Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA hutamani WAKATI UKO katika MAZINGIRA ya KIBINADAMU yenye vimtamanishavyo BINADAMU!

>> Friday, January 30, 2009

Labda....
.....Matendo yote afanyayo binadamu ni ya KIBINADAMU hata yale yahusuyo MUNGU yafanywayo na BINADAMU kibinadamu.

Swali:

  • Unafikiri MIJUSI haina dini na haiendi mbinguni?
  • Unafikiri Binadamu anaweza kufanya wafanyayo MALAIKA ?

Pamoja na UBINADAMU ni kuwa BINADAMU, binadamu ana BAADHI ya chaguo la aina ya UBINADAMU afanyao kabla ya kuwaachia walimwengu WENGINE waendeleze na mengine BINADAMU asiyoweza KUCHAGUA katika muda husika.

Labda pia....
....kama Upendo ni sifa ya kimalaika , kuna binadamu wapendao HILI , na kwa HILO wanafanya ya Kimalaika kabla hawajastukia kuna Simon wamchukiaye, tendo ambalo pia ni la KIMALAIKA, lakini la MALAIKA mwovu au kibaka.

Tatizo ni ...
.....matendo mengine yafanyikayo nyumbani kwako WEWE au MIMI sasa hivi wakati tuko sokoni muda huu, HAYO ya nyumbani ndio yametoka kwa muda huu, hayo HAYAFANYIKI mpaka baadaye kwa sababu inamaana katika muda huu tulioko sokoni tunafanya YA SOKONI.

Kuna mengi hayawezi kufanyika ndani ya muda mmoja kwa uwezo wa kibinadamu mwenye kichwa kimoja, na ujanja UKO KATIKA uchaguzi wa BINADAMU MUHUSIKA kuwa uwe JUU ya MTI au CHINI ya mti wakati unakula EMBE BOLIBO litokalo mtini , kama unafanya kihusianacho na MTI hai wa embe BOLIBO au hata NG'ONG'O.


LABDA...
.... tusikie AIBU kwa kutofanya ya kibinadamu wakati WEWE na MIMI ni BINADAMU.
Labda pia hata...
...kama huzini WAKATI UKO katika MAZINGIRA ya kuzini, SIKIA AIBU kwa kwenda kinyume na UBINADAMU ingawa ukifanya ni dhambi!:-(

Na NI kweli pia,....
....kujizuia kufanya vyakibinadamu bado ni UBINADAMU.

Na...
....Binadamu akijizuia kukupa ,inawezekana anafanya tendo la kibinadamu la UCHOYO, ingawa
akikupa YOTEYOTE kwa juhudi bila kuumiza akili, anaweza akaitwa malaya pia.

Swali :
  • Mazingira yako sasa hivi hayakutii majaribu katika tamanio la kibinadamu?

Usionje , SHAURI YAKO!

Naacha!
Mwenzio NAWAZA tu HAPA YA KIBINADAMU usistuke sana!
BAADAYE!

Tutulie na OSIBISA wakija na kibao- WOYAYA

Au Saul Williams ashushe USHAIRI katika - Black Stacey

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP