Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kusuluhisha Ugomvi wa Baba na Mama , kuna wadaio wako katikati!

>> Wednesday, January 14, 2009

Katika ugomvi wa Baba na Mama kama hakuna uegemeako zaidi , LABDA ni kwa vitendo tu ufanyavyo na sio KUMOYO!

Na inawezekana unaweza kudai unajua vizuri ni kwanini SHANGAZI anampiga MJOMBA ingawa hata siri yao ya walivyofikia kufanikisha kumtengeneza BINAMU hujui!:-(


Na....
....Katika kumuelewa asiyeingilia kuamulia ugomvi wa kuku na bata, labda kwa kawaida huyo MHESHIMIWA anajua AU kuhisi tayari mwisho wa vita, kuku ANAWEZA kufa.
(Samahani ambao hamjawahi kufuga kuku mwenye mchumba jogoo na bata watembeao bila viatu)

Lakini...
....Inasemekana wenye busara hawaingilii ugomvi wa ndugu kwa hofu NDUGU WAKIPATANA SEBULENI wakati uko chooni, unaweza kujisikia kutomalizia shughuli za MALIWATO ili usirudi SEBULENI.

NA labda ni KWELI, ...
.... usipoingilia UGOMVI ,ndugu anaweza kumuua ndugu !:-(

Cha ajabu ni....
...... mpaka wenye dini wampendao Mungu watadai katika dini zao za kistaarabu, Mungu hapingi vita na kuna watu wake hata kwenye vita atawapendelea na labda kuna wakati aliwashauri waende vitani:-(

Na....
...Katika hawa ndugu , Waisraeli na Wapalestina , ugomvi wao umefanikiwa kugawa watu kama ule wa BABA anamuonea MAMA .

NA pia ....
.....katika ugomvi wa WAISRAELI wanawatungua WAPAlestina, asilimia kubwa ya watu wako tu kama vifaranga JOGOO likimgombania KUKU, hakuna wafanyalo .:-(

Lakini ....
...Inasemekana Binadamu ni zaidi ya mnyama ingawa hata tunajua kuna binadamu Mtanzania aonaye kuwa binadamu ZERUZERU na KUKU au MKOJO WA KUKU MWEUSI TASA aagizwaye na MGANGA WA KIENYEJI , wote wako sawa, ukifuata masharti utatajirika na kuwa na MKOKOTENI.:-(

Swali:

  • Si inasemekana binadamu wote ni ndugu kama vile tu Waluo wote ni ndugu za Obama?
  • Bado unaamini binadamu ni mstaarabu na anahuruma ukiangalia Waisraeli na Wapalestina wanavyouana na kila mwenye busara aliye na nguvu kuna timu iuayo ambayo katika ugomvi anashabikia?
Tukirudi nyumbani...
.....Ugomvi wa Baba na Mama hata kama si mshabiki, unaharibu familia!
Na labda.....
..... binadamu ndio maana ni bingwa wakusifia MTU kuwa ni zaidi ya wanyama wengine kwa sababu Binadamu ni Mnyama!:-(

Swali:
  • Unafikiri Kuku au Bata kashawahi kumsifia Binadamu kuwa ni Babu Kubwa zaidi ya Njiwa?

NAWAZA tu MKUU na nimeacha!


Au tupumzike kwa kumuangalia binadamu akishughulika.....

Au tu Binadamu aendeleze....(Usiangalie kama utakwazika)


Au tu Lee ''Scratch''Perry azungumzie tu kurudi kwa KIBOKO YA NYANI katika - Return Of The Super Ape


Na asanteni wote ambao hamkunitenga siku hizi za karibuni ikiwa pamoja na hawa...


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket





Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket




Photobucket

Photobucket

Au ngojea tu Mbilia Bell amalizie kwa kusema - ♪Les Z'on Dit (Welcome)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP