Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwani UNAFIKIRIA unavyokojoa WAKATI UNAKOJOA?

>> Wednesday, January 28, 2009

WENGI tu ni WATAALAMU wa kujilaumu badaye kidogo BAADA ya kufanya JAMBO wakati ni kawaida kwa jambo kutofikiriwa sana wakati JAMBO LINAFANYIKA.
Swali:

  • Si ni kawaida kwa MTAALAMU kufikiria KUNYA kabla ya KUNYA na si wakati ANAKUNYA?
  • Kichambio si ni muhimu baada ya kunya NA hakifikiriwi sana kabla ya faragha?
(Samahani kwa lugha chafu na naahidi kujaribu kuifua iwe safi siku nyingine)

NA...
... Nikawaida kujikuna KIPELE bila kufikiria tunajikuna kipele kama shughuli yenyewe ni KUFINYANGA TONGE la UGALI.

KAMA...
...shughuli ni kusubiri JAMAA litoke MSALANI , labda hatufikirii tunavyosubiria JAMAA LITOKE CHOONI wakati shughuli yenyewe TUILENGAYO ni HAJA NDOGO, au kwa lugha ya kigeni KUKOJOA:


Swali:
  • SI mwenye NJAA wakati anakula anaweza kuwa anafikiria ALALE WAPI?

NAACHA!

Tupumzike na WATAALAMU WA MATUSI mtandaoni watuimbie madhumuni ya mtandao.(USIANGALIE au kusikiliza kama UTAKWAZIKA)...

AU tuwasikilize washabiki wa YESU katika.....Yesu kele Nzambi...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP