Heri YA siku MPYA!
>> Thursday, January 01, 2009
Baada ya kukoswaKOSWA na mvua za hapa na pale, labda UMKAVU bado.
Lakini MVUA ilinyesha.
HERI ya MWAKA mpya wa KALENDA ya bulicheka!
Swali:
- Si unakumbuka kuwa kama ukifika kesho maana yake labda utakuwa UMEKUWA mzee zaidi kwa siku moja?
Naacha!
Twende kidogo KENYA tukapumzike na WAKAMBA WAWILI- Muziki ya SOUL
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Dah!! Hii dhana kuwa kichwa chaweza kuzidiwa na masikio inatia shaka, lakini unaweza kuifikiria unapokuwa na shida. Si ushamuona mtu anatafuta gari mfukoni? Nilishaanza kufikiri kuwa umezama mawazoni mwako mwenyewe na ndio maana haupatikani. Haya na tuone mwaka una lipi mawazoni mwako ili maisha yetu yatupe changamoto za kuishi. Mwananchi mimi na wote kijiweni twakukaribisha tena kwa hii kalenda yetu "mpya". TuJielewe zaidi na zaidi
Blessings
Mmm mawazoni!!! aise nashngaa siku mpya ikiwa na gego na fizi zilezile, ikiwa imejaa maruhani yaleyale. Sahani na vijiko vipya labda na viganja navyo vitabadilika, mawazoni tu, pengine na mvua ibadili kalenda ya bulicheka.
hasa baada ya kuona ghorofa zimejengwa juu ya miti na mabadiliko mengine ya hali ya hewa yakiwa mapya aiseh hii hali MAWAZONI bwana
@Mzee wa Changamoto: Naumwa umwa kiasi fulani bado ni moja ya sababu za kibinadamu niko kimya.
Na inawezekan tunaweza KUJIELEWA kuwa masikio yamezidi KICHWA na bila CHANGAMOTO tunaweza tusisitambue na wala kujielewa:-(
@Markus: Lakini kalenda mpya inaweza kukuhamasisha kupata au kumpa mimba mchumba!:-(
Inawezekana mchumba kabobea katika kalenda na leo hayuko mwezini.
Post a Comment