Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

...ijifichapo AJENDA ya SIRI!

>> Thursday, January 07, 2010

[Tahadhari mwana tafsida: Tararila baadhi ya maeneo kitumizi la neno na kauli inapitiliza!:-(]


Mambo yangekuwa rahisi sana DUNIANI kama kila kitu kingekuwa tu kama CHOO kwa kuwa hata choo kiwe kisafi vipi hakuna siri kuwa kila mtu anajua kinaficha nini kunako SHIMO .Swali:
 • SI inajulikana kwa kila mtu kuwa mwili wa choo, tumboni unanini?


Kwa bahati mbaya hata choo bado hakirahisishi sana MAMBO kwa kuwa ungejua choo kinashuhudia nini wafanyacho huko UWASHUHUDIAO waendao chooni ,...

...waweza kusikitishwa kwa kugundua kuwa ni choo pekee ndio chenye ushahidi kuwa ASKOFU au tu Shekhe umuheshimuye chooni ndiko avutiako UNGA a.k.a mihadharati wakati umuonapo akienda MSALANI na wala sio zile haja namba MOJA au ile nzito ya namba MBILI.:-(

Tukiachana na hilo na kurudi katika ijifichapo AJENDA YA SIRI......kwa MWENYE TABASAMU,....

... ajenda ya SIRI inaweza ikawa iko kwenye TABASAMU na wakati unafikiri tabasamu linashughulikia KUKUPA ukarimu,....

.... kwa CHUNA BUZI tabasamu linaweza likawa lina maana JIINGIZE mtegoni MWANAHARAMU WEYE nikufilisi , kwana lione vile MENO kama NGIRI.

...kwa BOSI tabasamu linaweza kumaanisha mie sikupendi ILA ukinitaka ntakubali na kama unataka kujua WAKUTETAO hapa ofisini wewe NIULIZE tu mie , mwenzio na tete ulaji wangu tu hapa ofisini.NA,...
...ajenda za siri ya MTAKA ELIMU kwa wengi wala sio KUELIMIKA.:-(

......kwa Profesa MWINGINE elimu imetokea tu kwa kuwa TOKEA ALAZIMISHWE NA WAZAZI KWENDA SHULE UTOTONI ajuacho zaidi ni kujisomea na AJISIKIAVYO wakati akifanya MTIHANI ndio kulikomfanya hana hamu na NGONO kwa kuwa hakuna utamu MTAMU kama wakati anakokotoa MASWALA ili kutafuta JIBU na akipata jibu ukiusikiliza KWA MAKINI ubongo wake sauti uwezayo KUISIKIA unaweza kukumbushwa sauti uzisikiazo katika filamu za kikubwa a.k.a porno wakati unaziangalia kwa siri watu wasigundue kuwa ni wewe uliosababishaye neno SINEMA za NGONO kwenye search za google ni maarufu.


....kwa KIBOSILE na pamoja na watu LUKUKI WENGINE WENGI UWAFAHAMUO elimu ilikuwa ni CHAMBO TU cha kupata KAZI yoyote tu hasa baada ya kustukia VYETI na WAAJIRI ni kama INZI na MZOGA , na baada ya kupata kazi ni asilimia moja tu ya yaliyompeleka shule anayakumbuka na kuyatumia tena KIELIMU na hapa sigusii hata ile elimu ya kuvaa kondomu kabla ya kutumbuizwa na malaya.

Swali:
 • Unakumbuka vitabu vyako vya shule viko wapi mkuu?


NA,...
...ajenda za siri ziko mpaka kwenye DINI.

....kwa ASKOFU inaweza kuwa kisa kikubwa cha kujiingiza kwenye DINI ilikuwa ni kwa sababu tokea mtoto alikuwa anazimia magauni tu ya MAPADRE bila kusahau mapochoocho kutoka VATIKANI na hali halisi ya kwamba katika SEHEMU ZA dini ndio sehemu pekee unaweza kutoa SHOO inayoboa ila watazamaji wa shoo hawaondoki kama kwenye shoo nyingine kama za MDUMANGE au tu kwasakwasa zikiboa.

....na kwa Muimba kwaya dini inamsaidia sana kupata mademu wa KILOKOLE kanisani ambacho kwa kisiri ndio kimpelekacho kanisani .


Swali:
 • Si unakumbuka DINI kwa shekhe na Mchungaji ni kazi?
 • Kwani ulifikiri kazi ya dini ni kupeleka tu watu mbinguni ?
 • Unafikiri ni wangapi wakiwa kanisani au msikitini hawasikilizi kinachosemwa ila ni muhimu kwao kuonekana huko?NA,
...kuna ajenda za siri za KUJIPENDEKEZA pia.

....kwa ajipendekezaye KWAKO moja ya siri usiyoijua INAWEZAKUWA ni kweli ANATAKA kikweli kuwa rafiki yako wa KWELI.:-(

...... kwa ujipendekezaye kwake ajenda ya SIRI KWAKO inaweza ikawa ni kutimiza busara idaiyo mjue vizuri ADUI YAKO kwa kuwa KARIBU YAKE kama unataka kuepuka KUCHEMKA katika swala zima la kukabiliana na UADUI WAKE au tu ile BUSARA idaiyo tu kuwa ADUI muweke karibu zaidi hata kuliko rafiki kwa kuwa anapigika ROBA kirahisi, au tu unaweza ukamrukia kichwa , kumkata ngwala AU TU KUMTEMEA BONGE LA KOOZI akiwa karibu.:-(Na ,...
...kwa MMBEYA,..

....mara karibu zote ajenda ya SIRI katika MUONGEA UMMBEYA ni kutafuta habari zaidi zimuhusuzo mlengwa katika UDAKU a.k.a UMBEYA na chakusikitisha baada ya kupata UMBEYA mara karibu zote kunakuwa hakuna MANUFAA yoyote kwa MMBEYA.:-(

Swali:

 • Hivi ni kwanini hudhaniwa MMBEYA huwa afaidiki na UMBEYA?

 • Hivi neno MMBEYA ni kiswahili fasaha au huwa linaandikwa MBEYA kama mkoa wa MBEYA kwa kiswahili?
 • Heloooo MBEYA umejaribu kuuliza tu utakacho kujua CHA UDAKU bila kutunga kwanza kastori kakimbeya ili upate kujua fulani matako yake MUUMUKO WAKE ni wa bandia?
NAKATIZA wazo,....
...
na kwa hili la kuamua KUKATIZIA WAZO HAPA lina ajenda za siri, moja wapo ikiwa ni kutaka tu ufikirie MWENYEWE ajenda zako za siri leo hii kwa uliye mnunia, mchekea au tu kumkarimu lunch zilikuwa ni nini na je zimezaa matunda au utalazimika uzibadilishie mkao kwa kuwa kwa mkao huu kimdako wa mchungulio chupi haionekani?Swali zaidi katokori:

 • MHESHIMIWA unadhani hakuna ajenda za siri ambazo huzifikirii tu za karibu kila ufanyalo?
 • Si unajua ajenda yako ya siri ifichwayo ndani ya umchekeavyo FULANI kwa nia ya kumuambia unampenda HUYO FULANI , kwa kuwa HUYO FULANI ni maarufu na watu kibao wanamchekea hovyo hudhani usingefanikisha DHUMUNI HILOHILO la yeye kukustukia KWANZA kabla HUJAMUINGIZA MKENGE kirahisi kwa kumgeuzia kibano ukawa ni weye tu UMNUNIAYE kila akija KAZINI/pale umtegeapo BILA SABABU kwa BONGE LA MNUNO mpaka ajiulize wewe unatofauti gani ya ladha?

 • Kwani hujui kuwa ajenda za SIRI za baadhi ya Blogu ni KUJISHEBEDUA?


NI WAZO tu hili MAMA Kisebengo na USITISHIKE nimeliacha MHESHIMIWA!


Hebu ASWAD warudishe kitu -

Au tu ASWAD walete na -SHINE

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:44 pm  

DuH! darasa la leo mpaka naogopa kwenda chooni leo:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 8:32 am  

@yasinta usiogope, chooni kuna vitukama vilivyoma tumboni mwako..... samahani kama nakutukana!

kidogo tu nisomee uchungaji kwa kuzimia mavazi yao na jinsi waibavyo liturgia na kunyenyekewa na wanafiki kila wapitako

Simon Kitururu 12:25 pm  

@Da Yasinta +Komandoo Kamala: :-)

Simon Kitururu 12:25 pm  

@Da Yasinta +Komandoo Kamala: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP