Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Baadhi ya pesa hupitia mpaka kwenye TITI!

>> Monday, January 19, 2009

Sidilia ni pochi mwanadada akiamua!

Kuna waogopao ukoma lakini wakajivunia pesa wasiyo jua ni pesa KIRUKA NJIA!

Na....
.... ukiichunguza sana noti unaweza kustukia labda imewahi kuchambiwa KIDOOOOOGO!:-(

Na ni kweli...
... Ukimfuatilia nyuki katika matembezi yake, unaweza kustukia kinyesi kwenye kachumbari ya ASALI.
Swali:

  • Kwani hutumii noti na mashilingi kwa sababu kibonge una kadi ya benki?

Kwa chekibobu na sista du msafi....
...kumbuka labda pesa ujivuniayo wa mwisho kuishika ni ombaomba mwenye ukoma.
Na...
.... kutokana na kuingia na kutoka kwa pesa kwenye WALETI a.k.a pochi,KUNUKA kwa choo cha stendi na POCHI a.k.a waleti vinatofautiana kwa ujazo tu wa HARUFU!:-(NAACHA!
Nawaza tu hapa MKUU!

Kwa sababu leo ni siku ya watu fulani kumkumbuka Martin Luther King Jr... tupate tena kidogo...I have a dream...


Au tu Nyerere aongee tusichoelewa kwa hisani ya Suby production.......

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 7:37 pm  

Duh! Mkuu, labda ndiyo maana rangi nyeupe na nyekundu zinapendwa sababu ni mfano ingawaje hazitimizi agano. Basi kwavile tunajua tujuacho ndicho kijulikacho, inakuwa bongo la ujiko kujua kwamba kuweka pesa kwenye MATITI ni bomba hata kama watoto wakubwa hawanyonyi hadharani! Ndiyo maana wanajua kwamba Waleti hubeba vikorombwezo toka geti la nyuma hadi pale mlango wa dada fulani mweny mwanya uwavutiao wapendao kutafuna meno ya wenzao. Kumbe lile domo ni kubwa chapati inapwaya halafu anajongea kwa mikogo utadhani mkuu wa kitengo cha maficho ya pesa yaani MATITI. Aise vipo vifichwavyo hata vikionekana huwa kero, labda pesa nazo hunyonya kile kinyonywacho na watoto wakubwa wajuao utamu wa kunyonya maziwa ya mama mwenye kuficha pesa pale. Labda ni uhaba wa pochi tu ndiyo maana hata kule uani ni halali kuweka pesa zinukiazo manukato ya zenji. sijui pengine!

nimeshindwa kaka

Koero Mkundi 6:45 am  

Haya kaka, Mkodo, mzee wa mawazoni,
Ahsante kwa ubunifu,

Simon Kitururu 11:57 am  

@Markus: DUH!:-)
@Dada Koero: :-)

Unknown 5:56 pm  

na mimi nasema DUH!!!!

Simon Kitururu 8:26 pm  

@Kaluse: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP