Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UDHAIFU wa BLOGU uipendayo ni; UNAIPENDA!

>> Saturday, January 24, 2009

Usichokipenda LABDA ni shule zaidi ya UPENDACHO.

Tatizo ni...
.... binadamu si wavumilivu katika KUCHUJA NA KUDAKA MAZURI KATIKATI YA MABAYA.

Kizuri jujuu hukimbiliwa ndio maana UTUMBO husamehewa kwa mpenda nyama ya utumbo hata kama bado kwa ndani UTUMBO una chembechembe za mavi. (Samahani kwa kutamka tusi a.k.a mavi. Namaanisha kinyesi)


Tunadakwa na tufikiriayo ni mazuri hata kama kwa ndani ni mabaya.

Ukipenda unaweza kusamehe UDHAIFU.
Ukichukizwa na kitu , INAWEZEKANA kuna kitu utakikosa cha muhimu katika kikuchukizacho.

NA ni kweli....
....Labda kikuchukizacho kuna kitu kinagusa ndani yako na inawezekana kinagusa kaudhaifu kako maeneo.

Swali:

  • Kwani kuna kitu ukipendacho kisicho na udhaifu?
  • Unauhakika MUNGU hana udhaifu au umehakikishiwa TU na wahubiri kuwa Mungu anaweza yote na hana udhaifu?
  • Katika maisha usiowapenda sio MUHIMU?
  • Unauhakika uko kwenye BLOGU ikuhusuyo?


NAACHA!
Samahani kama nimekukwaza!:-(
NAWAZA TU HAPA MKUU!
NAKUTAKIA mafanikio chooni leo!

Tutulie na EDDY MURPHY aongelee ya Rais wa kwanza mweusi Marekani.....(Usisikilize kama unakwazika na lugha za sehemu za siri:-()


Au tutulie na IVOR Biggun katika wimbo Msichana wangu ana paka...(usisikilize kama utakwazika)...


Au nimuachie Zain Bhikha featuring Dawud Wharnsby waseme -ALLAH KNOWS...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP