Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KILA KITU kiko safarini!

>> Wednesday, January 07, 2009

Labda...
...kutu katika CHUMA ni DALILI ya ushahidi kuwa chuma kiko safarini.

Katika safari , mtoto mwenye bahati mbaya ya kuishi sana, atakuja KUZEEKA mpaka atakuwa mtoto TENA na labda atasifiwa amekula chumvi nyingi.
Swali:


  • Kwani ni ujanja katika safari HII ya maisha kuishi muda mrefu mpaka unasahau hata kuwa unaishi au UKO hai?



Ni kweli!...
.. katika safari ya mzunguko wa maji , LABDA maji ya chooni yatafika mpaka baharini baada ya kupitia ule mfereji ulioshuhudia jamaa wakiukojolea kabla haujageuka mvuke , mawingu na kurudi kwenye ndoo ya maji ya kunywa uliokinga mvua ILIPONYESHA.

Ndio,....
....katika safari ya maji , LABDA maji yote yalikuwa machafu kwa kupitia kwenye mavimavi mabichi ya nguruwe.

Na katika safari ya maiti ya marehemu binadamu, LABDA udongo wenye rutuba ulionenepesha nyanya na kabichi za kachumbari ulioisifia jana, ndio siri yenyewe YA utamu.

Chakusikitisha au kumtuliza MJANJA ni;....
.....Jana yako na YANGU hairudi tena katika safari hii ya maisha!

Nakutakia SAFARI NJEMA katika MAISHA!

Pumzika kidogo na CHARLIE CHAPLIN atuonyeshe jinsi ya kucheza balee katika TABLE BALLET


Au Mighty Sparrow arudishe SOCA katika - Ten to One is Murder...

Au tu twende katika Retro Zouk ,ZOOK WAVE .......katika nanihino itambulikayo kama SEX BOMB....


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:37 pm  

Salaaaaaaaaleeeee! Mkuu natubu kifo mbona hiki hapa! shabashi wala siogopi najua naogopa lakini najikaza kisabuni hata kama ni mbunju lakini ajuaye siku hiyo hakika nitamtunuku BIA halafu nitampa udongo awe kustawi kama bustani ya eden ILA asichume matembele ya TUTA la katikati maana asije akageuka mzeee saaana.
Mkuu falsafa kali sana, nafanya mazoezi ya kuwa MAWAZONI

Simon Kitururu 2:28 pm  

@Markus: :-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 3:43 pm  

na labda mbolea ya kinyeshi cha binadamu inazalisha vyakula vitamu zaidi! ebu panda nyanya karbu na choo chenu harafu uone!

kumbe uchafu usioonekana ndo unatungisha mimba. mimi simo

Simon Kitururu 3:24 pm  

@kamala. :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP