Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UPROFESA wa nukuu za mstari mmoja MMOJA!

>> Tuesday, January 26, 2010

Napenda kunukuu hasa nikitaka kulazimisha hoja nayoshindwa kuijengea HOJA.:-(

Na nawajua wapendao kunukuu kwa kuwa hoja yao ili iaminike kama ni hoja kuna WAWASIKILIZAO wapendao kusikia angalau jina maarufu ambalo kimtazamo lakubaliana na ya mdau mpya HOJA.


Na haki ya nani kama hoja yako ni ya magimbi,...
... na ukaingizia`; ``NA Yesu alisema ......,´´
...... halafu ukamalizia na hoja zako za magimbi ni matamu kuliko Mihogo kuna watakaosita kukubishia KUHUSU UTAMU WA MAGIMBI ingawa WANAPENDA MIHOGO kisa umemnukuu tu Yesu katika ya kutetea magimbi HOJA.


Na kama ni siasa za Tanzania za kujisifia unakula tu magimbi ...
... na ukaingizia na`` Nyerere alisema.....,´´
.... halafu ukamalizia na kula UBWABWA PEKEE MBELE YAO wakati kwenye SINIA KUNA MAGIMBI PIA kuna ambao hawatasita kukuunga mkono na HOJA YAKO kuhusu magimbi NDIO CHAKULA PEKEE kifaacho kuliwa wakati wanashuhudia wewe unalenga na unaonyesha kwa vitendo ni mtu wa UBWABWA kisa umemnukuu Nyerere na umeingizia magimbi katika HOJA.

Ndio ,...
...kunauwezekano kuwa nimepitiliza kudhaifisha kiunyambulisho hoja ya magimbi hapo juu !:-(

Swali:
  • Si unakumbuka lakini nukuu za mstari mmoja miwili katika STORI ya Bata Mjamzito inaweza ikafiti vizuri kuzungumzia au tu kujenga madhari kuwa stori ni ya mbuzi /BEBERU lisilo basha?

  • Kama wewe ni Mkristo kwani hujawahi kufanikiwa kusikiliza mahubiri yaliyojengewa hoja na baadhi ya vifungu vya BIBLIA halafu baadaye ukaendelea kusoma vile vifungu na kugundua wala haviendani na hoja viliyoisaidia wakati mchungaji anashuka mahubiri Kanisani?


Ndio,....
... tuna nukuu na baadhi ya nukuu haki ya nani lazima umtishe mtu kuwa wewe MSOMI SANA kama ukipatia kunukuu,.....
....na si utani kuna mpaka MAPROFESA wa nukuu za mstari mmoja mmoja na katika kuipamba hoja utakuta mtu anaweza kukusimulia stori hata ya MBWA kiruka njia halafu akanukuliwa kuanzia Plato, Socrates, Nyerere, Rais Mkapa , Askofu Mkoba, mpaka MIMI katika kukuelezea kwa nini mbwa yule hajapata bado gono na mbwa wenzake wanafikiri ni mchoyo wa MIFUPA katika jamii ya MBWA katika tu kujenga HOJA.


NAACHIA HAPA nikiamini unajua hili ni wazo tu na labda halina hata UKWELI!

Na katika nukuu za tishatoto za ghafla hapa nami nanukuu bila sababu maalumu;
~Andre Gide akidai ´´Believe those who are seeking the truth. Doubt those who find it.´´

Na ~Alfred Lord Tennyson adai :``I am a part of all that I have met. ´´


Na ~Baba Ram Dass adai ``Only that in you which is me can hear what I'm saying. ´´

Swali:
  • Umestukia ni hoja mamilioni mangapi nukuu hizo zaweza kuingizwa bila mtu kujua wakati wanaziongea NILIOWANUKUU walikuwa wanaongelea nini?


Hebu tuamishwe kimawazo na RZA arudishe ya dunia katika -La Rumba




Au tu Zain Bhikha arudishe busara za Mungu katika- Allah knows

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP