Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kuna WAONGEAJI watumiao sauti ili KUKAA KIMYA!

>> Wednesday, January 27, 2010

Wengi waongeao haki ya nani hawasemi KITU,...
....ndio maana usitishike na stori ndefu kwa kuwa kisemwacho chaweza kuwa kinajaa tu MSTARI.

Na ni kipaji kuwa KIMYA huku unaongea,...
..... na ajuliaye hicho kipaji NI mpaka baada ya kuagana naye ndio utastukia na kuanza kujiuliza:

  • Hivi jamaa lilikuwa linasema nini vile?
  • Hivi Mheshimiwa kunachochote kweli alichokuwa anajaribu kutuambia?

... kwa kuwa watumiao SAUTI kukaa kimya na wenye kipaji KWA HILO wakati unawasikiliza unaweza ukajiaminisha mwenyewe kuwa kuna kitu unapata katika waongealo.:-(



Na KWA MTAZAMO MWINGINE labda ukweli ni kwamba,...
.... ukichunguza utastukia kuwa tunaishi katika JAMII ambazo hufunza watu kuongea kwa SAUTI wakati huo huo katika baadhi ya mambo kukaa KIMYA.


Na labda ni kweli ukiniuliza miye ,....
.... KWA ASIYELAZIMIKA KUONGEA NAWE AKIFIKIA kuongea nawe ,....
huyo kashapitia UCHAGUZI wa afikiriacho kinafaa kukuongelesha, MANENO atakayotumia asije akakukwaza weye MSWAHILINA kwa maneno ya KILOKOLE au tu hata jinsi ya KUKUONGELESHA ustukie mahaba wakati neno mahaba limekaliwa KIMYA.


Swali:
  • Si unajikumbuka tu WEWE MWENYEWE wakati unaongea na MTU ukwepavyo baadhi ya MANENO, MAMBO au tu vitu fulani kimsisitizo, KIKUVIDOKEZEA au hata tu ugusiavyo baadhi ya mambo ili tu kufanikisha kukalia kimya baadhi ya mambo?

  • Si unajua stori yako ya kufeli mtihani iliyoko kichwani mwako itofautianavyo na umsimuliayo Mzazi?

  • Ukikutana na mtu si unastukia ni mambo mangapi ya kupitiayo kichwani kuhusu huyo mtu na wawezakung'amua ni asilimia ngapi ya mambo yamuhusuyo huyo mtu ambayo huyaongelei?
  • Kwani unafikiri kila unavyoongea kuna kitu hasa unachosema?


NI wazo tu HILI MKUU!


Samahani Caiphus Semenya yuko mawazoni tena na kitu - Angelina





Pat Shange naye arudie- Sweet Mama

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP