Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jamani jamani SHIKAMOO MPENZI![Sentensi HII imebaniwa pua na demu mwenye mafua.:-(]

>> Saturday, January 30, 2010

Na kuna watoao SHIKAMOO mpenzi ,....
... kama mkakati wa KISIRI wakumuambia MTU kiumri amezidi sana na KWA HILO kukwazwa asiombe PENZI.


LAKINI kwa kuwa HATA kama kwa UMRI ni mkubwa MPENZI,...
.... kumbuka lake laweza kuwa ni CHANGA na ndio kwanza limezaliwa tu PENZI.
Swali:
  • AU?SHIKAMOO KIPENZI,..
... yaweza toka kwa AHESHIMUYE lako PENZI.

Na kwa kuwa anakua KIPENZI,...
...umri wako na wake waweza kuwa UNAANZA kufanana kama kipimo ni PENZI.

Kwa kuwa KIPENZI,....
.... wakati wengine PENZI LAO linakua, wapo ambao WANAPIGA MAKITAIMU kipenzi.:-(

Kwa kuwa KIPENZI,...
... wakati wengine PENZI LAO LINABALEHE, wapo ambao PENZI LAO linakufa MPENZI.


Na SHIKAMOO MPENZI,....
....inaweza kufikia kumaanisha tu``SHIKAMOO MPENZI bila PENZI´´ kwa kuwa labda ni kweli kwa kuwa PENZI HUZALIWA, ....
... basi labda pia HUKUA, hudumaa, hunywea, na KUFA tu kama vingine vizaliwavyo MPENZI.

Swali:

  • AU?

  • Hivi SHIKAMOO maana yake ni nini vile?

  • Sasa hivi ni MPENZI au PENZI lake listahililo SHIKAMOO?

  • Tukiachana na PENZI na kuingia kwenye SALAMU TU,- NI mara ngapi weye MTZ utumiaye SHIKAMOO kama salamu huwa unamaanisha hiyo SHIKAMOO KISALAMU kwa umsabahiye?
NI wazo tu hili MKUU na NIMELIACHA ingawa kwako ni RUKSA kulifikiria kivyovyote vile UPENDAVYO Mheshimiwa!

SHIKAMOO basi!
Umefurahi eeh!
Jumamosi NJEMA!

Au hebu Frankie Paul abadili hali ya hewa Kijiweni kwa kumuongelea - SARAFrankie Paul alete tena -SHUB eeN
Au tu Delinquent HABITS na Hurricane G wabadili zaidi tena kwa -Underground Connection [Tahadhari: lugha watumiayo haijaoshwa mdomo!:-(]


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 1:22 pm  

Mtu akikuambia shikamoo basi. Basi ujue kalazimishwa na hali tu , na wala si kwa heshima ya aina yoyote!
Wikend njema mkuu

EDNA 1:27 pm  

Shikamoo maana yake Nipo chini ya miguu yako....Me naona ingefutwa imekaa kimwinyi mwinyiiiiiiiiii?

Yasinta Ngonyani 5:26 pm  

"Jamani jamani SHIKAMOO MPENZI![Sentensi HII imebaniwa pua na demu mwenye mafua.:-(]" Na hii ya SHIKAMOO MPENZI nimeipenda :-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:37 am  

Shikamoo Ysinta

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 10:56 am  

@Mt. Simon: Kama da Edna anavosema ni kweli basi yaweza kuwa WEWE Mt. ukiambiwa SHIKAMOO MPENZI SIMONI basi maana yake ni NIKO CHINI YA MIGUU YAKO NIONE KAMA WAWEZA NIPA MIMBA MWAKA HUU :-(

Simon Kitururu 4:39 pm  

@Mkuu CHIB:Siutani usemalo Mkuu!:-(

@Dada Edna: Miye nakubaliana nawewe KABSAAA! Ila nasikia kutunza mila na desturi ni ujanja ati ndo maana wako wang'ang'aniao mila hata kama ni ya kuwakeketa vigoli.

@Dada Yasinta: :-)


@Kadinali Ngwanambiti: DUH!

Yasinta Ngonyani 5:03 pm  

Kamala unatafuta nini china ya miguu yangu? kama ni ni kweli maana ya SHIKAMOO ni upo chini ya miguu yangu?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP