Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hata mwanamuziki awe mzuri vipi, SI kila wimbo wake UNATEKENYA sikio na ROHO!

>> Friday, January 16, 2009

Inawezekana kuna mpaka nyimbo za dini ambazo ni MATUSI kwa MPAGANI!


Na ni KWELI,...
.....NYIMBO zote ni KELELE!


Swali:

  • Unafikiri wapagani hawakwaziki au kuudhika na biashara za wauza MUNGU kwa mahubiri au nyimbo?
  • Kwani ni Waothodoksi tu wa Urusi ndio hawapendi wafuasi wao waimbiwe nyimbo za dini nyingine?

Labda...
.... kuna wimbo unaupenda kwa sababu unakukumbusha tu kuwa UNA NJAA!
Na....
....kunasababu zaidi ya uzuri tu wa wimbo katika upendaji wako wa wimbo zaidi ya UUSIKIAVYO WIMBO ikiwa HILO LIWIMBO lina kukumbusha hata marehemu KIROBOTO au siku liMTU ulipendalo lilipo KUKATALIA mahaba na kukuepusha kuchunwa BEBERU.

Lakini pia...

....Ufurahishavyo kwa hili, lijalo waweza kumliza KAMANDA.
Swali:
  • Kwani ufanyalo limchekeshalo Halufani ni lazima limchekeshe ABDALAH?

WikIENdi nJEMa!

Ngojea BOBBY McFERRIN akumbushie DON'T WORRY BE HAPPY

Au turudi AFRIKA tukatulie na BAABA MAAL azungumzie - NGALU

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 9:00 pm  

Hongera kwa kutimiza mwaka Simon. Sherehekea na nendelea kusikiza nyimbo zotezote....

Simon Kitururu 5:29 am  

Asante Serina!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP