Kama kulikuwa na MSWADA wa MWAKA jana katika SEKTA ya UCHAWI Tanzania!
>> Tuesday, February 02, 2010
[Tahadhari: Wazo hili limepinda!]
Moja sekta isemekanayo ILIFANYA VIZURI sana mwaka jana na ambayo BADO NI yenye mafanikio sana Tanzania ,...
.... ni ile sekta ya UCHAWI ambayo inasemekana ingawa huendeshwa kama N.G.O[Non-governmental organization] kwa ubora wa ufanisi WAKE matunda yake yanaonekana sana serikalini , makazini , mpaka tu mtaani kwa watu BINAFSI.
Imani za uchawi yasemekana kuchangia sana tu TANZANIA na UTANZANIA,...
.. hasa kwa kuboresha baadhi ya watu kuogopa GIZA, baadhi kusali sana usiku, kuogopa BUNDI, pamoja na kuwa na dhahabu na alimasi baadhi ya watu kugeuza NDUGU ZETU MAALIBINO kuwa maliasili, au tu kwa baadhi KUJIAMINI SANA TU kupita kiasi kutokanako na kujiamini WAMEAGA KWAO au tu hirizi katika fundo la KIFICHA NYETI a.k.a chupi au tu chale kadhaa KUWAAMINISHA zinawasaidia na HATA wakitaka kura au KULA , watu wengine NI lazima wawapigie KURA au wawape KULA ingawa wanakiri kutokuwapenda kwa karibu mambo yao yote na sio tu yale YAO ya UBINAFSi.:-(
Swali:
- Kwani hushangai uchawi usemekanao unafanyika kisiri bila kushuhudiwa Tanzania utishavyo watu kuliko Polisi na bunduki zao waonekanao MTAANI wawezavyo kutisha majambazi Tanzania?
Miye binafsi NAPINGA mambo ya UCHAWI,...
.... ila kwa kuwa nashuhudia jinsi jamii ya WATANZANIA iaminivyo USHIRIKINA,...
.... na wasiwasi labda ni UNAFIKI katika kujadili IMANI ZA WATU , wengi hujadili tu DINI kama vile UKRISTO na UISLAMU na kusahau kuwa MOJA YA imani ambayo naamini inamafanikio makubwa sana ambayo waifuatao wako kimya mpaka unaweza kutowastukia TANZANIA ni ya USHIRIKINA.:-(
NA labda hatusikii wachawi wakitutonya shughuli zao UKIZINGATI hadi leo hatuna hata MCHAWI mmoja ambaye kaanzisha BLOGU ya UCHAWI TANZANIA wakati naamini kati ya hawahawa MA anonymous HUMU MTANDAONI kuna MAGWIJI WA UCHAWI ambao wangeweza tu KUBLOGU KAMA MA-anonymous angalau kututonya ni nini hasa wakilengacho katika MAALIBINO au katika maswala madogomadogo kama tu ya kutujibu swala la kama kuna FIRST CLASS katika usafiri wa ungo kabla ya kuhitimisha na ni wapi pa kwenda kuwanga kwa WANASIASA wetu kabla ya UCHAGUZI ujao.:-(
Na labda hatusikii wachawi kwa kuwa wanaogopa kuwa WAAMINICHO hatukubaliani nacho,....
... na hasa tukikumbuka kuwa hata MTU wakawaida IMANI ZAKE zikiwa zinashambuliwa kwa kujihami anaweza kuingia mtini.
Na wakati IMANI au MTAZAMO wa MTU ndio UNAOSHAMBULIWA ,.....
...... mpenda CHAI na kiporo cha makande asubuhi naye anaweza kudai anahusudu CHAI ya maziwa na MKATE vipinganavyo na imani yake kama tu MUOGOPA kukandia KITIMOTO mbele ya wala nguruwe asio nania yakuanzisha nao MALUMBANO.:-(Swali:
- AU?
- Unafikiri kimtazamo na KIIMANI Uchawi ungekuwa ni BAB KUBWA tusingekuwa na maselebriti wapaanaungo ambao umaarufu wao ni Kupaa na ungo Tanzania?
Ila wakati kila mtu uliyekuwa naye NI ambaye KIIMANI na MTAZAMO anakubaliana nawe,....
... uharisho wako unaweza kufumbiwa macho na watu au ANGALAU wakajaribu kuurembesha katika kuukabili kwa KUJARIBU kuuangalia kama ni ya kawaida tu MAVI.:-(
Na siri ya kuendekeza UAMINICHO kizidi kupotea nawe,...
..... MOJA WAPO ni kujichomeka KATIKA KUNDI LIAMINILO KAMA WEWE au tu kama unataka MFANO MZURI , ni vizuri kuiga staili zitumikazo na dini za kuhakikisha kuwa unakwenda KANISA la aina MOJA au MSIKITI MMOJA na wengine waaminio kama wewe ili kukusaidia uzidi KUAMINI unavyoamini kwa msaada wa WOTE MFANANAO IMANI waabuduo HIVYO nawe.
Swali:
- AU?
- Hujastukia kuwa kama ni MTAZAMO wako au IMANI YAKO ndio inashambuliwa ujisikiavyo uhaueni kujua hauko peke yako uaminiye hivyo kwa kustukia kuna mtu mwingine umestukia naye anaamini kama wewe?
Na wakati MTAZAMO wako NDIO unaoshambuliwa,...
.... kama unapapara unaweza KUUMIA ROHO na kwa papara ukatetea hata ambayo HARUFU tu INATOSHA KUCHEFUA na KUHITIMISHA SWALA kwa kujipotezea muda kunyambulisha kuwa ni choo laini na WALA sio uharisho ingawa KWA WENGINE WOTE ni harufu tu ILITOSHA KUCHEFUA na katika HILO wala haiina msaada kunyambulisha ni aina gani ya MAVI.:-(
Swali:
- Kwani wakati ni mtazamo wako unashambuliwa WEYE hukai mkao wa kuutetea hata kama huna cha kutetea?
- Hivi wakati uaminicho kinashambuliwa si ndio upatapo nafasi ya kukifikiria vizuri na kukuza imani yako?
- Hivi kidemokrasia na kama wewe uaminicho ni UCHAWI au tu MCHAWI,- hufikirii kuanzisha chama cha utetezi wa WACHAWI na UCHAWI Tanzania kwa jinsi uaminicho na utendacho kinavyoshambuliwa waziwazi halafu tena na isemekanao ni WANAFIKI?:-(
- Unafikiri ni wachawi wangapi ni washikaji zako na huwajui tu kwa kuwa BADO hawana chama kama CCM au CHADEMA kiwasaidiacho kuwapigania haki ya kuwanga mchana bila kunyanyaswa?
SAMAHANI nimepitiliza,.....
...tukirudi katika HOJA,.....
... pamoja na kuuawa MAALIBINO kulivyoitangaza TANZANIA mwaka jana ,...
...TUKUMBUKE ni miaka nenda rudi maswala ya USHIRIKINA BONGO ni mambo ambayo yanaathiri sana TANZANIA na UTANZANIA.:-(
...TUKUMBUKE ni miaka nenda rudi maswala ya USHIRIKINA BONGO ni mambo ambayo yanaathiri sana TANZANIA na UTANZANIA.:-(
Na LABDA kama TANZANIA maswala mengine yangekuwa yanaenda kama ISEMEKANAVYO yaendavyo ya USHIRIKINA ,...
... NAAMINI kweli KIKWELI Bongo mambo yake yangekuwa TAMBARARE.:-(
Swali:
- UNABISHA?
- Kama kulikuwa na MSWADA wa MWAKA jana katika SEKTA ya UCHAWI Tanzania, hudhani kiutekelezaji angalau wa kuitangaza Tanzania kwa ushirikina ulifanikiwa ?
NI wazo tu hili MKUU ,...
...ingawa labda kama weye ni MCHAWI ingekuwa bomba kweli ukianzisha BLOGU kutujuza maswala YA mikakati mipya ya MWAKA HUU katika sekta NZIMA ya UCHAWI TANZANIA.:-(
NIMEACHA!...ingawa labda kama weye ni MCHAWI ingekuwa bomba kweli ukianzisha BLOGU kutujuza maswala YA mikakati mipya ya MWAKA HUU katika sekta NZIMA ya UCHAWI TANZANIA.:-(
Au hebu BUNNY WAILER aingie deep kimtazamo fulani kwa -RISE and SHINE
Au tu BUNNY WAILER aje live na kitu ileile banangenge- RISE & SHINE
9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nina wasiwasi kama naamini UCHAWI:-(
@Da Yasinta: Kutoamini ni Ruksa lakini pia kutoamini uwepo wa kitu hauondoi uwezekano wakuwepo kitu.:-(
Na kwa jinsi Maalibino wanavyouawa Tanzania, nukuu za biblia na korani kuhusu uchawi, au tu wingi wa waganga wadaio kuganga karibu katika kila mji Tanzania kwaweza kutumika na mtu kama ushahidi UCHAWI upo.:-(
Mt. Simon ahsante kwa kunipa ruksa ya kuamini hakuna uchawi. Nimesema hivi kwasababu kwa mtazamo wangu naona ni kwamba hao watu wajiitao wachawi wamekosa elimu. Huwezi kumuua mtu kwa kufikiri kwa unaweza kuwa tajiri. Labda tuseme kuwa wao wanaoamini hili wanaimani finyu
Pia ni ruksa kwa kwa wanaoamini kuna wachawi.
@Da Yasinta: Ni kweli usemacho!
Na kwa mtazamo mwingine hii ni MITAZAMO tu hasa tukikumbuka duniani wapo pia wenye mtazamo kuwa kuna MUNGU.
Je wewe una mtazamo gani kuhusu Mungu?
@Dada Yasinta:
Nivigumu kwangu kuwa na mtazamo wa uhakika kwa kuwa bado nahangaikia kuelewa. Na nawasiwasi labda kumuelewa Mungu ni jambo liendelealo kila siku kwa hiyo ni vigumu kuwa na Mtazamo wa aina moja kwa kuwa kuna siku Mungu ni Pendo na kuna siku Mungu huwa ni Tisha toto katika maisha yangu.:-(
Wewe unamuelewa Mungu?
Kaka Simon nimekuelewa, kwa mie ni hivi:- Kwanza nilikuwa namwelewa sana Mungu.Lakini siku hizi huwa najiuliza kama kweli Mungu ananisikiliza maombi yangu na kweli ananipenda?:-(
@Yasinta na Simon: nina wasiwasi nanyi nyote kama si WACHAWI :-(
kwa kuwa kwa kutoamini kwenu tayari mshakuwa wachawi :-(
ama mna uhakika, kukaa katika kiti kirefu kupata ugimbi na kushabikia saaa chai bila sukari si uchawi?
ama uchawi ni kufanya jambo ambalo laweza kuwa la ajabu ama lisowezekana kwa wengine?
unadhani Mungu si mchawi? (kwa mujibu wa BIBLIA, Mungu akasema na uwepo mwanga, ukawapo, nk) na kwa kuamini kwako uwepo wa mungu hata kama hampendi wala kumwelewa Yasinta hudhani kuwa unashiriki uchawi wake na hIVO nawe NI MCHAWI TU? :-(
NA kwa kutomwelewa mungu na kudhani kuwa hakupendi ama hampendi nduguyo, si inawezekana ikawa pia ni UCHAWI? :-(
@Kadinali CHACHA: labda tafsiri ya ``Uchawi ni nini?´´ na `` Mungu ni nini?´´ zisipofanana hakuna uwezekano wakupata jibu moja.
Si unakumbuka kwa wengine Mungu wao ni Ng'ombe?
Na si kwa wengine tekinolojia za aina fulani ni uchawi wa Wazungu?
Tafsiri ya kitu NI kitu cha ajabu sana!
Post a Comment