Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SWALA la DUA la kuku KUTOMFANYA mwewe AKONDE!

>> Tuesday, January 06, 2009

LABDA...
...DUA au hata laana haikuathiri kama hujui umelaaniwa au umeombewa DUA uwe na DOMO kama UPAWA.

Inawezekana kama dua au laana ingekuwa inashika...

  • WAYAHUDI wangeshaISHA hapa duniani kwa laana na dua za WAISLAMU .
  • Uislamu ungeisha kwa dua na sala za Wakristo.
  • Ukristo ungeisha kwa sala na dua za Waislamu.
  • Rais Bush, Mugabe ,Kikwete au mwanadada mzuri akuringiaye, wangesha kuwa WENDAWAZIMU.

Labda..

...unahitajika KUUA au KUJIUA , kwa laana au dua la kuua litimie.

Labda...

... Kwa waombeao KIFANYIKE , wakumbuke tu hata mimba HAIINGII bila WENYE NACHO kuhangaikaNACHO.

Swali:

  • Kama kuna wafungao na kutuombea sisi wenye dhambi tusamehewe, unafikiri kwanini JEHANAMU inaendelea kuwepo?
  • Unafikiri MWEWE wako anajua DUA LAKO la kuku?




NAACHA!


Tupumzike kwa kurudi tena Kenya kwa UKOO FULANI+MM -katika MASHAIRI....


AU tu Lee ''SRATCH'' Perry azungumzie SOUL FIRE....

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 5:20 am  

wanasema dua la kuku halimpati mwewe.
habari za siku kaka.

Nili miss sana hii falsafa yako ya mawazoni.
Je ulikuwa wapi?

MARKUS MPANGALA 1:01 pm  

Duu wanapoombea wenzao DUA hilo wanasahau nao wanaweza kuombewa, lakini uombaji unaweza kutofautiana. Labda waombaji waliopo karibu na mungu wanaweza kupona kutunga MIMBA, pengine hawajui wanatunga vipi ndiyo maana wanaombea wenzao DUA watungiwe mimba. Hata hivyo wanasahau kuwa kumsamehe mwenye dhambi ni sawa na kumwona mchungaji anahubiri halafu anamkodolea macho ya kukonyeza kwa dada fulani, anamwombea DUA la mabaya ati ameshindwa kumtimizia kile asemacho TUSINYIMANE eti ni dhambi kumnyima mwenzio. Eti akisikiliza nyimbo za dini na kufunga mfungo wa BIA na MAOMBEZI hawezi kutunga MIMBA, labda haendi kutunga DHAMBI ili asione jehanamu,Pengine twaweza kunyimwa bila kudhani dhambi lakini tukihangaikia kutunga DHAMBI tutakweda jehanamu na wanaoombea mabaya watakwenda kuosha miguu ya watenda dhambi Hee inawezekana kabisa tukakosa DHAMBI halafu tukawa na jehanamu, halafu DUA TUTAMWOMBEA nani sijui labda yule asiyejua kutungaMIMBA halafu akasahau jehanamu ipo ipo kwanza.

Mmm kaka Simon najifunza kuwa MAWAZONI napenda sana eeeh falsafa zako we acha tu

Christian Bwaya 3:23 pm  

Kazi nzuri sana Katibu. Napenda unavyoweza kuwasilisha ujumbe mzito kwa lugha isiyobashirika.

Kama kuna mtu anadai hakuelewi, mwambie "...mimi nimewaandikia wanaoelewa..."

Simon Kitururu 4:11 pm  

@Dada Koero:Mimi mzima kiasi!Mchanganyiko wa kuumwa na shughuli uliondoa kidogo hapa kijiweni.Nashukuru bado unanitembelea hapakijiweni:-)

@Mzee wa Nyasa:Nikikunukuu; ''Duu wanapoombea wenzao DUA hilo wanasahau nao wanaweza kuombewa''. Ubinadamu kazi kweli!:-(Nashukuru kuwa sijakuboa Mkuu!:-)

@Bwaya:Asante sana Bwaya! Karibu tena na tena kijiweni!:-)

Anonymous 11:56 am  

Sijafahamu bado dua maanake nini kusema ukweli...kumtakia mtu vyema kwa mfano haumaanishi kuwa atakuwa na maisha mema...kibinafsi heri vitendo kuliko dua...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP