Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukiangalia mfumo wa mtu wa kujifunza MATUSI NI NINI , umsaidiao Simon Kitururu KUTOTUKANA hadharani .:-(

>> Friday, February 12, 2010

[Tahadhari: WAZO hili SIO JIPYA hapa KIJIWENI na unaweza usijifunze kitu katika hii taralila a.k.a POROJO!:-(]




MAISHANI kuna mengi  ya kuzungumzia na kujifunza,...
.. na NI KWELI labda katika ya MUHIMU sio LA kujitahidi kufuatilia  lipi lilikuwa tusi lako la kwanza.:-(


Lakini KWAKUFUATILIA au KUFIKIRIA mambo madogomadogo kama jinsi mtu aonavyo neno ni BONGE la tusi,...

... waweza kujifunza silika za WATU ambazo katika kugeuza neno NA KITU ni tusi mfumo huo huo waweza kutabiri nini ni  mfumo ufanyao kitu au neno kama ``NAKUPENDA´´ ni MUHIMU kwa MTU.


Sababu kubwa  hata MATUSI  yasiyo na maana yana maisha marefu,...
... ni kwa sababu kuna waogopao MATUSI  mpaka katika waitayo ni MATUSI hawatafuti MAANA.

Na MAUMIVU ya tusi yako katika tafsiri,...
....ingawa kitukanwacho mara karibu zote  wala sio SIRI.

Swali:
  • Unakumbuka tusi lako la kwanza?

Waliokutangulia kuishi wanaweza kuwa ni waanzilishi wa mtazamo wako wa,...
... nini ni tusi.

Mtoto akizaliwa na kuanza kutamka maneno yasiyoeleweka kwako,...
... uguswavyo au kustushwa na anachotamka HATA UBISHE  ni mwanzo wa kumfunza  pia a.k.a SHULE KWAKE  MTOTO kuwa neno gani kwako tusi.:-(

NDIO, tusi kwako,...
....lategemea sana wewe binafsi unavyo litafsiri ndio maana tusi kwako si lazima kwa wengine ni tusi.

 Swali:
  • Unafikiri ni kwanini tusi la kutukania  mama  au sehemu nyeti ni TUSI  karibu katika kila jamii DUNIANI  ?
  • Unafikiri kwanini sentensi NAKUPENDA inatumika kudanganya MTU atongozwaye KWA MAFANIKIO   karibu katika kila jamii DUNIANI ?


Maisha ni kiboko,...
... kwa kuwa MAISHA ni shule.

Maisha ni kiboko,...
.... kwa kuwa waweza mpaka kujifunza MAISHA yako  HUKU kwa kuangalia MAISHA ya WENGINE  kule.


Swali:
  • Au?

Lakini MAISHANI  waweza pia kujifunza ;..

Matusi si LUGHA
Matusi si VITENDO

Matusi ni tafsiri
Matusi ni  MAANA

Unamaanisha nini na Unatafsirije ndio vyaweza geuza NENO na TENDO ligeuke MATUSI.:-(

Swali:

  • Unafikiri hujidanganyi kwa kutumia lugha YA MTU  kama kioo cha TABIA ya MTU?
  • Unauhakika huku  MTUSI mtu jana kwa kuwa tafsiri  ya MTU  YA TUSI sio yako?


SAMAHANI kama  nishakukwaza kwa kitu ambacho MAISHA yako yalivyokufunza NI MATUSI katika BLOGU HII!:-(


Ijumaa na WIKIEND NJEMA MHESHIMIWA,  hata kama KWAKO inabidi utukane KISIRI kwa kuwa JAMII imekung'oa uhuru wakufurahia faraja ya  TUSI WAZIWAZI ili UTUNZE REPUTESHENI YAKO a.k.a Muonekano weye ni MHESHIMIWA.:-(


Au hebu SEUN KUTI aongee nakurudisha BUSARA kijiweni...



au aendelee






Au ngojea tu SEUN KUTI agawe dozi iitwayo - Many Things



Au kaka yake SEUN ,  Femi Kuti arudie- Do Ur BEST

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

o'Wambura Ng'wanambiti! 7:04 am  

Duh! kweli kabsaaaa!

Yawezekana pia kutusi ni akili :-(

KWani hujaona mabingwa wa kutusi wakipewa heshima ya kuwa na akili sana hata kama matusi wayatoayo ni jambo lilopitwa na wakati?

Yasinta Ngonyani 11:09 am  

Hehima kwako mt. nimekuelewa na natubu ila sijui padre yupo wapi?

o'Wambura Ng'wanambiti! 1:45 pm  

Da Yasinta: padre huyo hapo juu. Ingia tu katika kibox cha kuungama utubu :-)

chib 4:39 pm  

:-) kwa maoni hapo juu.
Mimi kila siku huwa najiuliza kwa nini sehemu nyingi duniani tusi wanaloliona ndio zuri kumtusi mtu aliyekuudhi basi linashabihiana na utupu wa mwanamke.
Hata na sie waswahili kuna sehemu fulani za jamii tendo la ngono hasa kwa watoto wadogo wanapocheza mchezo wa baba na mama, pengine na watu wazima wakikutwa wanafanya basi husemwa kwamba walikuwa wanafanya matusi, ila hawasemi pale basha anapomnanihii msenge.
Nina swali kabambe hapo kwa nini....

Simon Kitururu 4:07 pm  

@Kadinali Ng'wanambiti:DUH!

@Da Yasinta: DUH!
@Mkuu CHIB: Nakuna kichwa kwa maswali yako.:-(

chib 9:57 am  

Nakuaminia ya kuwa utapata jibu tu Mkuu :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP