Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MATUNDA ya KUMCHEKEA kibosile AAMUAYE!

>> Saturday, January 10, 2009

LABDA ni kibosile AAMUAYE!
Swali:

  • Si unaamini kuna BINADAMU hata mwenye doa kwenye chupi isababishwayo na nukta ya mwili, NDIYE aamuaye?

NI kweli...

Labda ni KIBOSILE ndiye aamuaye ...
......ingawa ukimchekea aamuaye , UAMUZI wake unaweza kutokukuchekea kutokana na UAMUZI wa AAMUAYE!

AKUCHEKEAYE aamuaye,.....
......uamuzi wake LABDA si wakuchekelea INGAWA una sifa zote za umchekeaye AAMUAYE.

Mke wako sekretari wa AAMUAYE, si kweli ni lazima anajilazimisha kumchekea aamuaye kama anachakuchekesha AAMUAYE.

Ukijihami na kibosile aamuaye wa mke wako , NI MKE wako ndiye AAMUAYE.

Ukijihami na kibosile aamuaye wa bwana yako, NI WEWE ndiye UAMUAYE.

Swali:
  • Si unajua siku hizi mwanamke anaweza kumuoa mwanamke na mwanaume anaweza kumuoa mwanaume kama zamani tu?
Ukijihami na aamuaye amchekeshaye wako aamuliwaye,unauhakika WEWE HUNA chakuchekesha kama AAMUAYE?


Lakini...
... Kibosile wamchekeleaye, ....
.....KESHO aweza kuwa bingwa wa kumchekea AAMUAYE!

Lakini....
...Nani kasema KIBOSILE binadamu ajulikanaye kama AAMUAYE, akikunyima mshahara , ni yeye MAISHA YAKO aamuaye?

NAACHA!
Na kumbuka NAWAZA tu hapa mawazoni MKUU!

Swali:
  • Hivi RAIS MSTAAFU wa jana hamchekei RAIS wa sasa AAMUAYE?
  • Unauhakika kwa kumchekea aamuaye hujarudisha nyuma YAAMULIWAYO?

Tutulie na SAIDA KAROLI azungumzie MAPENZI KIZUNGUZUNGU....

Au turudi tu tena kwa LORD Kitchener azungumziye matibabu ya DR KITCH...

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 6:49 am  

Kaka nimepita kibarazani kwako kuchota hekima za hapa mawazoni.

Je u hali gani?

Simon Kitururu 7:42 pm  

Asante Dada Koero!Mimi sijambo naendelea tu kupumua.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP