Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UMEJIULIZA ukweli wa WASEMAYO wamjuaye MAREHEMU baada ya MAREHEMU kuwa MAREHEMU?

>> Wednesday, January 28, 2009

WOTE tunajua ni UUNGWANA au KAWAIDA kwa wahudhuria MSIBA kusema MAREHEMU alikuwa MTU mzuri.

Lakini....
... kuna WAJUZI wadaio kumjua MAREHEMU kwa kuwa walikuwa naye SEBULENI ,wasimuliao MPAKA jinsi WALIVYOMJUA MAREHEMU chooni ambako hawakuwa naye.

Na...
... pia kwa sababu MAREHEMU alikuwa na DODOKI bafuni, kuna WADAIO KUJUA au wachukuliao kuwa ni kweli MAREHEMU hakuwa na UKURUTU kwenye NYETI katika simulizi zao hata ambazo MAREHEMU angechukulia kuwa ni simulizi za ishu NYETI.

Labda ni kweli .....
....TUJUACHO ambacho NI KWELI, ni kwamba MAREHEMU alikuwa MTU ingawa LABDA HATA hatukusikia akiJAMBA!:-(

Swali:

  • Kama unaogopa MAITI unauhakika MAREHEMU alikuwa MTU mzuri?
  • Unakumbuka labda leo kabla hatujanya NINA WEZA au UNAWEZA kufa?
  • Wakati uko hai hujawahi kufa MOYO?

Kwa bahati mbaya....

......MAREHEMU akifanikiwa kuwapa uhakika washabikiao MAREHEMU msibani kuwa MAREHEMU amekuwa MAREHEMU , marehemu HANA KAULI yakujitetea ingawa bado MAREHEMU ana UJUMBE.

Kama unamjua MAREHEMU, marehemu bado anasema na anakupa au ananipa UJUMBE ingawa ni MAREHEMU.

INAWEZEKANA...
...labda Marehemu anaweza kukukumbusha MPAKA kuhusu alivyotoa au ulivyotaka akutoe BIKIRA hasa kama ndiye yeye aliyekuwa chaguo LAKO au hata kama pia ndio yeye ambaye HAKUWA chaguo LAKO la KUPULIZIA KIDONDA.

Swali:
  • SI unakumbuka si wanawake tu wenye BIKIRA?
  • Kama wewe ni MTANZANIA , hivi MAREHEMU NYENYERE , samahani NYERERE, hakukumbushi Tanzania haina DINI ingawa ni Marehemu?


NA ...

....kama WEWE au MIMI ni mpenda KUSIKILIZWA , tunaweza KULAZIMISHA tusikilizwe hata MSIBANI ingawa tuongeayo hayahusiani na Marehemu.

NA...
....STAILI yako au YANGU yakuzungumza kwa MAJONZI inaweza KUSABABISHA upendwe au kupewa SENENE waliotunzwa kwa ajili ya WAHESHIMIWA msibani.:-(

Na ni kweli...
...Pamoja na wote wenye simulizi TAMU au CHUNGU kuhusu Marehemu MSIBANI au NYUMA ya CHOO , .......HAKUNA AMJUAYE MAREHEMU kama marehemu alivyomjua MAREHEMU.

Swali:
  • Au unafikiri unamjua MAREHEMU?
  • Unauhakika UNAJIJUA?

NAACHA!
KUMBUKA NAWAZA tu HAPA!:-(
ISHI ingawa kama unaishi si lazima ni kwa sababu ni kweli WEWE au MIMI ni BINGWA wa kuwa HAI:
JAMBA basi uhakikishe kama UKO HAI!

SIku njeMA !

Ngojea HOMER SIMPSON ajaribu kubadilisha HALI YA HEWA katika BEER SONG.....


AU ngojea RED HOT CHILI PEPPERS waendelee kubadilisha hali ya HEWA.. katika DANI CALIFORNIA


AU CULTURE wamalizie kusema nijitahidivyo kueleweka ingawa sieleweki katika shoo yao ya South AFRICA katika - I TRIED....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP