Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hasira kama HISIA ni CHACHANDU ya maisha na kama hukasiriki , labda nenda KAMUONE daktari!:-(

>> Friday, January 15, 2010

Kuna mambo kama HASIRA utakuta kuna BINADAMU hujaribu sana kuyakimbia,....
.... labda kwa kuwa huo ni UBINADAMU.

Kuna mambo kama HASIRA ili binadamu awe BINADAMU hawezi kuyakimbia,...
....na hiyo ndio hali halisi ya UBINADAMU.:-(Swali:
 • Si unakumbuka STAILI YA KUONYESHA HASIRA inaweza mpaka kutumika kama ushahidi kwa uliyewahi KUMSIKIA AKIDAI au mpaka hata uakaamini kuna mtu hana hasira?
 • KIHISIA ZA BINADAMU SI umestukia kama KIFO kingekuwa kinapigiwa kura na BINADAMU au tu kinaweza kukimbiwa labda kufa kusingekuwepo duniani na kwa BINADAMU kujaribu kufa kwa uzee ingekuwa ni kitendo cha kuvunja sheria?


Lakini,...
....kama wewe ni BINADAMU ,ukifikiria HATA SIO SANA waweza kugundua kuwa HISIA zako zote kama binadamu zina umuhimu wake KWA BINADAMU na kwahiyo si kitu cha kipuuzi HATA KAMA HISIA ZENYEWE katika muda husika ni JIPU LINAUMA , na labda zinakupa tu shughuli ili maisha yako yalete maana KIBINADAMU yaletavyo sasa MAISHANI MWAKO.Ndio ,...

......hisia zako ni MUHIMU.

Kwa mfano ,....
... hisia zako kama za:


 • Njaa- labda bila kusikia njaa wewe labda usingestukia ujivuniacho kuwa unaakili kwa kuwa tunajua tu kuwa unaakili kwa sababu ya ufanyayo kazi na labda kisa unafanya kazi hiyo ya utafiti wa mende NI kwa kuwa tu unalipwa mshahara ambao UNAUHITAJI ILI UNUNULIE CHAKULA,- na wala huzimii kiasi hicho mende , panya, au hata sehemu za siri za ng'ombe ambavyo vimekupa PHD kama mtafiti tukuzimiaye kwa MIAKILI.:-(

 • Huzuni- hasa kama unastukia mchango wa kuwa na huzuni katika FURAHA yako.

 • Kukasirika- hata kama hapa nikigusia kukasirika kwa wazazi WAKO kama umestukia mchango wake katika kukufunza abadu usiwe toto tukutu.

 • Kuchoka- katika kukusaidia kupumzika ili baadaye ufikirie upya kwa akili iliyotulia.

 • Au tu HISIA zikufanyazo uhisi UNANUKA KIKWAPA au tu sehemu za siri - zikusaidiavyo kukufanya utafute maji uoge , AU TU uwe msafi na mwenye AFYA zaidi kwa kuwa msafi.

Swali:
 • AU?
Tukirudi katika hoja ya kukasirika a.k.a HASIRA,....

.....kujinyima kukasirika mara kwa mara, kama tu matatizo ya kutunza sana nyege mshindo kwa wenye ukame ,- kwaweza kusababisha siku moja kikukeracho kidogo kikasababisha UKASIRIKE sana KUBWA KULIKO na kutuonyesha vioja bure MHESHIMIWA !Kwa kifupi,...
labda jitahidi kukasirika mara kwa mara angalau ufanye mazoezi ya kujulia jinsi ya kuporomosha hasira kistaarabu au tu kuepuka KUKASIRIKA SANA ghafla kisa tu umejilundikia hasira kibao za vitu vingi na hapa siongelei umkasirikiacho Rais Kikwete au tu JIRANI.:-(

Swali:
 • Kutunza hisia KAMA WEWE ni MUUDHURIAJI MISIBANI si unakustukia KILIONI hasa ukistukia kuna waliao sana kupita kiasi KWA WASIYEMJUA na majina wayaliliayo hayana uhusiano na Marehemu aliyesababisha msibani hapo kuna mnuso?Lakini,..

...JARIBU kumkasirikia akukasirishaye basi,...
... kwa kuwa ni uonevu kukuudhi akuudhi BOSI wako halafu HASIRA ZOTE unaziamishia nyumbani na kukasirikia watoto , BILA KUSAHAU na pia kumnyima unyumba MZAZI MWENZAKO.:-(

Jaribu kumkasirikia akukasirishaye basi ,...
.....sio iwe LIMZAZI lenzio limekuudhi nyumbani KWA KUKATAA KUFAFANUA, halafu unaleta fujo BAA - samahani- kwa watu wengine OFISINI ambao wala hata hawajui unawasiwasi MZAZI mwenzio ni mgawaji wa tendo la ndoa kwa wengine na labda MDUDU unao.:-(Swali:
 • Unadhani ni kila wakati unauhakika ni nini kinachokukasirisha?
 • Kwani utanibishia nikidai hasira zina utamu wake wewe?
 • Unafikiri kwa TANZANIA haiwezi kuwa ni fasheni tu kuikasirikia CCM ikiwa bado inasemekana WATANZANIA wengi wasikikao wakiilalamikia CCM, ndio waipigiayo kura kwa siri?
 • Au ni kweli fasheni ya hasira siku hizi TANZANIA ni kuwakasirikia MAFISADI kabla mkasirikaji naye hajawa FISADI?

NIMEACHA wazo MKUU, na kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!


Hebu BB KING na Tracy Chapman warudie- The thrill is goneAu tu ngojea Sade azungumzie tu - King of Sorrow

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 9:35 pm  

Mkuu hiyo King of Sorrow hunikosha sana.
Niseme uwe na wakati mzuri wakati wa siku yako ya kuzaliwa hapo kesho.

Yasinta Ngonyani 11:55 pm  

nashukuru sihitaji kumwona daktari kwani kwa mimi ni rahisi sana kukasirika:-)

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 11:28 am  

mh! si mchezo!

Sina la kuongeza isipokuwa kukukaribisha ugimbi kidogo usokomezee hisia hata kama si za kukasirika :-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 11:04 am  

pumbavu!!!!!!!!!!!!!!!

samahani, habari hii imenikasirisha sana! lione vile

chib 6:42 pm  

@ Kamala !!!!!!

Mtakatifu.... ati wasemaje? Hasira ina utamu wake!!!!

Simon Kitururu 8:10 am  

@Papa Fadhy: King of sorrow inakuna mkuu.:-(
@Da Yasinta: Yani unabahati wewe!:-(

@Kadinali Ng'wanambiti:Asante kwa ushauri. Nami nahisi nahitaji ugimbi kiduchu!:-(

@Komandoo Kamala:Duh!:-(

@Mkuu CHIB:Hasira inautamu wake Mkuu! Ukitaka kukasirika halafu ukafanikiwa kukasirikia kitu bnge la faraja .Noma kweli kuishi maisha yako bila kufanikiwa kukasirikia kitu kitu kisaidiacho sana kujihakikishia kunavisivyo kasirikiwa. Halafu Mkuu kama ingewezekana hata kunyimwa kununa baadhi ya misuli ya uso ingekuwa na dhambi ya uvivu.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP