Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

USIDANGANYIKE na binadamu ASIYENUKA MDOMO, baada ya KUGUNDUA kupiga mswaki.

>> Monday, January 05, 2009

Katika SAFARI ya CHAKULA MWILINI mwa BINADAMU,...... mwanzo na mwisho wa SAFARI YA CHAKULA MWILINI unanuka.

Sababu kubwa zilizomfanya binadamu MVIVU apige mswaki , ilikuwa sio kuondoa HARUFU . Inawezekana kabisa ilikuwa ni SABABU za KUTETEA ALA za kutafunia, kama sio maumivu ya mapengo akitafuna MAGIMBI zilizo hamasisha upigaji MSWAKI.

HARUFU HAIMTISHI sana binadamu , ndio maana LIBINADAMU likimpenda MTU, linaweza kufurahia kunusa hata kulamba viungo vya binadamu vyenye tabia za kunuka ,hata kama ni kwa kisingizio cha kwamba analamba au KUONJA njegere KAMA sio bamia, kwa sababu za KUTAFUTA au kumlisha MTOTO.

Na ni kweli...
.... uvumilivu wa binadamu kama UVUMILIVU WA MTU KUNUSA harufu mbaya, unasifiwa zaidi kidogo kuliko ukweli wa sifa ZAKÈ ukizingatia MTU kama WEWE au MIMI avumiliavyo visivyo na MAANA.


Ukweli ni...
... kama BINADAMU HAFI AKINUSA HARUFU MBAYA, na inabidi anuse, ATAZOEA kunusa na baada ya muda kuna binadamu WATAKAOPIGANIA HAKI ya kuwa, KUWE na siku kwenye KALENDA YA NCHI , siku ya hata kunusa VIKWAPA.

Na...
...... harufu mbaya inaweza kumaanisha UVIVU KATIKA HADITHI hii!

Na kama inamaanisha UVIVU,....
..Watanzania wengi kidogo ZAIDI YA KIDUCHU, wamezoea uvivu na hawafi ndio maana unasikia zaidi WAPIGAO VITA UFISADI zaidi ya UVIVU.

NA...
...Inawezekana kuwa MAFISADI walalamikiwao sana, wanafanikiwa WAFANIKIWAVYO ,kutokana na baadhi ya wavivu WENGI wasiofaidi,wawaingizavyo KINGI MAFISADI katika BAO kwa UVIVU.


Lakini LABDA...!.....,...
.....KILA siku ni siku ya UVIVU!
Swali:

  • Umestukia siku hizi TANZANIA kuna washabikiao zaidi kidogo zaidi KUDAKA MAFISADI kuliko washabikiao kuacha uvivu na ukweli kuwa UNAWEZA KUWINI au kuopoa LIMTU ZURI kwa kutoka jasho zaidi ?

Sikuzungumzii wewe LAKINI!

Wewe SI ni MFANYAKAZI bora na TATIZO ni ulipo hapalipi tu ?:-(

NA labda ni KWELI...
.....ukiwa kwenye OFISI FULANI au katika kuchimba mihogo kwenye shamba la jirani, MAZINGIRA yakiruhusu , UNABIDIIII WEWEEEE!

Swali:

  • Unauhakika WEWE sio MVIVU ambaye ni sababu ya TANZANIA au Matombo kutokuendelea?
  • Kama chakula kingekuwa na pua halafu wewe unahuruma, ungekionea huruma chakula kwa kukunusa maeneo HASA yenye upungufu wa oxijeni?

Naacha MKUU!
Nawaza tu hapa MKUU!
Nyonya kidole GUMBA au mumunya PIPI basi kama hunielewi:-(
SAMAHANI tena LAKINI kama HUNIELEWI!:-(


Ngojea basi ARRESTED DEVELOPMENT wanisaidie katika wimbo EVERYDAY PEOPLE...


Au tu SISTER NANCY aseme...BAM BAM...

Au ngojea tu SISTER NANCY aongee alichoongea KWA kirefu...


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 6:01 pm  

Kunusa twanusa heee kumbe hata ufisadi twaweza kunusa, mm kumbe hata kufikiri sana unaumwa lakini mbono mimi nakuelewa kuwa unafanya kazi ndiyo maana unanusa/ ha ha ha nawaza tu mkuu

Simon Kitururu 2:26 pm  

@Markus: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP