Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA bado WA KWANZA DARASANI ndiye mwenye AKILI!

>> Friday, January 02, 2009

KATIKA darasa la WATU WAWILI, wote wawili si lazima wakawa WA KWANZA DARASANI.

Labda...
...katika darasa la wawili , WOTE wawili ni WA MWISHO DARASANI kwa kuwa wote wamepata TISINI na TISA.

Katika darasa la WATU MIA waliopata MIA katika MTIHANI, karibu wote WANAMUHISI au KUMJUA ni nani wa kwanza NA NANI wa MWISHO, ingawa wote wana MAKSI MIA.

Tatizo ni....
... ujitahidivyo kwa KUTOKULALA kujifunza KUPIKA NJEGERE au NYANYA, kuna agunduaye KABLA YA KUJITAHIDI kuzila mbaazi,njegere au nyanya MBICHI kwa furaha BILA kujishughulisha na AKAkuzidi AFYA.


NDIO!.....
....Wa kwanza darasani anaAKILI!

Lakini....
....mwenye akili wa kwanza darasani, anaweza akawa ni MTAALAMU wa KUKARIRI , na SHUGHULI YA LEO ni ya UBUNIFU na si ya KUKARIRI kama aliyekariri Biblia, Korani au staili zakuonja TUNDA katika KAMASUTRA.

Na ni kweli....
....Wa kwanza DARASANI ana AKILI na ATASIFIWA!

Lakini.....
....unajua WA MWISHO kajifunza nini kwa KUWA WA MWISHO ambacho ndio kimfanyacho labda KATIKA darasa la MAISHA yeye NI WA KWANZA?


NAACHA!

Au tujifunze kuibia MTIHANI kiduchu....katika.....How to cheat on any test


Au tu labda tusikilize ujinga kama MOVADO ajisifiavyo katika UGANGWE..katika.. TOP SHOTTA nuh MISS

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP