PONGEZI Barrack OBAMA ingawa tupo WATAALAMU wakunogewa wakati CHUNGU!
>> Tuesday, January 20, 2009
Tunaishi katika dunia ya mshindi kusifiwa ingawa aliyeshindwa hajakatwa makende !
Tunaishi katika dunia ambayo hata TUSIMULIWAYE kwa umaarufu wa KUPENDWA hawezi kutembea bila kulindwa asiuawe na binadamu wajisifiao kuwa sio wanyama na wenye busara kuliko Kuku mzazi achungaye vifaranga.
Binadamu wavaao nguo kusitiri nyeti kwa sababu wanatunza utu, huweza kumcheka nyani-MNYAMA ambaye bado hajastukia fasheni za vibwaya au busara za kumvalisha pete mchumba Ngedere wakati wakimuua mpaka NABII ISSA a.k.a YESU kwa kosa la kuhubiri UPENDO .
Binadamu kiumbe wa ajabu na anakatisha tamaa wakati mwingine!:-(
Labda tuendekeze udhaifu wa kibinadamu kwa;
- Kunogewa na tamu ili itusaidie kukabili chungu.
- Kuhitaji kiongozi ilitumfuate bila kuhoji.
- Kumsifia Rais kwa hotuba ASIYOANDIKA na iliyoandikwa na muandika hotuba tusiyemjua kwa jina ambaye hatumpendi.
- Tuchunguze hali halisi ya uwezo wa binadamu na kutomzidishia sifa binadamu zikazidi sifa za binadamu.
- Tuhoji mchango wetu katika jambo tuhitajilo KIONGOZI
Lakini labda....
.....tuwe na matumaini tu kuwa inawezekana ingawa ngumu!
Na kwa kuwa LEO NI SIKU YA OBAMA kuapishwa URAIS;
- NA TUWE na matumaini basi kama OBAMA aletavyo MATUMAINI!
Asante OBAMA kwa kuleta matumaini kuwa inawezekana!
HONGERA OBAMA!
Tutafika tu INGAWA hali halisi CHUNGU ingawa tunahangaikia KUNOGEWA kwa kujaribu kukwepa MACHUNGU kwa sababu kwa muda angalau mfupi INANOGA!
Swali:
- Huhisi RAIS Mugabe wa Zimbabwe pamoja na Marais fulani .....hawahisi RAIS Bush ni mjinga kwa kuachia ulaji Marekani?
NAACHA!
---------------------------------------------------------------------------------
Tutulie kidogo na kujikumbusha waliomdharau OBAMA kama katika hotuba ya Rudy Giuliani ionyeshavyo.
Tufikirie na THE LAST POETS waongelee WHEN REVOLUTION COMES....
AU tu tufurahie pamoja na COCO TEA akiimba Barrack OBAMA....
SIKU NJEMA!
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Je Afrika tutarajie nini kutoka kwake?
Kamala aliwahi kuniambia kuwa kama atafuata sera za masuala ya nje ya chama chakebasu tutarajie kina Jenerali Nkunda wengi tu wa kutosha hapa Africa.
Je hilo lina ukweli?
Je Afrika tutarajie nini kutoka kwake?
Kamala aliwahi kuniambia kuwa kama atafuata sera za masuala ya nje ya chama chakebasu tutarajie kina Jenerali Nkunda wengi tu wa kutosha hapa Africa.
Je hilo lina ukweli?
@Ambiere Kaluse: hakuna cha zaidi cha kutarajia zaidi ya alichofanya tayari kwa kuonyesha inawezekana ukifanyia kazi na ukiwa na bahati.
Post a Comment