Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BADO huwezi kuwalaumu BINADAMU wenye nguvu za kiMTU katika kujaribu kumtetea MUNGU!

>> Friday, January 30, 2009

Bado...
.....UNAWEZA kufikiri BINADAMU huhitaji dini kama muongozo wa kwenda MBINGUNI mpaka ugunduapo jinsi binadamu watumiavyo ZAIDI DINI katika kumtetea MUNGU WAO hata kwa chuki na KUUA labda hata zaidi ya DINI iwafanyavyo wafanye ya Mungu ambayo ni ya UPENDO.
mfano:

  • Umewahi kusikia Ukristo, Uislamu , Usingasinga, Uhindu ,.....au hata Upagani usababishavyo BIN-ADAMU apiganie nani yuko sahihi zaidi ya NINI ni SAHIHI?

Lakini....
.....PAMOJA na uwezekano humuombi MUNGU msaada wakati unaenda kuiba , kuna uwezekano pia hatushukuru MUNGU kwa kutuachia kufanikisha KUIBA na kubakia natulichoiba.
Ndio...
.....BINADAMU ni wagumu kurudisha hata SADAKA walizoiba.

Na...
...kuna wenye kufuata DINI zikatazazo kumtamani jirani yako, wawezao kujaribu kujisahaulisha kwa dakika kadha kabla ya kukiri MATAMANIO au kutubu kuwa NANIHII inatamanisha ,na ikibidi hawasiti kutoa sadaka kwa kutumia walivyoiba.


Swali:
  • Ushawahi kujistukia wewe au mimi binadamu NISIYEWEZA YOTE nikimtetea MUNGU AWEZAYE YOTE?
Au niseme,....
......Binadamu ni MTETEZI kwa AKITETEACHO!

Ni binadamu wachache ambao hata wakifeli mtihani ukawaambia wajitetee kwanini wamefeli wanaweza kushindwa kujitetea hata zile sababu za kuwa sikuwa na kitabu na nilikuwa naumwa kichwa au chini ya KITOVU kidooogo siku ya MTIHANI kama ndio sababu KUU ya kufeli!

BINADAMU ni MTETEZI hata wa maswala yasiyowezatetewa, na akishindwa atakuambia kuwa NIMAPENZI YA MUNGU ndio maana haiwezekani KUTETEA!

Ndio maana hakuna tofauti kama:.....
  • Ukimkuta muhubiri DODOMA karibu na IKWETA anawezakukuambia kuwa ;ikawa usiku ikawa mchana, MUNGU aliumba kitu gani siku ya kwanza .

  • Na mhubiri wa dini hiyohiyo aishie katika maeneo ya kaskazini ya DUNIA ambako karibu miezi mitatu ni giza tupu kila mwaka , ATATETEA maana ya siku kwa kukuambia jinsi gani ; ikawa usiku ikawa mchana, MUNGU aliumba kitu gani siku ya kwanza, wakati siku yake ya mchana au usiku yatofautiana na DODOMA kwa miezi KADHAA ya giza tupu au mwanga mtupu, lakini atatetea BADO SIKU ni SIKU na katika kitabu kitakatifu ataelezea SIKU MOJA inaweza kumaanisha siku elfu moja.

Swali:
  • AU?
  • Unauhakika lakini usemavyo ''TUMSIFU Yesu Kristo ''kuwa Yesu anataka kusifiwa au unatetea sifa?
  • Usemapo MUNGU ni MKUU unauhakika kuwa MUNGU hajui kuwa ni MKUU au unajitetea kwa WATU wakusikiao unasifu na sio unayempa SIFA?

Inasemekana kuwa ni kweli......
.....tusipokumbushana YA MUNGU , ya Mungu husahaulika , ndio maana ni ujanja kwa wapendao kuendelea kuabudu hata MTI kukutana mara kwa mara CHINI YA MTI ili wasije sahau staili za kusujudia MTI.

BASI ngojea tujikumbushe:
  • UNAJUA unaweza ukawa unahangaikia kumtetea MUNGU asiye HITAJI UMTETEE?

Na....
......Kama unanguvu za KIMTU au KIBINADAMU, muombe MUNGU kama BINADAMU na naamini mbele ya MUNGU hakuna MTAKATIFU asitailiye sifa .


Ndio...
... najua kuna dini zishaurizo waumini wake KUMPIGANIA MUNGU na ya MUNGU na hilo sipingani nalo kwa sababu ni juu ya waaminio dini hio ya MUNGU. Ila hakikisha kuwa ni kweli ni MUNGU ASEMAYE umpige BINADAMU MWENZIO katika kupigania ya MUNGU na sio Muhubiri TU wa dini ya MUNGU au ya NANIHII uifuatayo asemaye hivyo nakuhatarisha walimwengu kwa asiyojua na afanyayo kwa kutaka sifa.:-(

CHA kujiuliza tu ni kwamba:
....Unauhakika ni kweli Mungu muweza yote anahitaji msaada wa BINADAMU katika kueneza neno LAKE TUKUFU?

TUBU au MUOMBE MUNGU WAKO usipotoke lakini!
Niombee na mimi kama sio MVIVU au kama nakukwaza kwa kutaka sifa!

PAMOJA na yote,.....
...... kuna BINADAMU anaye MLAUMU binadamu ajaribuye kumtetea MUNGU wakati ya MUNGU ni fumbo na adaie anajua jibu LA FUMBO labda afanya hivyo bila kujua fumbo kwa kutaka sifa?


BAADAYE!
NAWAZA tu hapa MKUU na MUNGU yuko MAWAZONI leo hii!
Tubadili HALI YA HEWA na kuwapata ZE COMEDY katika.....


Au tujivunie tu TANZANIA....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP