Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAISHA ya MALAYA yangekuwa kama UFIKIRIAVYO yawe!

>> Wednesday, January 13, 2010

Maisha yangekuwa kama UNAVYOPENDA kuyafikiri watu WAYAISHI,...

.... labda HATA UBWABWA ungekuwa haunogi kwa MPENDA CHUMVI kwa kuwa kusingegundulika hata CHUMVI duniani kama weye cha muhimu katika MAISHA YA BINADAMU sio kula chakula chenye chumvi DUNIANI .:-(


Maisha yangekuwa kama UNAVYOPENDA kuyafikiria watu WAYAISHI,...

.. labda watu wasingestukia kuna MUNGU bado kitu ambacho kingewanyima watu muongozo muhimu uendeshao maisha ya wengi waishivyo sasa hivi ya kuogopa kufanya DHAMBI ilikukwepa kumuudhi Mungu hapa DUNIANI.:-(

Swali:

  • Unafikiria uwezekano wa KUWA jinsi uyafikiriavyo maisha yako LABDA NI KINYUME na wayafikiriavyo watu kibao uwajuao ambavyo wanafikiri wangeishi maisha yako?
  • MAISHA ya MALAYA yangekuwa kama UFIKIRAVYO yawe unafikiri ungestukiaje AIDIA ya starehe ya limpenzi lako kwa kuwa ni lako tu NI TAMU?
  • SI huwa kuna wakati unafikiri ni sahihi zaidi ufikiriacho maishani mwako ni sahihi?
  • Maisha ayafikiriayo MSENGE yangekuwa kama ayafikiriavyo si kuna uwezekano kusingekuwa na asiye msenge?
  • Unafikiri Maisha yangekuwa kama UNAVYOPENDA kuyafikiri watu WAYAISHI kuna ambaye angepata muda au wazo la kugundua chupi, ASPIRIN au tu kukaanga dagaa kwa kuwa vyote vyanzo vya wazo lake haviko katika staili ya maisha bora yako, MATUMIZI BORA YA MUDA KWAKO ?


Ndio,...
.... ukifikiria sana unaweza kugundua mpaka umuhimu wa cha muhimu kwako unapata msaada sana kutokana na ukweli cha muhimu kwako si kwa wote ni MUHIMU.:-(


Swali katokori:
  • Si umestukia wakati nafikiria zaidi kupata muda wa kwenda kucheza au kuangalia mpira kuna ambaye wakati huo ANAAMINI ni muda mzuri wa kujisomea kitabu?:-(
  • Unafikiri kujua sana au kuelimika sana kunamanufaa au ni matumizi mazuri ya muda mfupi wa maisha ya mtu?

NI WAZO tu HILI MKUU usikonde!


Hebu Stevie Wonder alete-I don't know WHY



Au tu Stevie Wonder alete- I am FREE


Au tu Pavarotti na Stevie Wonder wamalizie kwa -Peace wanted just to be FREE

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 5:15 pm  

Swali kwako mtakatifu..... Unafikiriaje kwenda baa na kupoteza muda ukinywa? Kwa nini watu wasiende na vitabu kusoma wakati wakiwa huko au... :-(

Simon Kitururu 5:40 pm  

@Mkuu: Kwangu baa na vitabu haviendani. Kwangu nikiwa baa shule ni watu. Kinachotakiwa ni ujue tu unatafuta nini cha kukijua kuhusu watu.

Na naamini kuna mambo MABAAmeidi kama tu kwenye Taxi alivyo TAXI Driver ukitaka kujua hao ni Maprofesa.

Na kwangu pia kuna miziki ambayo nanogewa nayo BAA na CLUB tu nikiwa na kinywaji hasa wakati natafuta wazo jipya ambalo sijawahi lifikiria.


Na tusisahau katika waenda baa kumi ukiwachunguza utapata sababu tofauti kumi kwanini wako baa na labda hakuna hata mmoja katika hao sababu ni kustarehe.:-(

Yasinta Ngonyani 6:27 pm  

Karibu tena Mt. maana naona ulichukua likizo:-) humo mie simo

Simon Kitururu 6:30 pm  

@Dada Yasinta: Asante Mwanakwetu! Na asante kwa taarifa humo haumo.:-)

nyahbingi worrior. 7:22 pm  

Simon sijakupata ingawa sina cha kusema.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 8:15 am  

na kutokana na fikra hizo tofauti na hali halisi utakuta hata tunashindwa kuchagua vizuri :-)

kama wewe ulivochagua kuwa kimya kwa siku kadhaa :-(

Simon Kitururu 10:51 am  

@Rasta Luihamu: Kunauwezekano kabisa nachojaribu kusema hakieleweki.:-(


@Kadinali Ng'wanambiti: Si utani!:-(

Christian Bwaya 4:26 pm  

Mie huenda baa. Sinywi. Ila kutizama mabadiliko yanayoambatana na kimeo. Baa kuna mafunzo. Ni jela iliyo huru

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP