Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Misingi na siri ya UJANJA WA MTU ni dhaifu ndio maana DUNIANI kuna MJANJA mpaka kwa kutovaa chupi PIA!:-(

>> Wednesday, February 10, 2010




[Tahadhari: Wazo hili linamwendo wa kusuasua kimtiririko!:-(]





Kitu kidogo tofauti chaweza tafsiri kwa watu MTU ni MJANJA ,...
.... na kwa wacheza SINDIMBA uchi chaweza kuwa ni kitu kidogo kama TU ni nani ULINGO kauvalia chupi!



Na kwa wengi siri ya wamstukiavyo MJANJA,....
.... ni utofauti wake tu na wengine katika MIKAKATI hata kama mikakati yake yenyewe  ifanikishacho ni kwenye mitumba ya suruali kudaka zilizojichanganya HUMO  zilizotumika chupi.:-(


Misingi ya tafsiri ya UJANJA umtofautishao katika kundi aliye MJANJA,...
... yaweza kuwa ni UJINGA wa TAFSIRI ya ni nini UJANJA ndio maana utekelezaji wa JAMBO LILELILE LA KIJINGA hata kama laumiza HATA BILA KUJUA WENGINE kwa kukwepa miundo mbinu ambayo watu wanaitumia kutekeleza jambo LILELILE ,...
....kuna watakao APIA ni UJANJA hata kama shughuli yenyewe ni kudaka mteja kwa kumkalia uchi na MODO MJANJA shughuli hiyo kaivulia chupi.:-(

Swali:

  • Si unajua siri ya misingi ya kimfanyacho MJANJA aonekane ni MJANJA KWAKO  labda ni kasumba zako tu?


NA kama BINADAMU angekuwa kwa kawaida anaishi MILELE,....

.... HAKI YA NANI TENA,...

....labda WAJANJA wangekuwa ni wale waishio maisha mafupi KWA KUJIUA na moja ya mjanja AMBAYE angesifiwa sana ni yule KATIKA STAILI YA KUFA  alijinyonga:-(

Samahani kidogo:

  • Lakini si kuna wajanja tuliowapa USHUJAA  kwa KUWA walijiua VITANI ili wasidakwe na adui na kudhalilishwa ?
  • Lakini kwa tafsiri fulani si MAISHA ni vita?


....kwa hiyo LABDA  ni UJANJA kukwepa kudhalilika,....
..... ingawa LABDA bado kama wote WATAKUWA WANAKWEPA kudhalilika ,....

.....MJANJA  MPYA ,......

....atapatikana  KATIKA  WADHALILIKAO  ambaye angalau kabla hajafa anaweza akawa anajulikana KATIKA WALIOFARIKI  na KUFA angalau YEYE  ndiye wa kwanza kujua na kuwa na UZOEFU wa SWALA ZIMA la  ni nini KUDHALILIKA kabla ya kukwepa  kibano na KUFA..:-(



NDIO ujanja MPYA  waweza kuwa sio KUDHALILISHA wadhalilika,....
..... kwa kuwa kama kila MTU anadhalilisha  basi labda imeshafikia kuwa KUDHALILISHA SIO TENA UJANJA  na atakayeibuka kama MJANJA atatokea kwa  wapendwa wadhalilishwao a.k.a WADHALILIKA.:-(

Swali:
  • Si  inasemekana Rais Obama  kama RAIS wa KWANZA kuwa na baba MWEUSI  Marekani ni mjanja?
  • Si kuna uwezekano Rais Obama kama RAIS ASIYE KUWA WAKWANZA KUWA NA MAMA MWEUPE Marekani bado hilo lilimsaidia UJANJA?


Ila taka usitake MAISHA ya UJANJA ,....
...... ni mafupi ndio maana WAJANJA wa kweli huwa hawakatizii denge SHUGHULI.

Na ukikosea kutafsiri UJANJA,...
.... wajanja MAISHANI mwako wanaweza wakawa wala katika UJANJA hawapatii SHUGHULI.:-(



NDIO,...
.....Misingi  na siri ya UJANJA  WA MTU  ni dhaifu SANA ,...
....ndio maana DUNIANI  kuna MJANJA mpaka kwa KUNG'ANG'ANIA faraja za  NEPI  hajastukia BADO duniani kuna jeuri ya chupi PIA!:-(


Swali:

  • Si inakumbukwa ujulikanao kwa sasa kuwa ni  USHAMBA ni uleule ulioonekana  UJANJA  zamani?
  • Unafikiri unajua  MISINGI ya tafsiri yako ya Ujanja kwako ni nini na imeegemea wapi?
  •  Ujanja unafikiri ni nini?
 Kama unajua kikweli ni nini UJANJA,...
....NA  unajua SIRI ya utafsirivyo nani MJANJA,...
...weye ushatatua moja ya UDHAIFU WAKO!:-(

Swali moja zaidi katokori:
  • Unafikiri  kujua UDHAIFU wako sio kujiponza pia?






NIWAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(
NA nakutakia kila la kheri uwe na uhakika wa kupata  choo leo MKUU!




Hebu tubadili kwa kumdeku Mjasiliamali-







Au tu hebu Chick Corea, Bobby McFerrin na Bela Fleck walete kitu -Spain





Au tu OUTKAST warudie- Rosa Park

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 6:53 am  

Hata kunikumbusha ngoma ya Outkast ya Rosa Park ni ujanja. Hata kitendo cha Rosa Park kugoma kupisha siti akalie mtu mweupe ni ujanja.
Ila huu ujanja wa kusikiliza pini zenye akili za Reggae na Hiphop unaonekana ushamba kwa vijana wa siku hizi kwa sababu kwao ujanja ni mabongo fleva.

Simon Kitururu 7:23 am  

@Askofu Fadhy: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP