Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa jina la WAZIRI MKUU , waganga wa KIENYEJI TOKA!

>> Tuesday, January 27, 2009

Tokea enzi za kale mpaka leo kulikuwa na USHIRIKINA na UCHAWI na huwezi kuuUA ushirikina au uchawi kwa kutunga sheria.

Palipo na USHIRIKINA na UCHAWI , waganga wa KIENYEJI wana nafasi yake hata kama HUTAKI
.
Na ukweli ni.....

.....katika TANZANIA ,ushirikina na uchawi kama vile tu UDINI , uko kwenye chati.

Swali:

  • SI mpaka leo uchawi unavutia ndio maana kitabu cha HARRY POTTER mtoto mwenye nguvu za kichawi, ndio maarufu kuliko Biblia na Korani katika nchi zilizoendelea?
Kwa nia njema...
...kuna wasemao pia ;'' KWA JINA LA YESU shetani TOKA''!
  • Ingawa inasemekana shetani hao huwa hawatoki kama utolewaye shetani huamini ya mtoa shetani.

Na ..
...kuna watumiao KORANI kusomea mtu ALBADILI katika kufanikisha.

  • Ingawa bado Wayahudi wanaendelea kuwapo na kuendeleza !

Mauaji ya Maalbino na wakongwe kwa sababu za kishirikina yanasikitisha sana!

MAUAJI ya MAALIBINO na WAKONGWE JICHO NYAYA ,inabidi yapigwe vita sana !
  • Na tusipoangalia NA kwa kuingilia SHUGHULI kichwakichwa ,haya MAUAJI YATAENDELEA KUWEPO kinamna .

Ila....
... naamini Maalbino hawajaanza leo kuuawa.:-(
Kama unakumbuka vizuri na ni kijana wa zamani, utakumbuka ilikuwa kawaida kabisa kwa watu wengi kuamini Maalbino hawafi ila wanapotea tu . Pia mpaka kulikuwa na waaminio hawapigiki picha.

Nakumbuka pia mpaka kuna watu walikuwa wanabishana kuhusu kama kuna mtu kaona kaburi la albino sio miaka mingi iliyopita. Hili ni jambo nalolisema nikiwa mimi mwenyewe MSHUHUDA wakusikia kwa masikio yangu watu ambao wanaelimu zao wakibishana kuhusu hili jambo.

Hii inaonyesha jinsi gani Watanzania wengi hatuwaelewi ndugu zetu Maalbino na sio tu Waganga wa kienyeji ambao tunawalaumu ndio WANASTAHILI KULAUMIWA.

Na...
.....Mganga wa kienyeji hawezi kufanikisha kitu kama sisi wateja tunaelewa nini kinaendelea na tunawaelewa ndugu zetu Maalbino na Wakongwe JICHO NYANYA .


Haiwezekani kufuta waganga wa kienyeji wakati jamii ukijumuisha na viongozi wenyewe ambao wanatakiwa kusimamia ufutaji wa waganga wa kienyeji, wana aamini katika waganga wa kienyeji.

Ukiwanyang'anya vibali waganga wa kienyeji, unachofanya ni kuwafanya waendeshe shughuli zao chini kwa chini kwa sababu wateja wapo.

Na kama unakumbuka.....
.....Uchawi na taaluma ya uganga wa kienyeji ni moja ya vitu tokea enzi hizo vimeshamiri na hushamiri zaidi chini kwa chini .Ndio maana mpaka leo bado tupo tusiojua kuruka na ungo.


Naelewa kuwa WAZIRI MKUU anasema waganga wa tiba ya jadi ambao wataweza kuhakikishia wanataaluma kuwa wagonjwa wao wanatibika watarudishiwa leseni.Lakini tukumbuke tu kuwa kuna watu wengi wanaugua kisaikolojia tu hata katika hospitali zetu za KWAIDA , na afanyacho mganga WA KIENYEJI kama MGANGA HOSPITALI FULANI ni kuwapa nguvu tu WAGONJWA. Nguvu ya kujiamini na NI kwelikweli KUNA WAGONJWA WENG TU warudipo nyumbani,SHUGHULI itajipa na Zubeda mwenyewe MIMBA ataipata kutokana na nguvu mpya na hari mpya aliyokuja nayo Simon Kitururu iliofanikisha mbwembwe za Simon Kitururu mdogo abanwe na chupi kabla yakuonyesha maringo yake.

Nachojaribu kusema ni;.....
.....''Kwa waaminio Mganga wa kienyeji , Mganga wa kienyeji anaponya kama TU katika waaminio maombezi Kanisani kuna watakaoshuhudia wamepona ''.


Tatuzi la swala hili zima ni elimu.

Tatizo la elimu yetu Tanzania, maswala kama haya hayafanyiwi utafiti wa kitaaluma na Vyuo Vyetu Vikuuu au hata Vyuo Vyetu Vikuukuu ili kuwa na njia iliyotafitiwa kitaalamu ya kutatua swala.Matatizo yetu katika jamii yanarukwa na elimu yetu na hata sheria zetu zenye misingi kutoka kwa elimu na sheria za kikoloni na labda zenye uhusiano na matatizo ya nchi za nje kuliko matatizo ya nchi yetu.

Kama dawa itakuwa kama aliyoshauri Waziri Mkuu PINDA kuwa auaye auawe bila kufikishwa Mahakamani, kuna watu ambao watauawa kwa kusingiziwa kisivyo halali .

Na...
....Vitendo vya kuua au hata kubagua Maalbino na Vikongwe ni vitendo vya kinyama .
Na...
....Vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kuua binadamu yoyote kwa kuhisi yeye kaua na labda kasingiziwa ni vya KINYAMA pia.

Ni jukumu la kila mtu kuelimisha jamii na sio kukuza CHUKI.
Vitisho sio dawa kama atishwaye kwa sheria anaogopa zaidi uchawi.


Swali:
  • Unafikiri ni wanasiasa wangapi maarufu ambao ni wateja wa waganga wa KIENYEJI?
  • Hivi wewe haufai kuuawa?


NAacha!
Na NAWAZA tu hapa MKUU!

Au ngojea tujifunze historia ya Marekani kwa mtazamo fulani.....katika AMERICAN HISTORY


Au tu Dru Hill waseme.....HOW DEEP IS UR LOVE

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP