Kama ampendeaye mtu TABIA bado naye atahitaji SEHEMU ZA SIRI ZA MTU ili penzi litimie!:-(
>> Sunday, January 31, 2010
[Tahadhari: Wazo limepinda na LINAWEZA kukukwaza kama mtoto au tu kama weye ni Mzee wa kukwazika!:-(]
Kuna wagundulikao kuwa pamoja na kudai wamempendea mtu SURA au tu nyonyo,...
....bado walengacho na wahitajicho kutoka kwa mwenye HIYO sura nzuri wala sio HIYO sura na labda ni zake tu SEHEMU zenye NYETI.:-(Na kwahiyo mara nyingine kumbuka kama hutachukulia hili kama ONYO,...
....kuwa pamoja na kwamba wako WASIFIAO HARUFU YA CHAKULA ambao hudai wamevutiwa na harufu ya chakula katika PENZI LAO LA HICHO CHAKULA,....
... lakini KUNA UWEZEKANO MKUBWA mapenzi YA harufu ya chakula kwa apendaye kula au MWENYE NJAA ni danganya toto kwa kuwa kwa yoyote mwenye njaa anajua kiliwacho katika chakula si HARUFU na afuataye harufu hata ya ubwabwa wa msibani ni KUGIDA MSOSI na sio KUSIKILIZIA HARUFU ndio SWALA NYETI.
Swali:
- AU?
- Unauhakika kikufanyacho umpende mtu sio CHAMBO tu chakukurahisishia kukabiliana na vipengele vyake huyo mtu ambavyo labda vinanuka na vinasura mbaya ambavyo ndio unavihitaji katika huyo MTU?
- Unafikiri harufu ya wali sio tu msaada KWAKO wakukuwezesha ule wali ingawa mahitaji yako yangetimizwa na MATOKE au ugali wa mhogo?
Ndio....
.... labda kuvutiwa kwako na SURA au tu shepu ya matako ya mtu,...
.... labda kuvutiwa kwako na SURA au tu shepu ya matako ya mtu,...
.... ambavyo UKIFIKIRIA labda katika huyo mtu hivyo ndivyo vipengele vyake ambavyo hutavitumia na huna mahitaji navyo,...
... NI DALILI ya udhaifu wa UZURI wa uvihitajivyo katika huyo mtu vikiwemo TABIA YAKE au tu sehemu zake uzihitajizo katika shughuli nzima ya KUUJAZA ULIMWENGU a.k.a kuzalishana hasa kama SEHEMU HIZO huzitumii kimaridhawa kama VYOMBO vya burudani.:-(Swali:
- Unauhakika ni nini hasa umpendeacho wako MPENZI?
- Unafikiri katika kila PENZI hakuna lako hitaji ambalo unalipata kwa huyo mpenzi ambalo halina uhusiano na kifanyacho MPENZI kwako anavutia?
- Unafikiri mapenzi hayana UBINAFSI na ni kweli unampenda tu MTU kwa roho yote bila ubinafsi kwa kuwa tu ANA ROHO NZURI na hakuna chochote binafsi upatacho KIFARAJA ?
Ndio,...
... kuna MAPENZI ya aina nyingi,....
.... kwa mfano yale ya NDUGU kwa NDUGU au tu MTU na MBUZI.Ndio,....
..... UKIFIKIRIA waweza kustukia hata MAPENZI ya mtu na MBUZI au KUKU aliyenona,....
... yawezekana ni DANGANYA TOTO hasa kama ASIFIWAVYO MBUZI na KUKU ni kimvutio WA MUONEKANO kama nia ya kuwafuga MBUZI au KUKU hao inalenga sana cha binadamu KITOWEO kuliko kupamba ya binadamu DUNIA.:-(
Swali:
- Unauhakika MAPENZI yako kwa NDUGU yako nayo kiyakupavyo faraja , KWAKO hayana UBINAFSI ?
- Wakati kuna adaie amempendea MTU mwanya AU MATEGE,-kama sio tako,- unafikiri MWANYA au MATEGE ya apendwaye unateleza kitu gani muhimu katika PENZI la hao wapendanao?
NAKATIZIA HAPA katika hili WAZO Mheshimiwa nikiamini unaelewa hili ni wazo tu na kulibishia RUKSA!:-(
Hebu twende tu tena Ivory Coast Meiway aendelee na -Voila String
Au tu MEIWAY aweke tu na-DJ Tassouman
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Simon kama hau-mind nina maagizo yako.
@Yasinta: Yawezekana si maagizo ya kuzinguka na kipengele muhimu ndani ya Mt. Simon :-( MPIRA wa KONA Huoooo!!! :-(
Nachizika na wazo hili! kwa kuwa yawezekana MTU kuona vilivyoITWA NYETI katika mtindo wa kuona kiungo kingine kama mguu wa BIA ama sauti ADAIYO kuwa ni taaamu!
Na nazinguka zaidi pale staili ya kutongoza inakuwaga NAKUPENDA sana badala ya NAOMBAKO HIKO KITU chako nijipoozee makali ya ashiki :-(
Na: hivi ni kweli kuwa wadaio kuwa HAWALI, HAWANYWI ama Wakinywa maji wanamwona kimwana/kijeba humaanisha kuwa ni KILE KIPENGELE wanachoki-mind zaidi? :-(
Samahani Boss!
@Da Yasinta: Ntakutafuta!
@Kadinali CHACHA Ng'wanambiti: DUH!
Mt. kaka Simon, ntashukuru sana ukifanya hivyo:-)
@Dada Yasinta: I promise ntafanya hivyo.
Post a Comment