Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mapungufu yajitokezayo katika NENO kutokana na UANGALIFU wa MTOA NENO!

>> Saturday, January 09, 2010


....kwa bahati mbaya UANGALIFU wa kitu wahitaji UJUZI wa kitu ,....
...... na kama WEYE unalimaindi NENO lako na unataka LISIPOTEE bure,...

... kwa mafanikio zaidi basi angalau MJUE umlengaye kwa hilo NENO.:-(

Swali:
  • Lakini pia si unakumbuka kujua tumizi hata la kikombe haitoshi kama hujui jinsi ya kukihifadhi kikombe, kama unakitakia maisha marefu kikombe?


...na BILA kumjua umlengaye kwa NENO ambalo unafikiria KATIKA UMAANA lina kitu,...
....waweza KUMCHEKESHA utakaye KUMKASIRISHA hata kwa kumlenga kwa TUSI ambalo kwako unafikiri ni TUSI KALI katika LAKO neno.:-(Swali:

  • Si umestukia hata maneno ya MWALIMU umuelewaye na kupasi MTIHANI ukimuuliza atakuambia anajua wanafunzi wake wanaofeli kwa kutomuelewa neno?

  • Si umestukia hata MAHUBIRI ya ASKOFU au mawaidha ya SHEKHE yakugusayo kwa neno huwa hayagusi waumini wote ndio manaa inasemekana kunawatakao kwenda jehanamu kwa hilo?


  • Na si unajua neno ulengwalo NALO likikukolea kwa kawaida mtu huanza kufikiri ndio kweli yenyewe KABISAAA kitu ambacho ndio kisa cha Papa WAKIKATOLIKI au tu Askofu wa Kilutherani kufikiri WASABATO kwa kusali jumamosi na kutokunywa mvinyo wenye KILEVI a.k.a pombe kanisani NI MATOKEO ya kuna neno la YESU hawajaelewa?


  • Si unajua kwako usiyenielewa , neno langu hapa katika blogu hii mie SIMON Kitururu LABDA mlengwa sio wewe?

  • Unabisha?
  • Unafikiri YESU anaeleweka?


NDIO ,...

... kunauwezekano wakati WEWE ni muangalifu hata wa NENO akutazamaye na kukusikiliza anaweza akawa ni yule ambaye kwake UMEZIDISHA makali ya neno na unavyozidi KUMTONGOZA mwenzio anafikiri UNAMKARIPIA.:-(
Ndio,...
... neno lina ubinafsi KATIKA KULIELEWA na kipimo ni wewe mwenyewe ndio maana wakati mie Mtakatifu Simon Kitururu wakati nafikiri nahubiri NENO weye waweza kudhani NATUKANA kwa kuwa utumiacho katika kupima uzito wa neno ni chako binafsi.:-(

Ndio,...
... katika neno hata YESU hakueleweka na KWA HIYO kama WEYE MTANZANIA unawafuatilia wafuasi wa NYERERE Tanzania leo hii usishangae kustukia karibu wote neno lake pia hawakuelewa.:-(Swali katokori:
  • Unanielewa naongea nini MHESHIMIWA katika hili neno?

  • Unafikiri wewe wakati MWANGALIFU misingi ya uangalifu wako hata wa ili usijetukana bure ni nini?

  • Si unakumbuka ukimtusi mwenye KICHWA kama DAFU kwa kukifananisha kichwa chake na`` Kichwa kama tako la MZEE´´ yawezekana ni tusi?NIMEACHA wazo Mheshimiwa KIKORE na kumbuka hili ni WAZO tu MKUU na ni ruksa kutolielewa!


Ngojea nimuachie BOPOL MANSIAMINA katika gita na ASSAKA BABA LEY katika kipaza sauti au tu ORCHESTRE MODE SUCCES waje na -Pitie, Je veux la reconciliation


Au tu ngojea tuyarudi magoma moto kutoka kwa Mheshimiwa MCHUNGAJI MUNISHI ashushe kitu kizito kiitwacho-Nawaombea WANAHABARI

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:54 pm  

Nanukuu "Ndio,...

... neno lina ubinafsi KATIKA KULIELEWA na kipimo ni wewe mwenyewe ndio maana wakati mie Mtakatifu Simon Kitururu wakati nafikiri nahubiri NENO weye waweza kudhani NATUKANA kwa kuwa utumiacho katika kupima uzito wa neno ni chako binafsi.:-(" mwisho wa kunukuu. Ni kweli kabisha mara nyingi kuna kutokuelewana kwasababu kila mtu anaelewa anavyotaka kulieliwa NENO.

Simon Kitururu 2:56 pm  

@Da Yasinta: Yani si utani Yasinta!:-(

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 3:00 pm  

Kwa bahati mbaya tumelelewa katika mazingira ya kushi kwa mazoea kuwa ni lazima tuelewe kila kitu...:-(

Na inapotokea kutoelewa neno..duh! hapo ndo kimbembe huanza :-))

Simon Kitururu 3:21 pm  

@Kadinali Ng'wanambiti: Si utani!:-(

Yasinta Ngonyani 3:46 pm  

Hivi ni kwa nini inakuwa hivi?

chib 12:25 pm  

Mt. naona umenena neno, yule anayesoma blog yako, kama hakuelewi... si mlengwa wa neno hilo :-)

Christian Bwaya 11:29 am  

Chib umenikumbusha yule mwandishi aliyekuwa akilalamikiwa na watu ati kwa nini unaandika vitabu vigumu kuvielewa? Yeye akajibu "kama huvielewi vitabu vyangu basi weye si mlengwa wa vitabu hivyo"!!!

[kama unasoma kitabu na hukielewi maana yake wewe si mwandikiwa wa kitabu husika. Tafuta ulichoandikiwa]

Blogu ya Baba Mtakatifu inaweza isiwe andiko sahihi kwa baadhi ya watu hasa waliokulia kwenye mazingira danganyifu (najaribu mara nyingi kutafuta muda wa kulielezea hili vizuri nashangaa siupatagi)

Yupo mwalimu wangu mmoja kasoma sana namjua ambaye mpaka kesho haelewagi kinachoandikwa humu. Feedback anayonipa-ga mara zote ni hisia za matusi.

Basi mie huelewa kwamba yule si mmoja wa walengwa wa maudhui ya humu ndani.

Baba Mtakatifu kazi mbele kwa mbele. Tunaokuelewa endelea kutuandikia:-)

Simon Kitururu 4:56 pm  

@Da Yasinta: Sina uhakika!:-(

@Mkuu CHIB + Mkuu Bwaya: Kuna uwezekano lakini kuwa ni staili ya kujihami kwa asiye eleweka kuchagua amlengaye kwa neno.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP