Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MOJA ya sababu KWA KAWAIDA MFIKIRIA SANA UKE , hadharani anaweza kujulikana na KUWA MAARUFU kwa KUONGELEA SIASA tu!:-(

>> Sunday, February 28, 2010

MAZOEA yaweza kumzoesha MTU kuongelea SIASA wakati shida yake ihitajiyo kuongelewa  ILI IPATE VITENDO MSWANO ni ILE  ya UKE.:-(

NDIO,...
... tatizo moja la BINADAMU AWAZAYE ni kufikiria pia kama AWAZACHO chafaa kuongelewa HADHARANI.:-(

Swali:
  • Si  umestukia hilo  hata kwa kufikiria ni vingapi ulivyowaza leo ambavyo huna-KIBEZI cha kuviongelea hadharani ili MAMA Mkwe asikie?
  • Umeshafikiria ukweli wa UPOTOFU wa kwamba ukiwazacho NI SIRI na   watu hawajui ndicho UWAZACHO?




Katika MAWAZO ELFU  YA MTU ndani ya siku ,...
.....inawezekana kabisa  BINADAMU huongelea kitu kimoja tu HADHARANI!


Ila BINADAMU ni MUWAZAJI wa maelfu ndani ya siku ,...
..... na waweza kirahisi kusahau hilo kwa kuwa MTUZ  ni CHAGUZI wa cha KUONGELEA hadharani.:-(




Swali:
  • Si unakumbuka hilo?



MAZOEA yanaweza yakawa yanasaidia  ni nini UNAONGELEA HADHARANI  zaidi,....
... wakati kikuwashacho KUNAKO NANIHII  zaidizaidi ufanyacho zaidi ni KUKIFIKIRIA TU.:-(


MAZOEA yanaweza yakawa ndiyo yasababishayo kirahisi MTU anaongelea SIASA zilizo maarufu  HADHARANI   zaidi,...
.....wakati tatizo lake ni UKE  na UMASIKINI usioguswa na SIASA  ZISIZOMAARUFU kuongelewa HADHARANI ambazo KIHESHIMIWA hufikiriwa TU.:-(



Swali:
  • Katika ulivyoviwaza leo si unakumbuka ni kipi UMEAMUA hautaweza kukiongelea HADHARANI ?
  • Umeshawahi kufikiria vizuri  ni nini kinachofanya baadhi ya uongeleavyo CHUMBANI hutaki wageni wajue huwa unavigunia,  SEBULENI?

Ndio,...
....kiongelewacho hadharani  labda wala si CHEPESI kuongelewa ki hivyo na MUONGEAJI ,...

......na kiwezeshacho KUKUTIA NGUVU ya KUKIONGELEA HADHARANI labda ni  ULIVYOJIFUNZA TU kuamini  HICHO  kinakubalika kuongelewa  HADHARANI ,....

....hasa kwa kuwa wote TWAFUNZWA KIHESHIMA hata bila kufikiria sana   kujua na kuamini  MAISHANI ni  VIPI vichache vifikiriwavyo ambavyo   ni sahihi KUONGELEWA HADHARANI.:-(

Na chakusikitisha zaidi  ni kwamba,...
....WATU wengi  sababu zao za kukalia KIMYA SHUGHULI ni za KUFIKIRIKA tu kwa kuwa kihalihalisi WAJARIBUCHO kuficha  kwa kutokiongelea kama kile cha kuwa wakati BADO WADOGO waliwahi kulamba KAMASI ,....

..... labda wamfichaye bado AKIWA NA KAMASI na  akihisi hakuna watu badala ya KUJIFUTIA kwenye KIJAMBA KOTI, Suruali  au KOCHI kamasi , kirahisi hulilamba KAMASI katika staili ya kulimeza tu kisa anaamini hakuna watu wampigao chabo HADHARANI :-(.




Swali:
  • Unafikiri kwa uhakika HII ni porojo tu?


Ndio,...
.... mpaka katika vitu MAMILIONI VIFIKIRIWAVYO  viwezwavyo HATA  kuanzishiwa BLOGU kuna waliochagua kuongelea FASHENI TU  hadharani.

Ndio,....
.... katika vitu MAMILIONI VIFIKIRIWAVYO viwezavyo kuanzishiwa BLOGU,  Mtakatifu Simon Kitururu huchagua kuongelea CHUPI na UJINGA  TU hadharani.:-(


Swali:

  • Unauhakika wewe unaongelea nini kirahisi HADHARANI?
  • Si unakumbuka  tukiachana na vile  BINADAMU afikiriavyo unavyoweza kumfanya kirahisi AVIONGELEE, -SI WAJUA BINADAMU MWENYE AIBU  ukimuandaa afikiriavyo waweza kumfanya kirahisi aonyeshe chupi hadharani kisa umemfunza kuita kificha nyeti `` BIKINI´´?

  • Si unajua katika vitu MILIONI alivyowahi kufikiria MTU huwa  kunasababu tu ni YESU Mtu FULANI apendacho kuongelea hadharani na sio ukweli kuwa kimsumbuacho  hata kusikiliza mahubiri vizuri ni NYEGE mshindo?



Ndio,....
.... kunasababu kuna  VITU milioni  ufikiriavyo wakati katika HIVYO ni KIMOJA ambacho uko huru kukizungumzia HADHARANI.:-(


Na kikubwa ni kwamba  UMEJIFUNZA tu ,...
.... ni NINI huwa KINAONGELEWA HADHARANI kitu ambacho ndicho KIKO NYUMA  ya  uchaguzi WAKO wa nini unakiongelea HADHARANI.


Na baada ya kujifunza ni nini katika kundi la wadaku ni RUKSA KUKIONGELEA HADHARANI kama unataka ufikiriwe UNAJIHESHIMU ,...

... kinachofuata katika uongeleayo kirahisi HADHARANI  ni MAZOEA tu ya ni nini unajisikia huru kurudia kuongelea  kitu ambacho husababisha aliyezoea kuongelea UDAKU kirahisi  ATARUDIA kuongelea  udaku  tu  HADHARANI.:-(


Na  haki ya MAMA KISEBENGO TENA !- ukishazoea kitu,....

..... si ajabu katika MATUSI yote  DUNIANI weye kirahisi UKIPANDISHA nyege ya KUTUSI  utatukania MAMA kama matusi ya MAMA ndicho ambacho  ULICHOJIZOESHA kutukana HADHARANI.:-(


Na ukishazoea kitu,....
......  katika  MAELFU YA UFIKIRIAYO  waweza kujikuta ukumbukayo kuyaongelea kwa kuwa ulichozoea kuongelea ni SIASA ,....

.....utakaCHOkumbuka kuongelea ni SIASA TU  kwa HATA wapenda FASHENI wakati kikusumbuacho wakati huo ni JINSI YA KUPATA UKE hadharani.:-(


Swali:
  • Si unakumbuka unaruhusiwa kunibishia?

Ndio,...
.... mengi  UYAFIKIRIAYO hujawahi kuyaongelea na sababu kubwa HUYAONGELEI  UYAFIKIRIAYO  MENGI ni za kufikirika tu NA  ni ALINACHA tu  ,...

.....na kwa hilo SAMAHANI kwa kukukumbusha  MHESHIMIWA!


NAACHIA HAPA WAZO Mheshimiwa!:-(

Hebu Naughty by NATURE katika kubadili warudie.- Jamboree



Ice Cube arudie - Today Was A Good Day[JIHADHARI: :LUGHA fulanikatika wimbo KAMA wewe ni msikiliza NDOMBOLO KATIKA NENO INASEMA NINI ... ndude  inatumia lugha ya namna gani kiheshima inaweza kumkwaza MLOKOLE.:-(]




Au tu Snoop Dogg abadili zaidi kwa- Pump Pump[Tahadhari: KWA mheshimiwa asikilizaye MANENO  anaweza kusikia lugha chafu!:-(






Nipo,....:-(

Photobucket




Photobucket



Photobucket





Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket


Photobucket


Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:55 pm  

Ahsante kwa taswira hizo nzuru:-) öl är gott:-)

Simon Kitururu 3:39 pm  

@Da Yasinta: Asante sana! Na asante nyingine kwa kutonitenga !

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP