Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kabla ya MUDA WAKO wa kueleweka KUFIKA, labda AKILI ZAKO na UFIKIRIACHO ni ukichaa kwa WENGINE!:-(

>> Saturday, January 30, 2010

Kuna watu mawazo yao yako mbele ya MUDA,....
..... na sasa hivi hawaeleweki ni nini WAZUNGUMZIACHO.Swali:
 • Au?

 • Unauhakika MAWAZO YA NYERERE ya siasa ya ujamaa na kujitegemea hayatakuwa ni MAWAZO na siasa inayotekelezeka mwaka 3000?

Na walio KIMAWAZO mbele ya MUDA,....
.......jamii inaweza kuwahukumu sasa hivi KAMA wafikiriacho wakikigeuza kuwa ndio WAKIZUNGUMZIACHO.

Swali:
 • AU?

Na ni mambo mengi katika huu muda,....
...... hayaeleweki ukiyachagua kuwa ndio UFIKIRIACHO,.....

.....na LABDA nikuanzia;

 • DINI,
 • NDOA,
 • SIASA,
 • WOGA WAKO,
 • ni nini LAANA,

.... au TU ni mpaka NI NINI ni aina ya gwaguro au chupi za wajanja,...

.... NA unayaona YANALETA MAANA kwa kuwa TU UNAFUATA MKUMBO WA watu wengi UWAHESHIMUO, utakao kuwa kama wao,NDUGU, au tu WALE TU udhaniao wameukata au tu wanaelimu kwa kuwa unajua waliposomea .:-(

Swali:
 • Au?
 • Unakumbuka UKWELI wa jambo hauathiriwi na IDADI ya watu na labda ni kweli KWELI ya kitu mara kedekede waijuao ni wachache?

 • Unauhakika na sababu za ujanja au tu mambo tu ya kileo kuleta maana kwa BINADAMU leo?

 • Unauhakika mambo ya kileo ya mpaka ya JUHUDI ZA WAJANJA kumvalisha mpenzi pete wakioa YANALETA MAANA wakati inajulikana pete haizuii mpenzi kuonjwa au kuonja LAWALAWA NYAMA MTAANI ingawa anakitumbua nyumbani?


 • Unauhakika wakati wa TANZANIA kupata uhuru haukuwa ni muda wa KAMBONA kuwa RAIS halafu wakati wa Rais MKAPA ndio ungekuwa wakati wa NYERERE?


Tukiachana na hilo,....
... naamini hata kisanaa TANZANIA ,...
... itafikia muda FULANI ndio ITAKUWA UJANJA kwa watu kustukia ni kwanini MORIS NYUNYUSA na ngoma ZAKE au tu Dr ZAWOSE ni mahiri kwa kuwa sasa hivi hawaeleweki kwa kuwa wafanyacho sio BONGO FLEVA.:


Tukiachana na hilo,....
Swali:
 • Si unakumbuka wengi wape kama tu zilivyokuwa demokrasia tuzisifiazo moja ya matunda YAKE ni kupotea kwa wengi hasa kwa kuwa NI KWELI lifuatwalo na wengi haina maana ndio usahihi wa hilo jambo?

 • Unauhakika IKIWA kura za wengi TANZANIA ni za wasio elewa hata ni nini wanakipigia kura maana yake hao wengi ndio wapatiao jibu la matatizo ya TANZANIA?

 • Hivi wewe MKUU unaeleweka?

 • Hivi Mheshimiwa wewe HUMJUI HATA MTU MMOJA ambaye ni wale wafuatao mkumbo wa jambo kwa kuwa ndilo lielewekalo AU TU LIFUATWALO na wengi?

 • Si unajua moja ya siri la urahisi wa kitu kuwa na wafuasi wengi ni MDHANIO wa urahisi wake kueleweka wakati tunajua MATATUZI ya mengi si rahisi?
 • Si unajua wazo lako lisilo wezekana leo labda tu muda wake haujafika?
 • Si wazo lihangaikiwalo NA MAARUFU leo linaweza kuwa ni wazo lililopitwa na wakati?
Naacha na ni wazo tu hili MHESHIMIWA !:-(


HEBU tu Fela andelee kwa kuleta another underground SPIRITUAL GAME kwa kitu - Beasts of no Nation.Au tu FELA KUTI aendeleze SPIRITUAL GAME kwa hiyo hiyo- Beasts of no NATIONAu tu Phil Collins atulize kwa NENO kueleweka kirahisi kwa - Another day in Paradise

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:48 am  

mada menishinda

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:48 am  
This comment has been removed by the author.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP