Labda bado tokea leo NAJIFUNZA kukupenda!:-(
>> Saturday, January 17, 2009
MAPENZI si hupata jina MTU akisikia kuna KITU kinaitwa PENZI?
Itabidi LABDA tu.....
......MPENZI atafute DAWA ya PENZI kwa kuwa penzi LANGU au LAKO kwa MPENZI , LA JANA, si la LEO .
Lakini....
.... mapenzi kama KIPORO CHA MAHARAGE YA NAZI , cha jana KINAWEZA KUNOGA zaidi leo.
LABDA...
...unapenda hata kama HUFIKIRII kupenda, INGAWA kama hufikiriii UWAPENDAVYO, kuna uwezekano UNAJIPENDA zaidi kuliko UWAPENDAVYO au upendavyo BAGIA.
Unaweza kufikiri unajua kupenda kwa sababu una MPENZI asiye KUPENDA akukumbushaye PENZI!
Lakini...
... .. labda kama una asilimia kubwa ya penzi kwa MPENZI, kumbuka kulifananisha PENZi na UTAAAHIRA kiduchu HASA kama unafikiri HUTUMII akili kwa kuwa UNAJUA PENZI katika kufanikisha hata MKUMBATIO wampenzi anukiaye vizuri manukato au KIKWAPA kwa kuwa UMEPENDA!
SAMAHANI!
BADO najifunza KUPENDA na nazeeka!
NA labda....
..... hushauriwi KUNISIKILIZA kuhusu hata MPENZI senene WAKATI UNAJUA hat mapenzi ya mwenyezi MOLA inabidi UJIPENDEKEZE au uote SIGIDA.!:-(
Swali:
- Si wewe NI ndugu?
- Unafikiri kama unapenzi NA UMEPENDA unahitaji USHAURI wa kukumbushwa KUPENDA?
NAACHA nisije nikakuzingua bure wewe UJUAYE penzi na una PENZI.!
Twende kidogo South Africa tukatulie kiduchu na Hugh MASEKELA aongelee...
Grazin' in the Grass
Au tu Conscious Youths waseme - Play ....
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kupenda nako taabu, unaweza kumpenda halafu anakuambia Penzi limeshuka bila kujali pengine lina Blanketi.
Unapenda kwa mengi lakini ukijiuliza ukipendacho kama kweli unakipenda JIBU unapenda sababu unajua kuna kupenda LABDA nawe uonekane unapendwa.
Sijui kwanini ukijifunza kupenda halafu ukaomba kupenda, kisha unamuuliza vipi unanipenda huku mkiwa wote mnagida PENZI.
LABDA ukipenda na kujifunza kupenda ni vitu tofauti. Huenda ukionyeshwa unapendwa basi unaringia hicho kinachomfanya akupende au akulaghai kwamba anakupenda sababu ya kitu fulani ambacho wakipendacho huku wewe unajua hicho ndicho kimfanyacho akupende.
PENGINE kupenda na PENZI ni tofauti pia, maana penzi ni kama simulizi za sodoma na gomora halafu kupenda ni fasheni ya kuonyesha upo pamoja nasi katika ulimwengu wa kujua kupenda.
Inaweza ikawa POA unapenda ukitoacho kuwa ndiyo tiketi ya kupendwa, lakini siyo ya PENZI.
KUMBUKA tumeambiwa tusinyimane cha ajabu wapo wanaokunyima halafu wanakubeza na kujipongeza wamekunyima kile ukipendacho maana wanachojua kwamba ukinyimwa wanajua wamekunyima ulikifikiria kupewa.
Wakati mwingine ukipewa tu unageuza kurasa na kuona kumbe upewacho hakina ubora kama cha fulani sababu yule fulani anaunga kwa nazi, nyanya, huku akiongezea matunda ya kila aina.
Hata hivyo nashangaa kinachotufanya tugeuze wakati tulikihangaikia kukipata. Si mnajua fashieni za PENZI? ndiyo maana PENZI ni kama unakula kupenda halafu ukitumaini PENZI liwe na utamu kuzidi kupenda halafu unajishtukia kwamba utamu wenyewe wa kukopa kwa wanja,manukato, maringo, na vikorombwezo vya kukuteka kwa PENZI.
Utaona PENZI ni kama adui wa kupenda halafu ukipewa PENZI ukawa na HAMU ya kutetemekea PENZI, kisha unagundua kwamba hata wafungwa wanatamani penzi ndiyo maana wanapita kwa mlango wa NYUMA kwenda uani.
Ndiyo maana wengine wamegundua PENZI ni mchanganyiko wa kupenda kutoa wakipendacho hata kama unapita mlango wa uani kuingia CHUMBANI. Haijalishi hicho chumba kina kufuli au hakina kwani ujuacho ni kuingia kwa raha zako lakini akingia PANYA unashtukia hukufunga mlango sababu ya ule mlango wa mbele haukuweza kukoleza PENZI. Pengine naweza kukonda uninyimapo lakini nanenepa unipatiapo PENZI ambalo nimekinai nashindwa kusema sababu kuna kitu kiitwacho kupenda. Lakini swali hivi kupenda kunatokana na nini? PENZI lako la fasheni na maringo ya ulichonacho sababu ni chako na chake lina maana gani? Akinipa yule unanuna wakati ulininyima chako hata kama uliwahi kuniomba MSHIKAJI wa KITIMOTO kwa muuza nyama asilia? kumbe ukipenda unaweza kunyimwa PENZI lakini kama utatoa PENZI huwezi kukosa kupendwa, heeeeeh kumbe kupenda na PENZI ni tofauti? ukigawacho kwetu na kwao kinatofauti au mimi na yule tunatofautiana katika miondoko ya BOLINGO na HIP HOP, labda sote tunakunja sura tuwapo stejini kwahiyo unatofautisha ukunjaji wetu wa sura. Labda jamaa anatoa sauti za miguno ya kugugumia maumivu ya KILIO cha kunyimwa alipogundua alinyimwa sababu ya kukunja sura kupita kiasi.
OOOOOOOOH napumzika na muziki niupendao unipao PENZI la dhati ingawa unanichosha wa KWAITO, sikiliza basi wimbo wa 'MYEKE BABA' wake MANDOZA kule kwa Mandela
@Markus.DUH!
happy bday mkuu..nakutakia maisha marefu na afya njema..1
@Sheria:Asante sana MKUU!
Post a Comment