakini....
... ni kweli labda mbwa mwitu huwa na hamu na mbuzi.

Tatizo...
.... hatujui apitaiti au mshawasho wa hamu ya MBWA MWITU huyu ya KULA, katika kumuachia mbuzi huyu achezee mpaka gololi zake.


Swali:
  • Si kuna chui walafi?

  • Hivi si nasikia kuna mbuzi wapendao kuliwa?

Lakini ...
.... Mbwa mwitu kama anaendelea kuishi maeneo yenye mbuzi labda kuna ukweli Mbuzi wanaendelea kuliwa.:-(

Tatizo KUBWA katika swala hili la msichana na mvulana linaweza likawa linajengwa zaidi NA hofu ya jamii ifanyayo Mbuzi ajisikie KULIWA zaidi na Mbwa Mwitu ajisikie kula zaidi kwa sababu jamii imekaa mkao wakufikiri chakula kiko tayari kila wakati.:-(

HADITHI imeisha !

DUH!

Hadithi imeisha na ujumbe hakuna!:-(


NAACHA!
Swali:
  • Sasa jamii itafanyaje wakati jamii lazima iwe na Mbwa Mwitu na Mbuzi katika jamii?
  • Hivi katika stori hii ya kijinga mbuzi anaweza akawa ndiye Mbwa Mwitu eeh?

  • Hivi wewe hujawahi kutaka kula wakati umeshiba?



Tutulie na Just for Laughs - Don Juan


Au ngojea BENNY BENASSI acheze na wimbo wa Eurythimics watukumbushe kila mtu kuna kitu anatafuta katika -SWEET DREAMS....

Mr KIBEBERU ndani ya siku! (Hadithi ya KIJINGA -kisogo cha kwanza)

ILIKUWA jumamosi kama jumamosi nyingine kwa Mr Kibeberu na siku ilianza kwa CHAI na KIPORO cha wali na maharage cha juzi.

Pamoja na kwamba kiporo kilikuwa kimeanza kuchacha kwa mbali, hii haikuacha kumfanya Kibeberu ale huku akiachia tabasamu kwa mbaaaaali huku akisema kimoyomoyo hii ni siku ya kujirusha hasa kwa mtu kama mimi niaminiye katika DINI ya KAZI KWA SANA na baada ya kazi ni KUTOA STIMU KWA SANA tu.


Wakati anamalizia kufunga zipu ya suruali na wakati akijiuliza kuwa kwa nini suruali yake ina zipu badala ya vifungo, Kibeberu aliendelea kutabasamu kwa kukumbuka kuwa jioni hii BENDI aipendayo ya Ochestra MSULI PEKECHAPEKECHA ndio itamiliki mirindimo ya mioyo ya watu mjini katika KUPEKECHA.

...............Kama kawaida saa za kikubwa hazikawii kuwadia na jioni ikamkuta Kibeberu akitumia kujulikana katika mchezo aliozoea wa kutaka kuingia kwenye shoo bure ingawa leo hii bila mafanikio.

Lakini kwa uzoefu wa nyoka alijikuta akijinyonganyonga katika foleni na kwa uzoefu alifanikiwa kuwa miongoni mwa washabiki wa Ochestra MSULI PEKECHAPEKECHA waliokuwa ndani ya ukumbi mapeeema!

Kibeberu ndani ya nyumba alienda na miondoko ya kusalimia awajuao na kuchekea VIMWALI wazuri asiowajua katika kujaribu kuweka jeduali likae katika mtindo wa kurahisisha mtongozo hapo baadaye, yote ni katika KUANDAA matibabu ya kujihami na upweke ujao baada ya shoo ili Kidume asijejikuta yuko pekee ghetto.

Kibeberu kwa unyenyekevu aliisogelea BAA yenye kuonekana kuvutiwa na ushabiki wa wajao kula KILAJI na kuipunguzia bugudha ya kujaa pombe. Wakati Kibeberu anatafakari bei za pombe mawazo ya POMBE SI CHAI na uharamu wa pombe yalimkatiza akilini mara mbili na nusu ,kwa kukumbuka makaripio ya SHEKHE na hata Mchungaji wa kanisa la kijiweni kuhusu madhara ya ulevi.

Wakati anaanza kukumbuka pia maoni ya wazazi kuhusu mambo ya anasa , KIMWANA MWANANA aliyekaa kwenye stuli ndefu pembeni ya baa akifyonza KILAJI akafanikiwa kurudisha ari mpya ya KIMIMINIKA na kilaji kikaagiziwa huku akikumbuka lakini sasa hivi NI kwa mbaali kuwa ; POMBE si CHAI.


Dakika chache baada ya kuwa akijaribu kutatua swala la hivi KIGOLI aliyempita yuko NUSU-uchi au uchi-nusu , akasikia sauti ya PAPAA MSULI ambaye ni kiongozi wa bendi ya MSULI PEKECHAPEKECHA akifoka kwenye KIFOKEO kwa msemo wake uliopo kwenye wimbo wake maarufu mpya,- alisikika akisema; ''GRISI kiunoni weka, MBINUKO pakua!'' na umati ukasikika ukijibu; ''MSULI pekechapekecha na MAkalio BINUA!'''
Mr Kibeberu akatabasamu mtabasamu wa kujua sasa shughuli imeanza!



Mr Kibeberu alifumbua macho na kuiona silingibodi anayoitambua kitu ambacho kilimfanya akenue meno kwa tabasamu la kujua alifanikiwa kurudi nyumbani SHWARI baada ya kimiminika a.k.a KILAJI cha kutosha jana usiku. Wakati anajaribu kukumbuka jinsi alivyofurahia jana usiku akashtuliwa na sauti ya kijambo pembeni yake na ndipo alipo kumbuka hakuja nyumbani peke yake.

Kwa haraka alistukia mpaka yuko uchi na kwa kawaida huwa halali uchi. Kwa mbali akakumbuka jana alikuwa anadansi na kimwana mwenye mwanya wenye ujazo mwanana.Na tabasamu likarudi baada ya akili yake kurudi katika mkao wa tamaa za fisi.

Lakini alipofunua shuka kumshuhudia KIGOLI, alipigwa na butwaa kugundua aliyelala pembeni yake bila nguo ni bibi kizee na hana meno. Wakati anajaribu kutafakari imekuaje yuko uchi na bibi kizee, akastukia gauni jekundu lililoko sakafuni linafanana na la yule kigoli aliyekuwa naye kwenye taa dimu mwenye bonge la mwanya mwanana na denda lenye uzito wa FRESH mtindi.

Ghafla moyo ukaanza kumdunda kwa spidi za sungura wafanyao mapenzi kwa kukumbuka jana usiku hakuwa hata na condom, huku akishindwa kuelewa ilikuwaje mapengo yalikuwa yanaonekana kama mwanya mwanana jana usiku!:-(


HADITHI IMEISHA!

Swali:

  • Unakumbuka pombe si chai?
  • Unakumbuka kumlinda na kujilinda ingawa wote tumekusikia ukitangazia umati HUFANYI uasherati?
  • Bado huongelei ngono na kondomu kwa sababu si utamaduni wetu ingawa uwapendao wanaendelea kufa kwa kutokujua?
  • Unauhakika kama umesoma mpaka hapa, huu sio ujinga ulioandikwa hapa?


BAADAYE!.....
Hebu tutulie kwa kushuhudia mtazamo wa HARUSI ya dada na dada katika- SOAP'S FIRST LESBIAN WEDDING..


Au ngojea CYPRESS HILL wazungumzie wao mtazamo katika - Under Mi Sleng Teng

Monday, February 16, 2009

NI KAZI YAKO au chaguo lako?

NAJUA uko kazini hata kama huna kazi!


WAKATI unafikiria hiyo kazi ya kuwazia kazi, ....
..... kuna uwezekano bado kuna chaguo la KUENDELEA NAYO au KUENDELEZWA NAYO.


Kuna uwezekano kabisa ni KAZI INAKUFANYA wakati wewe unafikiri unaIfanya kazi!:-(



Narudia swali:

  • Hiyo ni kazi yako ILIYOKUCHAGUA au ni chaguo lako la KAZI?


Labda hiyo kazi sio chaguo lako kama tu lisivyokuwa chaguo lako kuwa wewe ni mtoto wa RAIS MANDELA na lingekuwa chaguo lako ungetaka uwe mtoto wa RAIS LOWASA.:-(

Lakini kama sio chaguo lako katika mkao wa HALI HALISI uliyonayo , bado naomba tena kukuuliza SWALI:
  • Unauhakika hiyo ni kazi yako au haikua chaguo lako na ni kazi kwako?

  • Unauhakika ingekuwa ni chaguo lako ungetaka uzaliwe katika dunia hii yenye mpaka gono?

NAACHA!
Ngojea Mory Kante aendeleze tena katika- Yeke Yeke

Sunday, February 15, 2009

Nimecheki jana na UKWELI ni kwamba nina UKIMWI!

Ukweli ni kwamba sijacheki jana ingawa nacheki mara kwa mara labda kwa kuhisi nipewavyo katika kupakua MARA NYINGINE labda NINAPAKUA zaidi kama WEWE katika staili ya KUJIJAZIA.:-(


Swali:

  • Hivi kama KESHO nikicheki tena halafu ikawa ni KWELI kuwa NIna UKIMWI kama MHESHIMIWA naNIhii, UTAJIANDAA KUKATAA kunipa ingawa sitarajii KUKUOMBA unisaidie NANIHII?

  • SI unakumbuka kuwa UKIMWI ni ugonjwa tu kama BERIBERI na kwa ujanja wako unaweza UKAWA umeishi SANA kwa kukwepa mpaka ugonjwa wa MDONDO halafu ukawa huoni NISHAI kujinyea ingawa NI KWELI kwa ujanja wako umeishi mpaka UKAzeeka SANA na hukumbuki choo wakati UNAJINYEA na si mjanja?
  • Hivi ulikumbuka kucheki jana?
Nakushauri ucheki hasa kama umepata LIMPENZi jiPYA na unahisi mnaweza kutaka kuishughulikia SHUGHULI bila VIATU.

Cheki pia kama ulishakuwa hata katika ajali ya mkokoteni ambayo ulijeruiwa wakati uko na MAJERUHI.

Cheki pia kama katika uteja wako wa magonjwa unawasiwasi na sindano zilizotumiwa kukupa ugoro.

Wakati unacheki kumbuka mtoto wa mjini HIV ukimdaka leo kwa kawaida hata mwezi ujao na mbili haonekani, kwa hiyo rudia tena kabla hujajinoma bila viatu angalau baada ya miezi mitatu.


CHEKI TU ila jiandae kabla ya kucheki kwa sababu jamii imezoea hata kutisha watu kuhusu KIFO mpaka imetisha watu kucheki MDUDU, wakati ukijua mapema unaweza mpaka kupanga maisha yako vizuri na labda badala ya kuhangaika na maboksi ungeweza kurudi kijijini kwenu MVOMERO ukacheze mkulanga katika kufurahia maisha kivyako.

Inasemekana wengi wasambazao UKIMWI kwa makusudi ni kutokana na kwamba hawakujiandaa na baada ya kujua wanafanya yao ya udhaifu ambayo ni kufikiri inalipa kufa na watu.

Kumbuka aliyedaka UKIMWI sio lazima maana yake kafikia mwisho wa maisha na HAJINOMI.
Swali:
  • Unafikiri kwanini kuna aogopaye kucheki mdudu kwa kudhani ATAJUA atakufa wakati kuna wajitoleao kufa kwa ajili ya dini ambazo cha maana zifanyazo ni kuahidi YASIYOJULIKANA?
  • Unajua inawezekana unao kama ni kweli bado hujacheki ?
NAACHA!
Baadaye basi kama SIJAFA au HUJAFA!

Au ngojea tena Tender Mavundla atusaidie tena...

NIPE KIDOGO NIchangamshe DAMU!

Lakini.....
.....kabla hujatoa SI lazima ulipata wakati unafikiria labda unipe!:-(


Na....
..... WAKATI unatoa ni kweli ULIKUWA NACHO ndio maana unanipa na sio KWELI unanipa kwa UKARIMU tu.

Wakati unanipa UKWELI ,......
........chakusikitisha ni kwamba hakuna UHAKIKA unanipa NINI na kwamba ni kweli ni UKWELI kama siamini ni UKWELI.

Na ni kweli,....
.....LABDA wakati unafikiri unanipa KITENGO labda ni kweli unatembea huku umebeba mzigo wa MAUNGO kitumbua.


Kumbuka,....
....KUNA busara za kutua mzigo hata kama mzigo wako ni moja ya KIUNGO kwenye mwili.


Swali:

  • Hivi ni kweli unafikiri damu inahitaji kuchangamshwa?


Na,...
.... wakati damu INACHANGAMKA,...

............. jaribu kuwa na uhakika uko na watu wenye undugu na ADAMU na EVA katika ya KIBINADAMU na ya MUNGU muachie MUNGU uchangamke.

Swali:
  • AU?


JUMAkumi NJEMA!

Ngojea Michael Jackson na Britney Spears waseme....

AU tu RICHIE SPICE amzungumzie -GHETTO GIRL....

SAMAHANI ngojea basi SHABBA RANKS amalizie na -COOL COOL......


ASANTENI TENA WADAU WOTE!

Au ngojea niwaache TENA na picha zangu na baadhi ya WADAU niliofanikiwa kuwadaka hivi karibuni ya JUZI YA JANA....

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Friday, February 13, 2009

BAADA ya kuamka na KABLA ya kwenda KUKOJOA!

SIKUBISHII....
...... ukisema ASUBUHI katikati ya muda kati ya ULIPOAMKA tu na muda ulipoenda chooni KUFANIKISHA kwa mara ya kwanza, hakuna ulichofikiri.

Ingawa naweza KUJARIBU kukubishia kwa hoja angalau ya kwamba baada ya kuamka na kabla ya kwenda chooni angalau ulifikiria kwenda kukojoa,.....

...... unaweza ......
.....kudai kawaida yako ukiamka tu hubanwa na kiu ya maji na sio KUBANWA na shehena ya HAJA-msalani, hata zisizohitaji maji!:-(


Lakini .....
.......labda kuna kitu huwa unafikiria katikati ya safari ya kutoka kitandani kwenda choooni ukiamka TU , ingawa unahisi huwa unapiga MMMMHH-ayo TU ,bila kufikiri kwa sababu umeamka na umekenua MDOMO katika miondoko ya kujinyosha.


Kumbuka lakini kuwa ,.....
..... baada ya kuamka UKIKOJOA, umekojoa mkojo uhitajikao na daktari , DAKITARI akitaka kujua AFYA YAKO kupitia wako MKOJO kama sio kucheki chako kinyesi ambacho kama WEWE ni mbunifu wa kibebeo ,KINYESI huwezabebeka kwenye kiberiti.

Lakini asubuhi pia,....
......kuna wenye bidii mpaka ya kutaka kukipa KITENGO ujauzito ingawa ni kweli hawajaAMKA vizuri na kwa maajabu ya Musa, KIUNGO NANIHII cha mwili kimeamka na kinafikiria VIZURI ingawa hakina ubongo wenye akili.


NA ni kweli kuwa ....
.... akili yako kabla HUJAAMKA sawasawa inajua zaidi KULIKO ukiamka VIZURI na kuanza KUDHANI unafikiria zaidi kwa kuwa umeanza kufikiria:
  • Shule
  • Utakula wapi
  • Mnuno wa Bosi
  • Utakavyo mchekea mesenja
  • Kubeba maboksi
  • Hawala sijui atapiga simu?
  • Mchezo sijui utakuaje.
AU......
  • hata utachambia nini na nakadhalika tatu na nusu.:-(


Swali:
  • Lakini si umeamka?

Endeleza tu Mkuu kama umeamka na sio mzuka wako tu ndio UMEAMKA!

Kumbuka lakini kwa kuwa macho unapunguza uwezo wako wa kufikiria mengi kwa sababu KUNA ambayo unayapa kipaumbele kwa kuwa macho.

Labda.....
....... wakati UMEAMKA na uko MACHO kwa kuchunga POCHI, mwanawani unasahau kuchunga CHUPI.:-(


NAACHA!
MIe NAWAZA TU HAPA!
Tuko Pamoja!
WikiENDI njeMA!

Nakuacha na Mr VEGAS akisema -Nuh Want No Fren From Dem na Tek Weh Yuself..(Tahadhari kama mkwazikaji au mtoto halafu msikilizaji ,kuna mambo ni ya wakubwa:-()



Au tu Eminem ft. Dr.Dre & 50 Cent wadai - Crack A Bottle....(Tahadhari lugha kama mtoto au mkubwa akwazikaye na lugha.Kuna mambo ni ya wakubwa:-()

Thursday, February 12, 2009

BADO nina wasiwasi na URAIA wa RAIS NYERERE!:-(

KWA sifa anasifiwa na RAIA,...
.....mpaka na VIONGOZI wamwitao MWALIMU.


KAMA wanafunzi-WASIFIWA ni RAIA,....
...... wadai ni ujanja kudai wafanya ya MWALIMU,
.....mbona .....
ya WANAFUNZI-viongozi RAIA,....
..... wafanyayo HAYAFANANI na ya MWALIMU?


Labda tatizo ni mmoja haleti URAIA,.....
...... kati ya hili mwanafunzi au yule MWALIMU.

Kwa sababu WANAFUNZI wako hai na watajitetea URAIA,...
..... ngoja ni ridhike na wasiwasi wa URAIA wa MWALIMU.:-(

Na labda sielewi somo la URAIA,....
......yawezekana kufaidi nchi kiraia, yabidi kiufisadi uwe MWALIMU.

Kwanini Haleluya ni ya wote RAIA,....
......na AMEN yamfaidisha ambaye kwenye kitu TU ni MWALIMU?
__________________________________________________
Swali:

  • Kwani ni KWELI mwalimu alipatia mpaka wanafunzi wafuate ya Mwalimu?

NAACHA UJINGA!:-(

SIKU NJEMA ,au tulia tu na yasio SIASA kama ya WYCLEF akiongelea ya msichana katika- Guantanamera

Twendeni KUMTUKANA RAIS!

Wakati tunajiandaa kwenda kumtukana RAIS,.....
.......... tukumbuke tu kuwa SHAMBA BOY, mtumishi na pia aongozwaye na RAIS kasha tukanwa, anatukanwa kila siku na labda anatukanwa na RAIS.


Utamu na BURUDANI tofauti ya TUSI KWA RAIS ni jinsi ipewavyo UZITO TOFAUTI TU kwa sababu atukanwaye sasa hivi ni RAIS .


Kama RAIS ni mtu kama HAUSIGELI wa RAIS, usishangae kuwa labda ushamtukana Rais bila kufikiria umtukanaye ni RAIS kwa hiyo huhitaji sana kujiandaa sasa hivi kumtukana RAIS.

Au niibe msemo wa Obama katika lugha ya Kiswangliung'eng'e: ''YES WE CAN tukana'', na ukweli ni ''YES tume ZE tukanwa''!

Unaweza kubisha , lakini tusi ni jinsi tu utafsirivyo tusi.


NA...
.... katika KUJIPENDEKEZA KWA RAIS labda ndio aina moja ya tusi kwa Rais kwa KUMSIFIA KAMA ANAWEZA wakati unajua umahiri wa RAIS mpaka sasa hivi umebobea kwa alioshindwa na anayoshindwa kama Rais kiurahisi.


Swali:

  • Kwani sifa za uongo apewazo RAIS sio MATUSI rahisi katika jeduali la MATUSI?

MSIFIE tu RAIS kama HUFIKIRII hizo sifa si kipenyo kwenye TUSI mduara kwa RAIS.

Lakini wakati unamtukana Rais,....
......inawezekanaMWENZIO bado anaendelea kula KIURAHISI!:-(

Nakutakia KILA la kheri wakati unamtukana Rais tusi limfikialo Rais na linasawazisha afanyayo RAIS kwa kukuletea AHUENI sio katika kufaidi kutukana tusi TU kirahisi!

Matusi huhitaji SHABAHA na kulenga tusi kwenye kishimo katika matusi si rahisi!

Swali:
  • Hivi unajua kukokotoa kipenyo cha tusi katika kujua nguvu ya tusi kwa Rais ?

  • Si unauhakika kwa kutukana umeshatoa stimu na unasikia ahueni kwa hiyo Rais anaruhusiwa kuendeleza andelezacho mpaka utakapo mtukana tena baadaye kwa kuendelea kushindwa URAIS kirahisi?

  • Unauhakika simuongelei Rais wa shule ya vidudu hapa?


NAAACHA!

Nawaza tu hapa kumbuka!
Tutulie kwa kwenda Gabon kwa Oliver Ngoma katika nanihii ya- ICOLE...



Au ngojea nimuachie..JACKY RAPON aendelee kulainisha kwa Mi amor.....

KAMA nikiendelea kukuomba NINYIME au MNYIME tu kama INAMSAADA ukinyima!

Ingawa labda NIMETAKA MWENYEWE, kwa kutaka inamaanisha labda sio changu na KINA WENYEWE.

Ingawa unaweza kuomba upewe chako kistaarabu,......
....kumbuka MTOTO akiomba viumizavyo au vimdhuruvyo MTOTO, wampendao MTOTO humnyima MTOTO hata TAMU KUNOGA.

Nakubali,.....
.....TOTO likikua linaamini kuwa ni TOTO KUBWA na linajua jinsi ya KUSHIKILIA liombacho katika STAILI YA KUKIFAIDI MNYONYO kwa dhati , kwa hiyo linafikiri likiomba linahaki LIPEWE tu YOTEYOTE!:-(

Swali:

  • SI unakumbuka ingawa sukari inaonekana safi kama sukari lakini SUKARI inaweza ikawa imeingia SUMU?


Tukumbuke tu toto la bata wakati linatembea bila KUHARISHA , kuna uwezekano mkubwa kuna wenye busara wajuao ukweli kuwa BADO TOTO LA BATA lina mavi katika mwendo ingawa sasa hivi halinyi.

NA....
.... kama ningekuwa au angekuwa MTOTO ungemnyima kwa kuwa KUNA KITU UNAJUA, fikiri mara mbili kunipa au hata KUMPAKULIA mwenzio NANIHII akiomba, ingawa anaonekana mkubwa na ANATAKA MWENYEWE nonihino.

Swali:

  • Si ndio UTU huo jamani?
  • AU?
Usije UKAMPA na KUMUUA mwenzio jamani!
UNYIMI ni utu mara kadhaa katika maisha haya magumu!

Swali:
  • AU?
  • Kwani NI kweli wewe unaroho mbaya kwa sababu hugawi?


NAACHA!

Hebu tubadilishe hali ya hewa na kumsikiliza BILL COSBY aongelee watu weusi.....katika -MEET the PRESS


AU ngojea Mike DYSON naye alete mtazamo wake wa watu weusi.....



DUH!
Ngojea turudi tu ZIMBABWE kukutana na BONGO LOVE waendeleze uafrika.....

Wednesday, February 11, 2009

SAMAHANI kama bado sijafanikiwa KUKUKOSEA Mpenzi!:-(

MAPENZI bila kukosea,...
..... ni kama KWENDA haja kubwa bila mguNO.


NA katika ufundi wa kukosea,....
..... si LAZIMA penzi likatikiwe kiuNO


MPENZI utanogewa,....
..... kama ni TAMU na makosa yanaruhusiwa katika mavuNO.

NA kama unanogewa....
........kwa sababu bado sijakosea,
.................JIHADHARI na karatasi mwenzio nina peni yenye wiNO.


MPENZI samahani kama bado sijakosea,....
....... na jihadhari na JEMADARI awezaye yote bila kukosea
............wakati wajua hakuna binadamu ajuaye mNO hata mguNO.
_________________________________________________________________
Swali:

  • Hivi wewe bado unanogewa kwasababu HAJAKOSEA au hata akikosea hustukii kwa sababu penzi bado LIMEKOLEA?


SIku njEMA!


Tutulie kwa kwenda tena NAMIBIA kwa TATE BUTI...wakidai..- Oshitenda

UDHAIFU wa utakatifu wa MTAKATIFU SIMON KITURURU kabla hujamdaka AKIFANYA dhambi!

Dhambi unaweza ukawa umeishikilia kiuno huku unakataa HUIFANYI dhambi.

NI kweli....
....wakati unamtetea MTAKATIFU, dhambi ya mtakatifu huelezeka kwanini yenyewe sio dhambi.:-(

Kubwa zima bado linaweza kukwambia lina uhakika duniani kuna mtakatifu asiye na dhambi ingawa liko kwenye dini ziaminishazo UMATI kuwa hata toto lililozaliwa sasa hivi limezaliwa na DHAMBI ya ASILI na lisipobatizwa halitaenda kucheza mdako mbinguni.

Bin-Adam katika utaalamu wakutenganisha dhambi na sio dhambi ni mpaka lifundishwe na limtu jingine nini ni dhambi na katika hamu za Binadamu kuwa hana dhambi likikuamini wewe basi dini yako inakuwa ya kweli kwa sababu ndio itakuwa kirahisi imeshushwa na Mungu ingawa Mungu pia anahitaji tafsiri kabla hujakaririshwa ni yupi wa KWELI.

Mtakatifu Simon Kitururu labda dakika hii hana dhambi kama unaamini katika sayansi ya KUTUBU bila kutoa sadaka dakika chache baada ya kumalizia dhambi huondoa dhambi.

Swali:

  • Tukiachana na mtakatifu Simon Kitururu sasa hivi , una uhakika wewe huna dhambi?
  • Unauhakika tokea mara ya mwisho ukutane na Simon Kitururu bado hajapata utakatifu na hana dhambi mpaka baadaye kidogo?
  • Unafikiri mtoto wa mjini SHETANI alikuwa ZOBA kiasi kwamba hakujua Kijeba Yesu alivyo karibu na ya Mungu mpaka akaendeleza kutaka kumjaribu Yesu afanye dhambi?


NAACHA mahubiri kwa sasa!
Kumbuka NAWAZA tu hapa na kama unadhambi ambayo ukitubu dini yako inakupeleka mbinguni TUBU tu kivyako !Kumbuka labda hatutapanda basi moja kwenda mbinguni!

Ngojea tukutane tena na Yesu wa KILATINO Jose Luis de Jesus Miranda akumbushe kitu


Au R.E.M waongelee- Losing my Religion...

Tuesday, February 10, 2009

TATIZO la kuogopa KUONGELEA nanihii!

Labda BADO unasema na kuongea kwa KUKAA kimya!
CHAKUSIKITISHA ni ukweli kuwa hata wasemao hawaeleweki NDIO MAANA kuna BINADAMU wakagundua KUJIELEZEA.


TATIZO la kuogopa kuongelea laweza kusababisha watu kudhania KIJEBA ni BASHA kumbe ukweli wenyewe ni kwamba KIJEBA ni MSENGE!

Na katika kuogopa kuongelea,......
.....unaweza kusababisha MUISLAMU aendelee kuwa MUISLAMU na MKRISTO aendeleze UKRISTO kwa kushindwa kwako kutetea uishivyo KIPAGANI wakati unajina la KIHINDU.



USIPOANGALIA unaweza mpaka KUFA NA NJAA kwa kogopa KUONGELEA NJAA!

Swali:

  • Hivi unaogopa kuongelea tu au hata KUSIKILIZA HUSIKILIZI?

  • Kama UNACHAKUONGELEA unauhakika UNAWASIKILIZAJI?



USITISHIKE!

Labda unaamini huna cha KUONGELEA ndio maana UKO KIMYA!


Kumbuka tu kuwa hata PADRE , ASKOFU, SHEKHE na hata mganga wa kienyeji HAWAKOSI cha KUONGELEA kwa kustukia tu kama ulivyoSTUKIA kuwa kama huna vyako vya kuongelea unaweza ukaongelea vya MUNGU na kuna vitabu unaweza kukariri mistari ilikuongezea UAMINIKAJI wako katika KUONGELEA STORI uwashauriyo wengine wasifanye ingawa wewe bado unayafanya au angalau dhamira yako YAKUFANYA ipo na inakusumbua.

Na wakati hutaki kumuongelea MALAYA ,bado kama unavutiwa na uzuri wa MALAYA twaweza kustukia unavutiwa na MALAYA kwa sababu MALAYA mhusika ANAVUTIA hata labda si kwa UMALAYA ndio maana UNAVUTIWA.


Kumbuka tu kama UNAPUMUA ukipenda unaweza kuanzia kuzungumzia PUMZI katika KUONGELEA.


KUMBUKA tu;.....
......CHOCHOTE ni STORI kama unataka kiwe STORI.

Swali:
  • SI kama una roho nzuri utapenda kujua kama wengine watasaidiwa kuendelea HATA kupumua kwa kuwa UMEONGELEA SWALA ingawa unasita kuongelea Swala au NGURUWE?
  • Unauhakika huna tatizo la KUONGELEA ingawa laweza kutafusiriwa kwa neno UMBEA kama bidiii ZAKO za kuongelea zimezidi?

NAACHA!
NA kumbuka NAWAZA tu hapa nachojaribu KUONGELEA ingawa kinaweza kisieleweke ingawa NAKIONGELEA!:-(

Tuburudike kwa kuangalia HABARI MUHIMU kama ya Rais Obama kujigonga kama ni burudani , kama iletwavyo na chombo cha habari za maana cha CNN........


Au ngojea Sluggy Ranks azungumzie - Sodom & Gomorrah

Au ngojea tu Papa San alie tena .....katika - maddy maddy cry ... (sikiliza kwa hiari yako mwenyewe mie simo....!)

HAKUNA kiletacho maana kama hudhani KINALETA maana!

Binadamu wakagundua mpaka dini katika kujaribu kusababisha ilete MAANA.

Usipoangalia mpaka unaweza kudhani inaleta maana!:-(

Swali:

  • AU?

Kama HULII sasa hivi KUNAUWEZEKANO kuna kitu UMESAHAU!:-(

Kumbukumbu za utamu zinaweza kukusaidia KULILIA mpaka MTU.
Maumivu yanakuliza wakati unaumia lakini kumbukumbu za utamu zinaweza kukuliza wakati unakumbuka hata penzi lilivyowahi kuwa tamu.

Lakini.....
.....KUNAUWEZEKANO kabisa wakati unakumbuka kitu KUNA kitu unakisahau!

USIPOANGALIA unaweza kusahau KUKUMBUKA KWA MAKUSUDI kwa sababu kwa kisiri kuna KITU hutaki kukikumbuka sasa hivi.

Tatizo ni.....
..... hata usipotaka kukikumbuka kama kipo, KIPO TU na kinakusubiria chobisi!:-(

Na ni kweli hata masikini anaweza kupitisha siku bila kukumbuka kuwa yeye ni masikini ingawa ndani ya siku anapambana na kitu ambacho mtu mwingine atatafsiri ni mapambano ya umaskini wakati kwa mtazamo wa maskini anajaribu tu kupitisha siku kala chakula na labda pakulala papo.


Inawezekana kabisa masikini anajitahidi kuishi ndani ya siku na MUDA MWINGI ndani ya siku ya kimasikini MASIKINI hataki kukumbuka kuwa yeye MASIKINI.

Inawezekana kuwa si BUSARA kumkumbusha masikini kuwa yeye masikini kama vipimo vyenyewe vya utajiri haviaminiki.

Swali:

  • Unafikiri tajiri sio masikini?
  • Unafikiri kwa sababu LEO HULII hakuna kikuumizacho ?
  • UNAuhakika sababu za kutokulia kwako sio tu UZOEFU wako wa kulea maumivu?


Wakati MAKALI ya yaliyowahi KUTULIZA hatuyasikii sana sasa hivi, kuna uwezekano kuwa yamezidi na TUMEZOEA TU MAUMIVU!:-(

NAACHA!
SIKU NJEMA!

Tulia tena na Russell Peters katika- SHOW ME THE FUNNY....


Au tu Curtis Mayfield arudie - Superfly Live

Monday, February 09, 2009

NIMECHACHA!

Naomba!
Labda niliomba!
Bado nahitaji ingawa si poa kwa mtazamo wako KUOMBA ndio maana LABDA unakumbuka zaidi ukiombwa.:-(

Swali:

  • Unakumbuka ?
  • SI nimewahi KUKUOMBA?
  • HIVI unauhakika Ushawahi KUOMBWA au unajisikia tu UMEOMBWA kwa sababu katika TAFSIRI yako nimekuomba?

Naendelea KUHITAJI mwenzio ndio maana mpaka najaribu kukumbuka kuwaomba mpaka wajanja kuliko wewe ambao MJANJA aita mmojawapo MUNGU!:-(

WAKATI naleta JEURI ya KUOMBA najua UNAkumbuka NA unajua inaruhusiwa KUNYIMWA!:-(

UNYIMI ni SANAA !
UNYIMI inaweza kuwaBURUDANI!



UNAWEZA mpaka UKAKOSEA KUNYIMA mpaka ukamnyima ASIYE HITAJI na hakuomba hata MAENEO kwa nia ya BURUDANI!:-(
Swali:
  • UNAUHAKIKA nimechacha kwa sababu kuna KUCHACHA katika BURUDANI?
  • Si unakumbuka kuchacha zaidi hasa kwenye UKAME wa NANIHII ndio maana hukumbuki starehe ya KUWANACHO kabla hujafikiria au kukumbuka burudani ya KUCHACHA?

Katika utaarabu wa KUCHACHA unaweza mpaka ukastukia na kuelewa BUSARA ZA WALIOCHACHA katika BURUDANI usipoangalia!:-(


NAACHA!
Samahani lakini kama ulishindwa KUNINYIMA BURUDANI wakati ulinipa wakati UMECHAHCHA!:-(
Tutulie na OJ MASAI A LEADER WHO KNOWS EVERYTHING. GTV

AU Tulainishe ya ALLAH katika ALLAH HOOO (GOD IS ONE) na USTAD NUSRAT FATEH ALI KHAN katika miondoko ya MUZIKI aina ya QAWWALI.....

AU tuendelee tu na JAMES BROWN olympia mwaka 1966 .....

Katika KUSHUGHULIKIA shughuli!

Kama uko HAI ni lazima hata kama HUTAKI unashughulika!:-(
Katika kushughulikia hata UJINGA ni SHUGHULI.
Na....
....katika kushughulikia shughuli mpaka Yesu aliwahi kuuawa ingawa shughuli za kufufuka kwa MADENGE alivyokufa inahitaji IMANI katika shughuli ya IMANI.
Swali:

  • AU?
  • Si unakumbuka SHUGHULI inaweza kukushinda au IKAKUTONESHA katika SHUGHULI?
Kumbuka kuwa LABDA kuna ukweli kuwa SHUGHULI inaweza kushindikana KISHUGHULI.:-(

NAACHA!
BAADAYE basi!
Asanteni wadau WOTE !
Ngojea tutulie katika shughuli wakati AMY SEDARIS akitukumbusha baadhi ya SHUGHULI zioshwavyo....

Au tu VYBZ KARTEL na marehemu NATASJA waongelee SHUGHULI au UMBEA katika- Talk of THE TOWN(TAHADHARI LUGHA kama wewe mtoto au mtoto KIkwelikweli kwenye SHUGHULI!)

ASANTENI pia WADAU ambao tulikuwa pamoja JUZI YA JANA katika SHUGHULI ambao baadhi kamera yangu iliwadaka katika SHUGHULI kama hivi.....






Photobucket

Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket



Photobucket





Photobucket

Photobucket

Photobucket




Photobucket



Photobucket


Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket




Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket


Friday, February 06, 2009

Kwa MPENZI sura ya MALAIKA! Tupande KIBAJAJI mwenzio BENZI sina!:-(

Kwa mpenzi Midomo Mizuri!

Dhumuni la barua hii si kukujulia hali tu , bali na kutaka kuharakisha safari ya penzi letu ifikie pale niaminipo nimelipata penzi lako kiuhakika ili mwenzio niache KUKUDANGANYA.

Mpenzi Midomo Mizuri kama ya bata, ni kweli nikikuona moyo unapiga mdundiko na kwa jinsi macho yako malegevu yanavyoniwashia indiketa kuwa ni zamu yangu kupita, napata mshawasha wa ari mpya na nguvu mpya yakufika nawe faragha tukafanye ya faragha. Lakini pia indiketa ziniambiazo hii ni zamu yangu kupita zanikumbusha kuwa labda aliyetangulia alizionja zabibu hizo kwa mitindo ambayo mimi siwezi kuchuma zabibu.:-(

Mpenzi naombea ningezaliwa enzi zile wazazi na kijiji kizima wangekujua zaidi kuliko mimi na kazi yangu ingekuwa ni kusikilizia ni lini wazazi wangu watakutana na wazazi wako katika kunirahisishia ujio wako maishani mwangu tule zabibu.

Mpenzi midomo mizuri, mwenzio na wasiwasi pia kuwa hupandi baiskeli, ingawa Phoneksi yangu iko pimped na nyuma imeandikwa maandishi kwa lugha ya kisasa ''NO SWEAT''! Tetesi hizo nimezipata baada ya kusikia hata VIBAJAJI hupandi na ulishawahi kumtukana Kamanda aliyekuja kichwakichwa kukuchukua na PICK UP kwa kudai kuwa kaja na gari la kubebea majani ya ng'ombe na sio kumpakia Kisura Midomo Mizuri.:-(

Mpenzi katika barua hii naomba kukiri kuwa nahitaji huruma yako ili niache kukudanganya. Nafikiri inabidi nikiri tu kuwa hii misuli sio ya gym bali ni ya kugonga kokoto. Na suti yangu ya Kaunda sio fasheni bali ni kweli ilikuwa ya Kaunda na nilipewa na hausiboi wa Kaunda tuliyekutana na kuzoeana katika mikutano na semina za mahausiboi za kuboresha jinsi ya kumnyenyekea akupaye kazi kubwa kwa mshahara mdogo.

Na nimeshauriwa niendelee kukudanganya kwa kuwa inajulikana kuwa WEWE unafurahia sana mdanganyo kwa dhati, na wenye busara wanaendelea kudai kuwa nikikuambia ukweli hatua ya ndoa hatutafikia . Na unajua tena mwenyewe dunia tuishiyo kwa wastaarabu kama sisi wa dini za kupokea kutoka kwa wageni kistaarabu , tendo la ndoa linahitaji refa au libarikiwe na Padre au Sheikh kabla hatuja likokotoa kistaarabu.

Mpenzi Midomo Mizuri, wakati najisikia kukuambia ukweli, ngojea nikiri pia kuwa ni kweli sio kila siku unapendeza na ukiniuliza kuhusu nguo zako nijuazo unazipenda kuwa zimekupendeza ,nalazimika kukudanganya kuwa ni kweli zimekupendeza. Ni kweli pia unanuka sana mdomo nikigongana na wewe asubuhi na tako lako halitingishiki ukitembea kama nikusifiavyo. Samahani kwa kukiri PIA kuwa hizo ni baadhi za vitu vinivutiavyo kwako sana tu ingawa nasikitika kujua unavikimbia kwa kupiga mswaki na kujaribu kwa nguvu na nusu ya ustadi kutingisha makalio.

Kabla sijamaliza barua hii ningependa kukuomba angalau leo nijitahidi kuja kukuchukua kazini mwako na BAJAJI. Ni matumaini yangu utachukulia huu ni utani na utapanda bajaji twende kwenye nyumba husika karibu na Shekhe alipo nikiwa na tumaini labda tutafumaniwa kwenye mkeka na kufungishwa ndoa ya mkeka maana hela za kitchen pati , begi pati na hata Fweza za harusi ya kuhalalishia watu au kujulisha umati tendo la ndoa RUKSA na labda tunalifanya KIMANDINGO sina !:-(

Nimatumaini yangu kabisa baada ya kusoma barua hii utatabasamu kwa kuzani si kweli ni kwenye BAJAJI na sio kwenye BENZI ndio matarajio yangu tutaanzisha ukurasa mpya wa PENZI. Hali halisi MPENZI ni kwamba bado niko kwenye hatua ya BAJAJI ya kukodi ingawa nina PENZI LA KWELI pamoja na kwamba nilikudanganya ilikupata sikio lako lililozoea kusikia utamu wa asali kuliko wa ndimu. Nasita pia kukiri ukweli mwingine kuwa mwenzio hata ndoto za Benzi sijafikia Mpenzi.

NAKUPENDA Mpenzi Midomo Mizuri Cheusi Dawa Mwanambilimbi!
Nakupenda sana na naahidi kukupenda kwenye CHEUSI na hata kwenye MKOROGO!
Pata basi busu la kikohozi cha bata MPENZI na kwa mapenzi usiteme!
Nakuahidi nitakuwa mwenye juhudi za kujitolea kwenye shughuli za faragha mpaka kitengo kitapata ujauzito tu Mpenzi!

Nitunzie nafasi angalau ya kigoda kwenye moyo wako Mpenzi!
Tutaonana basi mbele ya ofisi yako ukitoka ofisini tukaendeleze ule mpango vipi!
Au vipi Mpenzi!

Wako katika penzi ,
MPENZI.
--------------------------------------------------------------------------------
Swali:
  • Unauhakika Mpenzi ni nini?
  • Unauhakika husemi tu na ukweli ni kwamba huelewi penzi wala hujui kupenda ni nini ingawa unadai kwa juhudi mbele za UMATI unampenda hata Yesu au Mungu?
  • Unauhakika ni kwanini umeisoma hadithi hii ambayo labda ni ya kijinga mpaka sentensi hii hapa Mkuu?
Loh !Lione vile!:-(

Au twende tu na Kibajaji maeneo...:-)

AU?
Photobucket

Photobucket
NIMEACHA!
NAWAZA tu Mkuu hapa !
WiKIenDI njeMA!

Tutulie na NANKO arudie kusema.....-.LUCKY U


AU tu Pepe Kalle aseme....-HIDAYA..


AU tu Pepe Kalle aendeleze kwa kusema- Milla....

BUSARA zikizidi ni UJINGA na AKILI zikizidi ni UKICHAA!:-(

Kwa kawaida ni mwenye AKILI na BUSARA za wastani ndiye asifiwaye kwa kuwa na AKILI SANA au BUSARA SANA kwa sababu wenye AKILI SANA na BUSARA SANA hawaeleweki kwetu tuliozoea kutumia busara na akili ADOADO ilimradi siku inapita tukiwa katika majonzi au kufurahia NANIHII tuzipatazo kiADOADO!:-(

WENYE akili na busara sana hawaeleweki na wanaweza wakawa wameshajiua tayari au wanajiua sasa hivi kinamna kwa ajili yangu au yako kama sio kwa YALE tuyafanyayo.

Inawezekana lakini....
.... kama umezidiwa BUSARA , ukapunguza BUSARA ZAKO na usionekane kufanya UJINGA ingawa ukashindwa kupunguza AKILI ZAKO ambazo kwa bahati mbaya zinapungua zenyewe ukizipa MUDA WA KUTOSHA.


Swali:

  • Mtaalamu si unakumbuka kama utafanikiwa KUISHI VYA KUTOSHA akili zako za UPASUAJI WA UBONGO zitafikia kushindwa kukukumbusha KITANDANI si CHOONI?
  • Hivi labda si ni kweli unang'ang'ania AKILI na BUSARA hata zikupazo MAJONZI kwa kuogopa kuonekana HUNA BUSARA na MJINGA?


NA tatizo ni ukweli....
.... DUNIA INAENDESHWA na WENYE busara za wastani kama si za KIJINGA na WENYE akili za WASTANI kama sio chini ya wastani AMBAO KWA BAHATI MBAYA ndio wana eleweka NA WENGI.

Narudia....
... kwa mtazamo wangu,.....
.........WENYE BUSARA SANA huonekana WAJINGA na WENYE AKILI SANA huonekana VICHAA na kwa bahati mbaya hao wote hawako katika FASHENI YA KUSIKILIZWA wala KUELEWEKA.:-(

Swali:
  • Bado unaamini BINADAMU WOTE wameumbwa kwa mfano wa MUNGU?

NAACHA!
Kumbuka NAWAZA tu HAPA usitishike na wala sikuongelei WEWE!
Tutulie tena MTOTO ANUNE....

AU Ikiwezekana SAMBA MAPANGALA amalizie kwa kutukumbusha ...-Nyama CHOMA..

Labda YULE NI mjanja kwa kuanza JUZI na sio MWAKA JUZI!

Moja ya TATIZO la walioanza zamani ni KUZOEA SHUGHULI!

Na....
..... shughuli IKIZOELEKA afanyaye husahau kuwa wakati alivyokuwa anajifunza KUIKATIKIA SHUGHULI, ni kweli shughuli ilikuwa ni UJANJA.

Ni kweli....
...... walioanza MWAKA JUZI wengi wako kimya ingawa wanafanya SHUGHULI ingawa unayemsikia ZAIDI ni aliyeanza JANA.


Na ALIYEZOEA tokea karne ya juzi.....
.... anaweza kusahau unamsubiri kwenye FARAGHA akupakulie MAUNGO wakati hisia zako za KIUNGO zimeiva.

Na AANZAYE juzi....
......anaweza akakereketwa na alichoonja kwa MARA YA KWANZA JUZI mpaka akakusimulia visivyo simuliwa kuwa KAONJA visivyoonjwa.:-(

Lakini Swali:

  • Hivi aliyejua MWAKA JUZI unauhakika bado anajua utamu wa ILE KITU leo?
  • Hivi aliyeonja ile kitu MWAKA JUZI akionja tena leo, hivi HII KITU haina LADHA mpya?

Inasikitisha kukiri,.....
..... labda ajuaye juzi pamoja na MCHECHE WAKE WA ULENA, anasikilizia zaidi UTAMU WA JUZI aliouonja kwa SIKIO JIPYA na kwa mara ya kwanza kuliko MZOEFU ajuaye A,B,C za utamu tokea karne ya MWAKA JUZI!:-(

Tusisahau lakini kuwa kuna aina za utamu kama UTAMU WA BIA ambao huongezeka kwa jinsi UZOEAVYO BIA ,
......na labda pia,....
....... BIKIRA aliyeonja kwa MARA YA KWANZA JUZI katika kumbukumbu za utamu ni MAUMIVU au AIBU za aliyofanya BILA UZOEFU kwa mara ya kwanza JUZI!:-(

Swali:
  • AU?
  • Kwani unakumbuka UTAMU wa MAZIWA YA MAMA kama ulivyoonjeshwa miaka ya karne ya juzi?


KWAHIYO,.....
.... labda tusiMCHEKE aliyeanza juzi kwa kuwa msemaji MKUU WA ULICHOKIZOEA tokea KARNE YA JUZI kwa kuwa mwenzio labda bado ANAKISIKILIZIA USIVYOKISIKILIZIA tokea karne ya juzi , kwa kuwa kakionja kwa mara ya kwanza JUZI.

NA labda MUONJA juzi,....
.... utamu wa chakula cha juzi bado UPOUPO na ni utamu FRESHI, na kama WEWE hukula tokea mwaka juzi , wewe ni MFU nanikweli hujaonja vya JUZI kwa ulimi wa JUZI.

NAACHA!
Ngojea tena tujifunze kufungua SIDILIA katika -How To Undo Her Bra With One Hand...


Au niwaachie Ray Parker Jr. & Bobby Brown katika - Ghostbusters

Au turudi tu kwa Mtanzania a.k.a Freddy Macha atukumbushe Kilimanjaro na kuleta nguvu mpya ya kuendeleza siku....

Thursday, February 05, 2009

Labda AMINI tu kama huwezi KUHAKIKISHA!

Wakati unajiandaa kutotakakuhakikisha ili uamini;
Swali:

  • Hivi unauhakika MUNGU sio MWANAMKE?

Na LABDA unaweza usiamini tu kabla HUJAHAKIKISHA !:-(
Swali:
  • Si huamini ni kweli katika mwaka unalala karibu miezi sita ?

Na hata usipoamini,...
.... labda NDIO MAANA kuna kuamini kwa sababu ya UWEPO wa uwezo wa KUTOAMINI.
Swali:
  • Unauhakika wewe ni mtu na rafiki zako sio shetani?
  • Unaweza KUHAKIKISHA?
BAADAYE!
Samahani lakini kama nakukwaza NIWAZAVYO katika mtekenyo!:-(
Tulia basi na EDDY MURPHY ajaribu kumpa kauli OBAMA katika- Change is coming to AMERICA.......


Au tu BUNNY WAILER akumbushie tuta -RISE and SHINE...

LABDA mpaka leo kila AFAYE na AISHIYE kashindwa KUMALIZIA kwa sababu hakuna KILICHOMALIZIKA.

Kama wewe ni MTANZANIA unaweza kumshangaa hata NYERERE kwa kuishia katikati katika SIASA zake za UJAMAA NA KUJITEGEMEA, kwa kusahau INASEMEKANA hata aliyoanzisha YESU hayajamalizika kama tu ya MTUME na hata ya BUDDHA katika kutafuta NIRVANA au KUMALIZIA.

Na kama wewe unaishi, labda unaanzisha ambacho hakitamalizika au unaendeleza walichoanzisha MAREHEMU au MAREHEMU WATARAJIWA ambacho utafariki hakijaisha.

Swali:

  • Kwani kama marehemu walianzisha unafikiri waishio wanafanya nini kabla hawajaMAREHEMUKA?

  • Unauhakika MUNGU alimalizia kuiumba DUNIA kama mpaka leo bado inabadilika?


Unaweza kubisha!
Lakini....
.....LABDA alichoanzisha marehemu au aliyehai yeyote hakijaisha na kama kuna aaminiye kimeisha , anatafsiri nyingine ya kumalizika kwa kitu na SHUGHULI ZA kuondoa dosari aionayo katika adaicho KIMEMALIZIKA atadai hamalizii SHUGHULI ila au labda ANAFANYA UKARABATI.

Labda ....
......kwa aaminiye hata kuwa DUNIA na viumbe vyake MUNGU alimalizia kuviumba enzi hizo za zamani, basi mabadiliko ya DUNIA na VIUMBE vyake yaendeleayo kutokea KWAKE si matokeo ya MUNGU kuendelea KUMALIZIA na labda si UKARABATI.:-(

Swali:
  • Unauhakika ungekuwa unauwezo wa kuumba kiumbe chako ungetaka KIHANGAIKIE kula CHAKULA halafu KINYE?
  • Hivi inawezekana ni mbinguni ndiko Mungu atamalizia ukarabati wa liMTU MIMI kama sio MTU WEWE?
  • Unafikiri Kijeba na binti Halufani wakikamilika watahitaji kwenda MSALANI MBINGUNI?


Pamoja na kuwa kuna watakaodai :
  • Kwa sababu ulizaliwa , basi kuna Marehemu kadhaa walifanikiwa kumpa au kupewa mimba na kazi yao ilimalizika ndio maana leo hii kuna wanaoishi!

  • Simon Mkodo KITURURU kufikiria KAZI YA MUNGU YA KUUMBA HAIKUISHA ndio maana labda hata mpaka leo hii BINADAMU BADO TUNAKUNYA hapa mawazoni, ni KUKUFURU!
Unaweza ONGEZEA nakadhalika saba na nusu za mengine yote yawezayo kukupitia kichwani wakati unafikiria uendelee kunisoma au LA HASHA,.... kwasababu NI RUKSA udaicho na kuna watakaopingana na udaicho!


Swali:
  • SI wapo wajanja WADAIO wanaendeleza kazi ya YESU , Mtume MOHAMADI, BUDDHA, MRUNGU, hadi mpaka MBUYU MWANAMBILIMBI katika dunia hii ambayo kwa binadamu kila siku ni KUANZISHA , KUSHINDWA KUTUNZA na KUKARABATI kwa sababu HAIJAISHA?
  • Hivi kwa MCHORAJI kuna picha ILIYOISHA isiyofaa kupitishwa HATA BRASHI mbili-NNE ili kumalizia PICHA?


Sibishi!

Labda....
..... kazi za MAREHEMU walizoachia WALIMWENGU ni kuweka wazi tu nini kiendelee kufanyiwa KAZI na ndio sababu nyumba ILIYOMALIZIKA KUPAKWA RANGI inaendelea KUPAKWA tena RANGI , katika kuendeleza hata tudaicho MAREHEMU alimalizia KUPAKA RANGI!

Na unaruhusiwa kudai kila AFAYE na AIISHIYE kuna kitu ALIMALIZIA kama unauhakika HATA kwenye utumbo ukimsafisha MHESHIMIWA MAITI au KISURA ALIYE HAI hakuna makombo ya mavi ambayo hakumalizia kuyatoa katika SHUGHULI ambayo HAKUMALIZA:-(

DUH!

Swali:
  • Unafikiri umemalizia KUZEEKA?
  • Unafikiri maiti haimalizii KUZEEKA?

NAACHA!
NAwaZA tu HApa Mkuu USITISHIKE na samahani kama nimekukwaza!
Nakutakia kila la KHERI chooni!

Tutulie basi na mshabiki wa Yesu a.k.a ISSA , ROSE MUHANDO akumbushe waaminio- Baba nipe uvumirivu


Au twende tu tena Somalia kwa K'naan azungumzie -HARDCORE...

Wednesday, February 04, 2009

Swala la WEWE ni MZURI SANA na NAKUPENDA WEWE TU!

HAMU ya aliyesifiwa kutaka KUMILIKI aina ya SIFA aliyopewa JANA kutoka kwa LIMTU alipendalo , asipoangalia ataendelea kudhani sifa ile YA JANA ipo hata LEO wakati MTAALAMU hana sifa za jana LEO.

Labda....
.... kweli wewe ni mzuri, LAKINI limtu lako kama ni LIBINADAMU , inawezekana halikupendi wewe TU ingawa ukiliuliza bado lina busara zakukuambia;
''NAKUPENDA WEWE TU!''.

STAREHE ya kusikilizia SIFA kutoka kwa MPENZI ambazo usingependa MPENZI awe anazigawa ZE SIFA kwa wengine, usipoangalia UNAWEZA KUZIAMINI NA KUZIDAI sifa za jana LEO!:-(

NA ingewezekana....
.....kuna ambao wangetaka kuzinunulia BIMA sifa au angalau kuzisajili wawe na HATI MILIKI ili hata -ukienda mbele sendema , rudi nyuma sendema ,- sifa za mtaalamu ni zake hata nyumba iungue MOTO.

Swali:

  • Kwani wewe unampenda uliyemwambia tu unampenda?
  • Kama kuna usiyempenda unauhakika MAZINGIRA YAKIRUHUSU huwezi kujifunza kumpenda?
  • SI kuna watu wenye wapenzi maalumu kwa makutano ya gizani NA WANAPENDANA KWA YAGIZANI tu, na kwenye mwanga hatuwaoni?

LABDA ukweli ni....
.....unapendwa KAMA UNAPENDEKA ,lakini watu wengine wanapendeka tu kama wewe UMPENDAYE akiwapa NAFASI ya pendo waonyeshe maringo yao dingilidingili mpaka chini.

Swali:
  • AU?
PENZI kama vile DINI , mara nyingi ni swala la IMANI YAKO INAKUPONYA TU kama WEWE ni mtunza IMANI KATIKA PENZI ULILOPO kama tu dini uliyopo na sio HALI HALISI ukiijua HALI HALISI!:-(
Swali:
  • AU?
  • SI ni kweli unafurahia kwa sababu unaamini na LABDA hata ingekuwa ni kweli INAAMINIKA lakini huamini, bado usingefurahia MTEKENYO?

NAACHA!
Ngojea turudi tena kwa Waziri wa Utamaduni wa Brazil a.k.a Gilberto Gil anisaidie kusema -'Aquele abraço' / ' Back in Bahia '

Au turudi tu BONGO kwa RAY C asimuliye binadamu wajaribucho kufanya katika...-Na wewe MILELE

Kuhusu uwiano wa UCHAPAKAZI, uhodari na UMADHUBUTI katika kuonja na UKUBWA WA KIONJEO!

Kama daktari ALIYESPESHALAIZI kitu, KIONJEO hujua makubwa kwa KUONJA PADOGO.

LABDA utaaminishwa....
.... punje chache za wali zinaweza kukuhakikishia utamu wa sahani NZIMA ya WALI.

UNAWEZAPIA kuaminishwa.....
.....KUBWA ZIMA hutumia kiungo kidogo kuonja hata BOMBA LA MWILI.

LABDA NI KWELI....
....KIONJWACHO si lazima kiwe KIKUBWA kwa KIONJEO ingawa ulimi UONJAO ni mdogo kwenye BOMBA la MWILI.

Lakini......
..... starehe ya kuonja ni KWELI kama wewe ni MTAALAMU WA KUJIVUNGA , unaweza UKATEMA kama hupendi ULICHOONJA usipotaka kufaidi mabakibaki ya MTAPIKO.

LAKINI Swali:

  • SI TANZANIA kuna walioonjeshwa mpaka UJAMAA NA KUJITEGEMEA washindwao kutema WALICHOONJESHWA?

  • Si kunawalioonja UBEPARI BONGO na hawana KIANZIO na PA KUTEMA?

Tukumbuke tu ....
.... hata kubwa zima linukialo manukato au PAFYUMU bado mwilini lina NUKTA au kishimo kinukacho na MNUKO wake si PAFYUMU.

Na labda.....
..... kijiko kimoja cha wali usifiwao hakikuchotwa kwenye SEHEMUSEHEMU ya sahani yenye KABICHI na MAHARAGE yaliyochacha.

NI kweli kabisa labda....
.... shughuli yenyewe IONJWAYO ni KUBWA na kionjeo ni KIDOGO ambacho ndio kitu kisababishacho UJUE utamu wa ulipoonja tu wakati mbele yake kidogo ya PALIPOONJWA, si patamu kama ULIPOONJA.:-(
NAACHA!
NAWAZA tu mkuu USITISHIKE!

Ngojea Ze Comedy Tv Show watupe - Habari Ndio Hiyo....




AU ERIC B & RAKIM watukumbushe....-Don't Sweat the Technique

ASANTENI wadau wote ambao hamkunitenga mitaa ya juzi ya jana bila kumsahau Valentine, Raymond mtafungwa,Fide a.k.a Mtimkubwa, Aliko Mwakanjuki, Allan Karani na wengine wote ambao baadhi mko katika baadhi ya picha mchanganyiko zilizodakwa na kamera yangu hizi....

ASANTENI sana WADAU WOTE!
Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Tuesday, February 03, 2009

CHEKA BASI! Usitukasirikie wakati ALIYEKUKASIRISHA hajui kuwa KAHUSIKA!

TATUZI la tatizo husika,
.....labda ni kumweleza aliyeHUSIKA.

N
a hata leo ni siku HUSIKA,
...... kama UMENUNISHWA na bado hujamwambia MHUSIKA.

NA bado ni masika,
......hata kama hakuna mvua za MASIKA.

NA usituonee kwa kutufulisha SHUKA,
........wakati shughuli za KULITIA MADOA shuka hukutualika na HATUKUHUSIKA.

ETI kuniona unakasirika,
... wakati hata mipaka ya salamu SIJAVUKA!

MJULISHE mhusika,
........au usituzingue na mkasirikie ALIYEHUSIKA.

LIONE vile lilivyonuna mpaka sura lataka PASUKA!:-(
-----------------------------------------------------------------------------------
NIMEACHA!
NAWAZA TU hapa MKUU na labda wewe si MHUSIKA!



Au tu Jamiroquai wadai- Love FOOLOSOPHY....

AU Beenie Man feat Ms thing and Shawnna waendeleze ridhim ya maisha katika - dude remix(Tahadhari lugha kama wewe ni mtoto au msikilizaji)

TANGAZO na kijulisho: ZENS In Da HOUSE

Zens In Da House
05/02/2009


Zens will be playing soulful funky disco House from labels like Defected ,Hed Kandi & Ministry of Sound

Happy hour 7-8pm . Local beers 1800, Glass wine 2500


Find us in Mikocheni “B”at Exclusive Resort Opposite St. Laureate Int. School, Kwa Warioba, Msikiti street

CALL US ON +255 783671600

OR

E-mail:info@zensbar.com

Kama HUPENDI magimbi jaribu VIAZI ingawa MAGIMBI yanazoeleka!

Ni kweli....
......hata UGUMU unazoeleka baada ya KUJILAZIMISHA kama haukuui.:-(

Tatizo ni....
...... maisha ni mafupi na usipoangalia unaweza kujikuta unatumia muda KEDEKEDE kujaribu kuzoea HATA kula MAGIMBI kwa MLENDA wakati labda ungeweza tu kuishi zaidi kwa kula VIAZI kwa CHUNGA.

Kama vile tu USTADH na MLOKOLE awezavyo kuzoea kutukana baada ya kufanyia mazoezi KUTUKANA, mheshimiwa unaweza kuacha MATUSI kwa kujinyima MATUSI.

Kumbuka tu.....
....... utamu wa kujaribu KUZOEA kitu unaweza usiustukie kwa kutogundua HATA ni siku gani hasa ULIYOHITIMU kuzoea.

Swali:

  • SI unakumbuka unaweza kuzoea hata mpaka KUPIGWA kama unabidii ya KUJIZOELESHA ingawa MHESHIMIWA MZOEFU umesahau ni siku gani uliyoanza kuzoea KIPIGO?
  • Unafikiri hujazoea kutukanwa kama siku hizi husikii matusi?


Tatizo ni.....
  • UNAFIKIRI unamuda wa KUJIZOELESHA wakati unaweza kuishi na ulivyovizoea TAYARI?

NI kweli.....
...... VIAZI vipo kama huhitaji kujizoelesha MAGIMBI.

Na pia ni kweli....
......MBWA ni chakula kama tu PANYA ukilazimika KULA.

NA.....
....... kama unafaidi zaidi MAISHA kwa kufanyia mazoezi kuzoea MAGIMBI ingawa VIAZI vipo, ......KULA MAGIMBI mwanawane!

NAACHA!
SIkuNJEma!
Tulia na LEADBELLY katika- IRENE GOODNIGHT

AU tu Ivete Sangalo alete za - Chica Chica Boom Chic

Monday, February 02, 2009

UTAMU WA KUONJA na govi!

Labda....
..... kama umekatwa ,UNAONJEA kilichokatwa.

Ukikatwa , BADO unafikiria na kuonja UTAMU kwa kisikilizacho REDIO au SIKIO kwa sikio au NANIHII iliyokatwa:-(

Na...
.... labda SI kweli ALIYEKEKETWA au kukatwa JANDO hakumbuki au kufaidi utamu ahisio au aoneao wivu GOVI.
Swali:

  • Utamu si ni HISIA?
  • Hivi neno GOVI si ni TUSI kwenye HISIA?

Labda....
....kichwa kuonja jua na kofia, BADO KICHWA kimeonja jua ,na kofia ni KIONJEA jua.

Na labda....
......Tafsiri na msisitizo wa kuonjea utamu GOVI hausikilizwi vizuri kwa sababu GOVI na UTOKO kwa USTADH , Mlokole au WEWE ni tusi.

TATIZO la kuonja bila kufikiria KIONJEO , govi linaweza kupata GONO.
Kama unasikiliza MAONO na unakumbuka KUKUMBUKA KISIKILIZIO labda:
  • Utasikia zaidi
  • Utaonja zaidi
  • Utaonjwa zaidi
  • Utalenga tusi kwa MLENGWA zaidi
  • Utasikilizia TUSI uliloTUKANWA zaidi

Na pia unaweza kugundua au kukumbuka UMUHIMU wa CHUCHU kwa TITI katika KUONJA.
Swali:
  • Si chuchu ni KIONJEO cha TITI?
  • UNAKUMBUKA kukifikiria kionjea UTAMU wakati unaonja UTAMU?


NAACHA!
Lakini onja kama huna GOVI ingawa mwenye govi anaendelea kufikiri anaonja na GOVI.
NAKUTAKIA leo mafanikio saana tu CHOONI !

Ngojea nirudie KUSEMA....

AU tu OSIBISA watukumbushe SUN SHINE DAY....

AU TU tupate Jungle Massive wakati - Bailey Drops 3 Ragga Trax 2007...

Sunday, February 01, 2009

Hivi MHESHIMIWA mdau uko HAI?

Labda....
..... ni kweli uko hai kwa sababu unaUHAKIKA uko HAI.
Swali:

  • Unafikiri waliokufa wanafikiria au WANAJUA wamekufa?

SAMAHANI ngojea niache na niende MSALANI kujaribu KUFANIKISHA!

BAADAYE basi!
Ngojea FISHbone watukumbushe FREDDY IS DEAD.......

Labda Ni KWELI mshindi KAJAMBA!

NI kweli......
......UKISHINDA katika kujamba, bado kuna WATAKAOJIPENDEKEZA kama WANAVYOJIPENDEKEZA kama vile MTU MAARUFU akijamba BADO umaarufu si HARUFU ya kijambo.

Swali :

  • Umestukia jinsi UWEZAVYO KUAMINI labda ukijipendekeza inarahisisha kupata KIDAKWA au KIDAKA TONGE na pia uwezavyo kusamehewa kanisani na HATA msikitini ukiinama na kujamba?
Samahani kama au LABDA ,....
...... wewe ni yule ambaye HUJAWAHI kufikiria KUJIPENDEKEZA ili KURAHISISHA nanihii IAMINIKAYO kuwa NI irahisishayo KUPATA TONGE kama tu kujamba.

NIsikutishe na sikusemi wewe ingawa ni kweli WAJIPENDEKEZAO labda WANA NAFUU kwa kuwa wanafikiria wanarahiSISHA!

Na...
....katika TAALUMA ya KUJIPENDEKEZA mtaalamu anaweza KUONJWA NANIHII katika kushughulikia NANIHII kutokana na breki za kijambo ALIZOCHUNA katika kujitahidi kuangalia SHINIKIZO liko wapi katika NANIHII!:-(

NA ni kweli.....
...hata kama WAJIPENDEKEZAO wanajua ulijamba na ulitarajia HAKISIKIKI kwa KUONYESHA jitihada zako za kutumia TAALUMA ya KUZUIA KIJAMBO, bado ni kweli BILA AIBU mtaalamu AJIPENDEKEZAYE anaweza kukiri katika UMATI HUKUJAMBA.

DUH!

Labda pia NI kweli ,....
... pasipohitajika kijambo WATAALAMU hawasikii KIJAMBO kama UMAARUFU hauletwi na HARUFU au MLIO wa kijambo.

NA.......,
.... wengi washeherehekeao USHINDI katika KUSHINDWA ,watajaribu kutuhakikishia kuwa pamoja na kwamba MSHINDI wakati anatoa HOTUBA ya USHINDI, ni BAHATI MBAYA akashindwa kuzuia KUJAMBA .
Basi ,......
....................kijambo cha MSHINDI labda kwa shabiki wa MSHINDI hakikuharibu umaarufu wa aliyecheka kwa kutosikia UJUMBE wa hotuba na mpaka JUZI YA KESHO KUTWA bado MDAU anakumbuka MHESHIMIWA aliJAMBA.:-(

Swali:
  • Hivi MSHINDI aliyeshinda anahitaji kukuhakikishia ushindi kama ulisikia AKIJAMBA?
  • Hivi AJULIKANAYE kwa ushindi wa KUJAMBA unauhakika ALIJAMBA?
  • Hivi unauhakika hapa kubwa zima Simon Kitururu linaongelea KUJAMBA?

HADITHI imeisha!:-(
NAWAZA tu MKUU usitishike!:-(
BAADAYE MKUU!
Twende Tanzania kwa WAKRISTO kumsikiliza Dr. Aril Edvardsen katika - Miracles in Tanzania...


AU twende Tanzania katika UISLAMU katika kujivunia SHEKHE MTOTO kwa jina Sheikh Sharifuddin Khalifa.....katika...-NENO


Au turudi tu BRAZIL kwenye LAMBADA kulambada na KAOMA katika- LAMBADA....