Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

POLE sana ABDULKARIM MBEMBELA kwa kufiwa na Mzazi!

>> Wednesday, January 14, 2009

POLE SANA ABDULKARIM MBENBELA!
Mungu amlaze mahalipema Mzee Mbembela!

Kwa habari zaidi....



Salaam,
Imefahamika kuwa Abdulkarim amefiwa na baba mzazi mwanzo wa mwezi huu na baada ya kuwasiliana naye ameelezea nia yake ya kutaka kusafiri kwa ajili ya kuhani,kwa kuwa mazishi yalikwishafanyika.
Jumamosi baadhi yetu tulijumuika kwa ajili ya shughuli nyingine ila tulitumia fursa hiyo pia kuliongelea swala la Mbembela. Na tulikubaliana kuwa tutachanga kwa kadiri ya uwezo ili mwenzetu apate uwezo wa kusafiri. Ahadi zilitolewa na kiasi kama cha euro 500 inategemewa kupatikana
Jumapili pia wenzetu walikusanyika mahali Helsinki na kujadili na wao pia waliafikiana kuhusu kumchangia chochote ili aweze kusafiri. Ahadi pia zilitolewa na euro 125 ilipatikana, na wao waliweka mkakati kuwa tujitahidi kwa kadiri ya uwezo ili ifikapo tarehe 17 Januari tuwe tumeshakamilisha. Ni imani yangu kuwa wengi tunaliafiki hilo kwa kuzingatia kuwa japo mwenzetu aweze kuhudhuria arobaini.
Nimekubali kuchukua jukumu la kukusanya michango yetu mpaka hiyo tarehe 17 Januari. Napenda kila atakayejaaliwa kutoa na aweke kwenye account ifuatayo:Nordea 127735-83595 EPHATA SOZIGWA. Tafadhali uwepo ujumbe usemao Mchango wa Msiba. Ikiwezekana, weka ujumbe wa maandishi kwenye simu yangu pia +358 40 375 508 02
Taarifa zaidi ya maendeleo nitaitoa baada ya tarehe 17.
Tukumbuke kuwataarifu na wenzetu ambao mimi sina anuani zao
Natanguliza shukrani,
Wasalaam

Ephata Sozigwa,

F I N L A N D.
Tel: +358 41 544 874 5
&+358 40 375 508 02

Kwa asiye na uhakika rafiki yetu Abdulkarim ni nani, basi ni huyu hapa...
Photobucket

Photobucket

Wakati wa furaha tulikuwanaye kama hivi...

TUSIMTENGE basi kama inawezekana wakati HUU wa huzuni na matatizo.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP