Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hongera Rais ZUMA kwa kuoa MKE wa TATU kiwaziwazi!

>> Tuesday, January 05, 2010

Pamoja na Rais Zuma wa AFRIKA KUSINI kulalamikiwa na baadhi ya watu kibao kwa uamuzi wake wa kujipatia JIKO la TATU kwa madai yapewayo nguvu na apendavyo kutunza MILA na DESTURI za KABILA lake,.....

....twaweza pia kupata changamoto kwa kujiuliza hivi ni MILA na DESTURI zipi ambazo ni busara kuzitunza.


Na wakati tunafikiria hilo kama tu kawaida ya WANYOSHEA VIDOLE wengine katika yao,...
..... twaweza pia kujiuliza HIVI watoto wazaliwao leo AFRIKA hasa mijini ni mila gani NA DESTURI za KIAFRIKA ambazo wanajifunza na kujivunia ili hapo baadaye angalau wawe na CHAKUJIVUNIA?




Halafu:

  • Kwani unafikiri ni watu wangapi ambao hawakiri tu kuwa na WAKE WENGI kisa kuna MILA na DESTURI labda hata zidaiwazo ni za KIKRISTO ambazo wanazitunza kinafiki kwa kuwa wanawasiwasi watu watawaonaje kwa hiyo nyumba ndogo zao a.k.a WAKE WENGINE wanawafanya siri?

  • Kiislamu inajulikana kuwa kama unaweza ni ruksa kuwa na wake kadhaa LAKINI unafikiri KIKRISTO ni kipindi gani WAKE LUKUKI ilibadilishwa na MKE MMOJA ikawa ndio mswano wakati yajulikana akina King David , Solomon na watu kadhaa ambao wanaheshimiwa KIBIBLIA walikuwa na WAKE LUKUKI?

  • Unafikiri huyu mke wa tatu wa Rais ZUMA alimuomba RAis ZUMA apimwe UKIMWI kabla hajamkubalia hasa kwa kuwa inajulikana na DUNIA nzima Rais ZUMA alisha ngonoka na Mwanadada mwenye UKIMWI na kudai ili kuzuia VIRUSI alioga chapuchapu?



HONGERA Rais ZUMA kwa kutoficha udhaifu wako kama wengine watusaidiao kueneza UASHERATI mtaani KISIRI wapendavyo kukaa viti vya mbele MAKANISANI na kujifanya NANIHII hawananihii!.:-(


Hebu ZE COMEDY wabadili kwa- SEGERE


Au tu FATUMA RAJABU alete -DOMO LA UPAWA

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Upepo Mwanana 3:01 pm  

Zuma ana sifa kubwa ya kuhusudu masuala ya ngono. Kaahalalisha rasmi ili watu wasimpake matope.
Nasikia ana watoto karibu ya 20!! wakiwemo wa chini ya miaka 5

Simon Kitururu 6:19 pm  

@Upepo Mwanana: Inasemekan ni hivyo ! Demu akimchekea anamkaribisha ikulu kwa dhumuni la tumbuizo PEMBEJEO sehemu za siri.

Lakini hayuko peke yake watu kibao wanafanya siri tu lakini wao fulu kunogewa na NANIHII!:-(

Faith S Hilary 4:42 am  

ZULU PRESIDENT!!!!!!!! NANI KAMA YEYE? Kazi kweli kweli...mke wa tatu...ndoa ya 5...LIFE IS GOOD KAKA SIMON...lol

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 9:10 am  

Yawezekana kati ya wale wanaomzodoa akiwemo Mt. Simon ni wale wanaokizimikia hicho kifaa alichokibeba na wanatamani japo wapate busu lake badala ya kupata busu la mdoli... :-(

kwa wakurya ni ruksaaa kuwa na wake wengi na kwa wale wanaosema umaskini ni wa kipato kikurya maskini ni yule mwenye mke mmoja (wakati wa kula ze ugimbi yeye hukaa mlangoni!), watoto kiduchu, ngombe kiduchu na shamba dogo...:-(

Nami karibu ntaanza kbandika maobi ya wanaotaka kuolewa.... :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP