Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kuangalia WAAMINIO MUNGU wahangaikavyo na ni nini ni MAPENZI ya MUNGU!:-(

>> Monday, February 01, 2010

Kuna waaminio kama ni MAPENZI YA MUNGU,...
.... hata ukwepe vipi utanasa tu na kwahiyo ukitongozwa na malaya UKAKATAA usijisifie sana kwa kuwa yote mpaka kukubalia mtu ni MIPANGO tu YA MUNGU.:-(


Moja ya UDHAIFU Mkubwa katika kutafsiri ni nini MAPENZI ya MUNGU,...
...... labda UKO katika imani ya MTU na AJUAYO MTU KUYAKABILI kama MTU kabla ya kuyakabili ambavyo KIFIKIRA anafarijika zaidi na KUSHINDWA SWALA KIBINADAMU kwa kuwa na jibu kuwa ni kwa sababu ni MAPENZI YA MUNGU.



Na labda kuna mengi BINADAMU humsingizia tu MUNGU,....
..... wakati ni maamuzi ya KIBINADAMU na yanafanyika na BINADAMU na wala sio MUNGU.

Swali:
  • Kwani ukiambiwa usitumie madawa ya kulevya kwa kuwa yanaweza kukufanya mtumwa wa madawa ya kulevya a.k.a TEJA ukatumia madawa ya kulevya na kweli kuwa TEJA hayo ni mapenzi yako au ya MUNGU?

  • Hivi kuna uwezekano ni mapenzi ya MUNGU Tanzania na Watanzania wengi masikini?


UDHAIFU wa uelewaji wa ni nini ni MAPENZI ya MUNGU,....
... waweza rahisisha uridhikaji wa MASIKINI kubakia masikini kwa kuamini kama ingekuwa sio mapenzi ya MUNGU , masikini angezaliwa katika familia TAJIRI na kuwa tajiri tu hata bila kumuamini huyo MUNGU.



UDHAIFU wa uelewaji wa ni nini ni MAPENZI YA MUNGU,...
.... pia waweza kumfanya kijeba asiogope MALAYA awajuao kwa UMALAYA NA MDUDU kwa kuwa ajali kazini kama zile za kupata UKIMWI , GONO au tu KISONONO , tukiachiliambali ile YAKUJIFIA TU KWA MALAYA zaweza tambulika tu kuwa ukinaswa, itakuwa tu ni MAPENZI YA MUNGU.:-(

Swali:

  • AU?
  • Unafikiri kuna aaminiye MUNGU amuelewaye MUNGU?

Kumbuka tu ,....
... kuna mambo ya kibinadamu mengi yaelewekayo sana tu KIBINADAMU ,....

..... kwa hiyo kama WEWE NI BINADAMU na unakula MAHARAGE na kupatwa na DHARURA ZIJULIKANAZO hupewa MOTISHA na kula maharage kama vile KUJAMBA ,...

...LABDA usitake kusingizia kuwa ni miujiza kwa kuwa inajulikana na BINADAMU mara zote aina ya KITENDO FULANI lazima izae MATOKEO ya KITENDO FULANI na kwahiyo kama umefanya kitendo cha kula maharage zaidi na sio MCHICHA matokeo yake ni aina tu fulani za USHUZI usiosababishwa na ulioukwepa MCHICHA.:-(

Swali:

  • AU?
  • Kwani unafikiri kufeli kwako MTIHANI wakati hujisomei ni MAPENZI YA MUNGU?
  • UNafikiri kama una maharage TU leo nyumbani MUNGU akipenda msosi hautakuwa MAHARAGE?
  • Lakini KAMA HUPENDI MAHARAGE lakini una maharage NYUMBANI, hujipalii makaa kwa kujitia majaribuni KUYAGIDA hayo MAHARAGE kwa MAPENZI YA KIBINADAMU TU na sio ya MUNGU?
  • Si unakumbuka DUNIANI kuna wasioamini MUNGU na kwa hilo automatikali hawaamini kuna SHETANI?
  • Hivi kunauwezekano ni mpaka uamini kuna MUNGU ndio ukimkosea MAPENZI YAKE ufanyayo ndio yanakuwa ya SHETANI?


SAMAHANI,...
....NI wazo tu hili MHESHIMIWA na nalikatizia hapa!:-(


Na ngojea twende Kameruni - MANU DIBANGO abadili hali ya hewa kwa kitu -Sax Medley & voices




Au tu MANU DIBANGO na wenzake walete na- Amio


6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 11:11 am  

Ati mungu naye ana mapenzi? :-(

na linapokuja swala la lawama waweza kuta mtu katukanwa na mkewe/mumewe nyumbani akahamishia hasira zake kwa sekretari wake ofisini :-(

ama kaudhiwa na bosi wake akaenda kumbonda mkewe ama watoto nyumbani :-(

Na haya ni mapenzi ya mungu? :-(

Yasinta Ngonyani 4:56 pm  

Au pia unakuta wawili wanaopendana lakini ni vigumu kuwa pamoja kwa sababu hizi na zii.:-

Pia marafiki wapendanao wamepoteza mawasiliano kwa muda mrefu:-(

Je na hayo ni mapenzi ya Mungu?

Upendo Daima

Simon Kitururu 5:00 pm  

@Kadinali Ng'wanambiti + Dada Yasinta: Yani Mmmh!

Yasinta Ngonyani 5:40 pm  

Mt. Kaka Simon una maanisha nini usemapo "Yaani Mmmh!"

Simon Kitururu 7:18 pm  

@Da Yasinta: Nimguno wakumaanisha nafikiria tu ``MAPENZI ya MUNGU´´ baada ya fikira hizo kuchokonolewa upya na mkao wa comments zenu.:-(

Yasinta Ngonyani 8:09 pm  

key! kakangu basi ngoja niache na nimeacha kikweli:-) Jamani jamani!!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP