Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama BINADAMU atafikiria hata MALALAMIKO ya mbu MJAMZITO , atafutaye PROTINI kwa kunyonya DAMU hata ya MJAMZITO!

>> Friday, January 30, 2009

Na labda Mbu jike tunayempiga na kang'atuka,
...... mchango wa nguvu za mwili katugea.

Katika dunia ambayo wadhaifu hutoweka ,
...... si binadamu wadhaifu wakesho watakao ilea.

Maringo ya viumbe vingine kwa binadamu MHUSIKA,
.......... hakuna kingine zaidi ya chanzo TU cha magonjwa kuenea.:-(

Lakini nguvu ya binadamu kuhimili magonjwa husika ,
................ si huhitaji mazoezi ya kuhimili maradhi yaliyoenea?

Nipe nikupe ni mchezo wachezao WANYAMA na MIMEA husika,
....ingawa binadamu huchukua bila kutoa hata katika KUMEA.

Wadudu, minyoo wapata shida wahangaika,
.......kwa binadamu kuhangaikia kughairi kufa tofauti na mimea.

Binadamu sumu ajifunza kutokuila ninahakika,
............ingawa apulizia SUMU mpaka HEWA.

Alalamika kama vile BINADAMU yamuumizayo kichwa akilalamika,
....... hayasaidii akili au hata umbea.

Yajulikana lakini akili za kijeba zamjulisha kama sio hata ya malaika,
.............basi angalau ajue baada ya YA kutambaa kuna ya kutembea.

Akili zamjulisha mbu AUMAYE ni protini kwaajili ya mimba zimfanyazo anahangaika,
.........zifanyayo DAMU anainyemelea.

Mbu ajishughulisha MPAKA kwenye giza anaimba akishughulika,
......mimba kuilelea.

Cha ajabu binadamu kuhusu ya mbu yanayomshughulisha nauhakika,
........ si ya MBU bali ya MTU kumtetea.

Aua MBU mhusika,
...... kwa kukwepa denge na malaria.

Lakini....

Mnyoo Binadamu amshughulisha kuhakikisha ikibidi anarutubika,
...... ili udongo wa rutuba aendelee kuulea.

Kasitukia kinyesi cha mnyoo aliyeumbika,
.... kwa udongo BINADAMU autegemeao ni mbolea.

Twakumbuka JONGOO na viumbe vingine HUSIKA ,
.....dunia vyailea?


Na kama binadamu DUNIANI ndio kiumbe pekee husika,
........ bila viumbe vingine duniani BINADAMU pekee aweza kuilea?
__________________________________________________________

NAACHA!
NAWAZA tu hapa kuhusu viumbe vingine ambavyo vinalazimika kuishi na binadamu hapa DUNIANI.
Swali:

  • Unafikiria KIBANO na hali ya viumbe vingine zaidi ya binadamu WENZAKO hapa DUNIANI ingawa sisi binadamu wenyewe maisha magumu halafu tunakufa?
  • Si ulishawahi kujiuliza kwanini ni mbu jike ahitajiye damu akupaye malaria?

Tutulie na LABI SIFFRE akisema - SOMEthing inside SO Strong.

Au LABI SIFFRE aendeleze kwa kusema tena -WATCH ME...

DUH!

WikieNDI NjeMa!
Turudi Tanzania kwa PAPI KOCHA na NGUZA VIKING waseme ya mpenzi -SEA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP