Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA ungepata UJAUZITO kirahisi kama sio wewe UZAAYE!

>> Friday, January 09, 2009

Labda UTAUA kama ni mimi NITADAKWA!

Ukifuatilia ni kwanini Wajerumani karibu nchi nzima hawakuwa wanajisikia vibaya kwa vitendo vya Hitler, utagundua kuwa walijiengua kutoka katika lawama kwa sababu aliyekuwa anaamua na wakulaumiwa alikuwa ni Hitler na sio wao.

Ni rahisi kulifumbia macho jambo kwa kujiaminisha kuwa halikuhusu, na wengi hatufikirii JAMBO mara mbili kama sio majukumu yetu.



Kunatafiti kama hii ya Genovese Effect zionyeshazo kuwa mara nyingi kwa wengi; mtu akiwa peke yake ndio huweza hata kumsaidia mtu aliyepata ajali kuliko BINADAMU huyohuyo akiwa kwenye kikundi cha watu ambacho kila mmoja anamtegea mwenzake aanze kufanya NANIHII.

Swali:

  • Unafikiri hata katika swala la kujenga nchi hutegemei kuwa labda NI SHUGHULI ya MJUMBE WA NYUMBA KUMIKUMI ambaye ATAFANYA ,kwa hiyo usifyeke NA tupa tu matakataka mbele ya nyumba YAKO?
Na....
....Ukifuatilia utafiti wa Stanley Milgram, utastukia kuwa asilimia kubwa ya watu hufanya waamrishwayo na waaminiye ni mkuu au waaminiye atachukua majukumu na lawama kama kitu kitaharibika.




Kwahiyo labda ,......
...........Naweza au unaweza usifanye kama unahisi MWINGINE atafanya .

Swali:
  • Lakini unafikiri sungura ataachia shughuli za kumpa ujauzito mchumba wake KIPENZI kwa sababu kasikia au ANAHISI kuna sungura jingine linamshughulikia MREMBO mchumba katika maswala ya hasi na chanya ya wajanja kupeana UJAUZITO?
NAACHA!
Nawaza tu hapa MKUU usitishike!
WikiENdi njEMA!


Tutulie tena na FutureMan aniuae kwa kupiga chombo alichotengeneza mwenyewe akiitacho Drumitar.Kwa kifupi anapiga ngoma kama gita. Bela Fleck kwenye Banjo na mdogo wake Roy ''FutureMan''Wooten au Victor Wooten kwenye bass katika - Lochs Of Dread



Au niwaache John na Kristina wacheze katika ..... - Strictly Come Dancing 2008 Round 8 - BBC One

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 5:13 pm  

kaka Kitururu, mimi ninavyoogopa mimba, yaani usiseme.

Huwa namuuliza mama ilikuwaje akatuzaa watoto sita?

Sijui itakuwaje siku hiyo ikifika!!!!

Simon Kitururu 7:22 pm  

@Dada Koero:Nogjea tusubirie ufanikishe halafu ututonye shughuli ikoje:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP