Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BINADAMU katikati ya MAPENZI ya PUA NA KAMASI!

>> Friday, January 23, 2009

Labda SI kitu rahisi kuwa PUA au KAMASI.
Masikini PUA mpaka HUBINYWA atoe KAMASI.

PUA, pamoja na yote , ni nyumba ya KAMASI...
....ingawa mwenye MAFUA pua haina krisiMASI.

Kwa WALIMWENGU wasiothaminisha PENZI kama tu wathamanishavyo KAMASI.......
......Pua ni TUNDU la kupumulia na si nyumba ya KAMASI.

Kama kupumulia PUA ni muhimu kwa PUA kuliko KAMASI,.....
....apumuliaye MDOMO hapendwi na PUA yenye KAMASI.

Pamoja na yote....
....Kitu cha tatu AMBACHO NI MTU ndio KIINGILIACHO PENZI la pua na KAMASI.

....Kitu cha tatu hiki HUINGILIA hata PENZI LA BINADAMU wawili wapendanao kwa sababu wako nasi na hawana KAMASI.


Katika wawili WAPENDANAO kama pua na KAMASI....
.....Ni MIMI au WEWE tumpengeshaye mmoja PENZI lake kwa mwenziye na kulitoa kama PUA kutoa KAMASI.
PENZI lao likiisha na chuki kunawili, bado twajifanya tunashughuli na hatutaki wale nasi.

Kama WAWILI wamependana kama PUA na KAMASI......
....Kwa nini tusihemee mdomo na kumuachia pua KAMASI?

----------------------------------------------------------------------------------

Nawaza tu MKUU na NIMEACHA!
Swali:

  • Unakumbuka penzi lako na mpenzi linaweza kufa kwa msaada wa mtu wa tatu asiyehusika katika shughuli zako na PENZI?

  • Ushawahi kuwa na hamu ya kupata mafua ili ufanye mazoezi ya KUPENGA?


Au kama unamuda, mpate ZE FRANK azungumzie tukutananayo kwenye WEB katika jitihada za kuchekesha ingawa sina uhakika kama inachekesha ,katika What's so funny about the Web?....


Au mtoto anune....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP