Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA kuna umpendaye, UNAUPENDELEO weye!

>> Tuesday, January 20, 2009

Ni kweli kwako au kwangu .....
.....BINADAMU hawako sawasawa kama unahisi kuna UMPENDAYE!

Kama kuna umpendaye , basi kuna umchukiaye.
Swali:

  • Kwa asemaye hanachuki na mtu kajuaje anapenda watu wote na sio kuwachukia watu wote kama kwake binadamu wote ni sawa?
  • Kama unampenda mtu inawezekana unajua HIVYO kwa sababu unamchukia mtu, na chuki si ni dhambi?[shauri yako , unaweza kushindwa kwenda kunywa togwa mbinguni kwa sababu ya dhambi!:-(]

Labda...
....hakuna usawa katika binadamu ndio maana unastukia kuwa katika BINADAMU kuna UMPENDAYE!:-(

Unaweza kujisikia mpaka kumpa KIDUDE umpendaye UMPENDELEAYE asiye hitaji kidude chako na kumruka ahitajiye kidude chako ambaye angekiliwaza kidude ingawa ndiye AMBAYE hajabahatika kufarijika na wako UPENDELEO.

Chakushangaza...
.....katika binadamu apiganiaye USAWA, hakawii kujihifadhia AMPENDAYE kwa kuwa ANAMPENDELEA kwa UTOFAUTI WAKE asemao ndio kidaka pendo ambacho ananyimia nyie wengine KUGAWIWA kwa sababu ni wake MPENZI na ni chake kidude!:-(

Ni kweli....
....WAPENDAO, sifa yao kubwa ni UCHOYO wa kumgawia mtu mwingine WAMPENDAO au kidude wakipendacho.

Labda...
....kama unagawiwa kidude umo miongoni mwawapendelewao katika dunia hii isiyo na USAWA.

Swali:
  • Kwani hujui KUNA WADAIO katika binadamu hakuna upendeleo katika kugawiana kidude kwa sababu WOTE tumeumbwa kwa mfano wa MUNGU?
  • Ushawahi kunyimwa kidude cha kuchezea?
Tatizo ni.....
.....labda ukimuondoa Mungu wa upendo ACHOMAYE au kukupa MBINGU, ampendaye na amchukiaye BINADAMU mkubwa ni BINADAMU.
Na labda....
......aninyimaye KIDUDE ni BINADAMU niliye mnyima KIDUDE!

Na tukumbuke tu kuwa....
......umuhimu wa vidude kibao ni wa muda mfupi tu, na wote tutakufa baadaye kidogo na kuacha au kuoza na vidude ambavyo labda tusinge kuwa na UPENDELEO labda vingekuwa na manufaa zaidi au vingetumika zaidi kuongezea chachandu za WAISHIO .

NA....
.....Sina uhakika sana na busara ya BINADAMU KUTUNZA SANA VIDUDE ikiwa binadamu mwenyewe HATUNZIKI na atafanikisha KUZEEKA au KUFA baadaye kidogo pamoja nakujinyima kula ANGALAU nyama ya paka.

NAACHA!
Ninawaza tu hapa MKUU!

Siku njema!

Hebu twende NAMIBIA tukutane na Tate Buti katika- Super Focus (Drive Slow)


Au tu U2 wazungumzie The Sweetest Thing...

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 5:39 pm  

DUH!!!

Simon Kitururu 5:57 pm  

@Serina: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP