Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BADO nina wasiwasi na URAIA wa RAIS NYERERE!:-(

>> Thursday, February 12, 2009

KWA sifa anasifiwa na RAIA,...
.....mpaka na VIONGOZI wamwitao MWALIMU.


KAMA wanafunzi-WASIFIWA ni RAIA,....
...... wadai ni ujanja kudai wafanya ya MWALIMU,
.....mbona .....
ya WANAFUNZI-viongozi RAIA,....
..... wafanyayo HAYAFANANI na ya MWALIMU?


Labda tatizo ni mmoja haleti URAIA,.....
...... kati ya hili mwanafunzi au yule MWALIMU.

Kwa sababu WANAFUNZI wako hai na watajitetea URAIA,...
..... ngoja ni ridhike na wasiwasi wa URAIA wa MWALIMU.:-(

Na labda sielewi somo la URAIA,....
......yawezekana kufaidi nchi kiraia, yabidi kiufisadi uwe MWALIMU.

Kwanini Haleluya ni ya wote RAIA,....
......na AMEN yamfaidisha ambaye kwenye kitu TU ni MWALIMU?
__________________________________________________
Swali:

  • Kwani ni KWELI mwalimu alipatia mpaka wanafunzi wafuate ya Mwalimu?

NAACHA UJINGA!:-(

SIKU NJEMA ,au tulia tu na yasio SIASA kama ya WYCLEF akiongelea ya msichana katika- Guantanamera

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 11:54 pm  

Umenifanya hata nianze kuu-question pia uraia wa Yesu kwani naye wanafunzi-viongozi raia wake mwendo wao ni mbagombago (zigzag) pia.

Simon Kitururu 12:36 am  

@Profesa: Lakini WANAFUNZI- VIONGOZI raia wa Yesu ndio hao wenye nyumba na magari mazuri mpaka kwenye vijiji vya kigagagigikoko:-(Labda ni kweli raia:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP