Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA shetani ASIFIWE!

>> Sunday, January 25, 2009

Pamoja na yote....
Labda shetani asifiwe kama:...

  • Waaminio MUNGU wanafanya ya SHETANI.
  • Kwa waaminio MUNGU , vitamu vingi kama sio VYOTE ni vishawisi na nyuma ya YOTE unogewayo ya kidunia kama NANIHII au labda MBATATA, ni propaganda za SHETANI.
  • MUNGU wako waupendo anasababisha UMCHUKIE aaminiye MUNGU KWA STAILI TOFAUTI NA YAKO ya kumtukuza MUNGU.
Swali:
  • Unadhani wasiojua MUNGU wanamatatizo na SHETANI umjuaye?
  • Kwanza unamjua SHETANI?
  • SI waaminio MUNGU ndio wajuao kuna kitu kinaitwa MUNGU au SHETANI?

Unaweza kubisha !

Lakini...
.... labda SHETANI ASIFIWE kama:

  • Wanasiasa uwaaminio wanaapishwa kwa vitabu vya MUNGU na wanafanya ya SHETANI kwa kuiba na kutojali WANA watesekao wa MUNGU.

  • WEWE uaminiye MUNGU unakwazika na mimi BINADAMU hata LABDA kwa HATA kuongea niongeacho,na badala ya kufikiria MUNGU unachukia, unakasirika , unataka kugombana au unakumbuka maswala ya kishetani zaidi ya YAMUNGU kwa sababu unanichukia.

Swali:
  • Hivi unanichukia?
  • Wakati unamuamini na kumuabudu MUNGU, unafikiri SHETANI pamoja na mafanikio yake yote yakukudaka na KUNIDAKA mara kiduchu nakadhalika, hasitahili SIFA?
  • Unafikiri mpaka JUMAPILI hii ni SHETANI au MUNGU aliyefanikiwa kukudaka MARA NYINGI?

TUBU kama unahisi mrembo SHETANI bado anakuvutia zaidi kidogo ingawa unaongea ya MUNGU.

Kaza BUTI katika ya MUNGU kama UNAAMINI MUNGU na unataka usidakwe na mtoto wa mjini a.k.a SHETANI.

Niombee kama nakutia majaribuni au unahisi nimepotea zaidi kuliko wewe na nahitaji KUOMBEWA!

NAACHA!
Bwana , Bibi na MTOTO wasifiwe!
jumAPIli njeMA!

Niko katika JAZZ na Bongo Flava ya SOMALIA Mukichwa!
Tulia basi na DUKE ELLINGTON katika shoo yake ya mwaka 1942 katika C Jam BLUES...

AU twende tu SOMALIA kwa K'naan katika kibao -SOMALIA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP