Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASILI ya MIIKO kwangu na UASISI /MWASISI wa ni nini MWIKO kwako!:-(

>> Tuesday, January 26, 2010

Asili ya vingi ambavyo ni mwiko kwangu ni KUTISHWA ,...

... na vingi ambavyo bado kwangu ni MWIKO na ambavyo sijatafuta sababu zake ni kwanini ni MWIKO, sababu za hiyo miiko bado SIJAPATA.

LAKINI pamoja na sababu ya MWIKO yaweza kuwa ni kutishwa BADO ni MWIKO !:-(
Na MWIKO kwako labda sio MWIKO kwa wengine hata kama hukutishwa,...
... na kwa hilo ukitafuta sababu ni kwanini , sababu UTAPATA.:-(

LAKINI pamoja na sababu ya MWIKO KWA WENGINE yaweza kuwa sio kutishwa BADO ni MWIKO !:-(Na kwa wengine ni MWIKO kula KITIMOTO, au KUTAHIRIWA ,..

... wakati wengine MWIKO ni POMBE kama Uarabuni , au wengine ilivyokuwa sio mwiko katika mila baadhi kucheza ngoma matiti nje kama TANZANIA, au tu RUKSA bangi kidogo kama Uhindini,...

....ingawa NA kwa wengine Msichana mkubwa kuoga uchi na baba yake ni RUKSA na sio MWIKO kama Ufini, au tu Mwanamume kumuoa Mwanamume mwenzako ilivyo RUKSA na sio MWIKO Sweden ,....


... na ukitafuta sababu , UTAPATA.


Swali:

  • Unafikiri asili ya MIIKO ambayo kwako ni MWIKO ni nini?

  • Unafikiri kushika MAKAA YA MOTO wakati wewe na kila MTU wanajua MOTO UNAUNGUZA ni mwiko?
  • Unauhakika MIIKO ya wengine kwako inaleta MAANA?

  • Unafikiri MIIKO yako kwa wengine INALETA maana?


Ndio KILA MWIKO unaasili zake,....
..... na labda kama kuna asiyevunja MIIKO basi kila MWIKO itafikia hakuna ajuaye kwa uhakika sababu ZA UZALIWA wake kitu ambacho kitasababisha KUNA KIZAZI CHA UMMA NA KIJIKO kitahitaji kuwe na PROFESA afanyaye utafiti wa KUVUMBUA ni kwanini baadhi ya JAMII ziliamua ni mkono wakushoto ndio wa kuchambia mavi na kufanya baadhi ya jamii kufanya ni MWIKO kuutumia MKONO HUO wa KUSHOTO kumsalimia mgeni au kuutumia kuchovyea tonge la UGALI WA YANGA kwenye bakuli moja la maharage swafi ya nazi,- na yote hayo IKIWA TU ni katika juhudi za kujaribu kuelewa MWIKO.:-(


Na ni kweli MWIKO unaasili yake,...
... na baadhi ya miiko ya hapo baadaye labda MWASISI ni wewe na tabia zako!:-(


Ni wazo tu hili Mheshimiwa USIKONDE!

Na hebu R. Kelly abadili kwa-Bump & GrindAu tu Wu Tang Clan warudie- The heart gently Weeps

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP