Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama PENZI limekufa ,HUWEZI lifufua MOCHWARI!:-(

>> Thursday, January 29, 2009

Kama Mapenzi hufa,
............kabla ya kuzikwa labda yako MOCHWARI.


Maiti kabla haijazikwa bado imekufa,
.........kabla ya GEST-KABURI hupelekwa MOCHWARI


Na penzi huanza kufa,
.........pale wapendanao WAPUMZIKAPO kwa kudhania mambo yako shwari.


Kama unaPENZI ndio mwenye penzi liwezalo kufa,
......kwa kujisahau kulihudumia, usishangae kulikuta MOCHWARI.


Hivi twasubiri mpaka UMATI ujue penzi limekufa,
.......ndio tujifanye kupeleka penzi gereji au tuamini mambo si shwari?


Tibu penzi wakati lina dalili ya kifafa,
....... halitibiki tena kama lishafika MOCHWARI.
---------------------------------------------------------------------------------
Swali:

  • Si unahitajika kuwa na MPENZI kabla ya kuachana na MPENZI?
  • Si inawezekana hukuwa na MPENZI wakati unafikiria kumuacha MPENZI?
SIKU NJEMA!
NAWAZA tu MKUU!
Nakuacha na ISLEY Brothers wazungumzie penzi .....(tahadhari:wimbo wa kikubwa)

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 12:04 pm  

MMMh nimerudi kijiweni, nipo miji ya watu. Hili kweli kabisaaaaaaaa! mtu unajifanya kuonyesha machungu kumbe ujinga wa machungu unakolezwa na igizo la komedi za machungu duh!

Simon Kitururu 7:15 pm  

@Markus:Karibu tena!Kuhusu swala.....,KAZI kwelikweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP