Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kuna afikiriaye ana MUDA wa kufanya AFIKIRIALO na awezalo SASA HIVI, baadaye!

>> Wednesday, January 13, 2010

Kama unachakufanya SASA HIVI,...
... na UNAMUDA SASA HIVI labda ni busara UKIFANYA SASA HIVI.



Ndio najua,....

.... labda unahisi una MUDA baadaye wa kufanya ambacho ungeweza kufanya SASA HIVI,....

... kitu ambacho kinafanya WAZO LAKO limekaa mkao wa sentensi ,...

-`` NAJUA nina muda baadaye HALAFU najisikia UVIVU KWELI kufanya kitu kingine wakati kwenye TV kuna bonge la ISIDINGO sasa HIVI´´ .



Swali:
  • AU?

Lakini ,....
.....hebu tuangalie pia madhara yawezayo kujitokeza IKIWA kila mtu atafanya atakacho kufanya sasa hivi:

  • Labda ungebakwa sasa hivi kwa kuwa labda kuna litokwalo na udenda KUHUSU WEWE ambalo litakalo kufanya ni kukuonja hata kinguvu SASA HIVI.:-(


  • Labda Ungekufa sasa hivi kwa kuwa nia yako ni kujiua kwa kuwa unajisikia kufakufa kwa kuwa maisha magumu au tu unahisi ile siri yako ndio ishajulikana SASA HIVI .:-(

  • Labda ungetajirika sasa hivi kwa kuwa ambacho ungefanya sasa hivi na sio kukifikiria TU ndio siri ya umilionea kwako kama utakivalia njuga SASA HIVI .:-(

  • Labda ungestukia ujinga wa swala zima UFIKIRIALO NI BONGE LA BUSARA baada ya kulijaribu kwa kuwa ukweli ni kwamba ni la kijinga na kwako ni mpaka ulitende ndio utastukia ,kwa hiyo kwa kifupi unajichelewesha kustukia ujinga wako kwa kutofanya kitu SASA HIVI.

  • Kuna uwezekano UKATALIWACHO ungekubaliwa sasa hivi kwa kuwa utakaye kumuomba anajisikia kukubali SASA HIVI.
Swali:

  • Hufikiri labda kuna umuhimu pia wa KUKOSA SABABU ZA kwanini hufanyi sasa hivi ingawa ungeweza kufanya KITU sasa hivi?

  • Unafikiri hakuna WATANZANIA wajifunzalo kwa kutofanya sasa hivi kitu ambacho kinawawezesha kulisaidia TAIFA LA TANZANIA liendelee kuwa MASIKINI sasa hivi kitu ambacho ni funzo kubwa kwa WATANZANIA la somo muhimu la : ``Busara za MASIKINI katika umasikini muhimu ni nini kitu ambacho wananchi wa mataifa matajiri kibusara WANAKOSA´´?


NI wazo tu HILI na NIMEACHA mheshimiwa!


Ngojea DWELE alete- I'm CHEATIN'

Au tu DWELE na SLUM VILLAGE wazungumzie-Tainted

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP