Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA dunia IKO kama ILIVYO kwa sababu WAJUAO wako KIMYA!

>> Tuesday, January 06, 2009

Kila siku kuna aliyeshuhudia ambacho WENGINE WOTE hatujaona hata kama ni kifo cha MENDE ,na aliyeona ndiye AJUAYE mende alivyotapatapa wakati ROHO INAMTOKA.

Labda...
....wote tupo ingawa KUNA ashuhudiaye MAREHEMU NZI afavyo ingawa wengine hatuoni, na AONAYE ndiye mwenye UJUZI na ushahidi kwanini NZI KAFA kalalia mgongo ingawa anakibiongo.


Na labda...
....hata kama wote tupo sebuleni, kuna ambao MAWAZO YAKO CHUMBANI na hawastukii mwanadada amekaa vibaya kwa SEKUNDE SITA, na mfuko wa sehemu za siri WAMAUAMAUA ulijitokeza kupunga hewa na ndio maana KIJEBA anakodolea macho kusubiria raundi ya pili ya MCHUNGULIO wa faragha.


Labda...
... wajuao ni WACHOYO!

Labda...
... wajuao hawajui vizuri ndio maana wanatishika kutujulisha tusije kujua zaidi.

Labda....
...Ujuacho tayari unajua na ukiambiwa zaidi utajua zaidi kitu kisababishacho kitisho kwa akujulishaye kuwa utajua kuliko ajuavyo.

Swali:

  • Hivi ujuacho leo hakuna uwezekano hautakijua kesho?

Lakini...
... ukimya wa wajuao unaweza ukawa unatujulisha KITU.

Na labda....
...mtu mwenye udhaifu wa KIBINADAMU akikuambia kwa sababu anajua , ndio MTU wakujihadhari naye, hasa ukikumbuka hata MALAIKA SHETANI asiye na udhaifu wa kibinadamu hakujua Mungu atamfukuza mbinguni AKINANIHII, ndio maana yuko huku anatusaidia kufurahia kuua, wizi na siku moja moja kuzini hata migombani na LIMTU la mtu.

Swali:
  • Unajua labda ni wewe peke yako ujuaye ULIHARISHA leo?
  • Kama wanajua, wangekufa?



Naacha!
Unajua NAWAZA tu hapa MKUU!

Tulia na Wazekwa katika -Moi Je Sais


Au tuendelee tu tena na LOS LONELY BOYS katika Heaven..

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP