Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SHOGA njoo pembeni TUMSENGENYE MAMA MWENYE NYUMBA kwa kuwa HAUSIGELI ni kibonde , TUTAMSUTA uso kwa USO!:-(

>> Monday, February 22, 2010

 Katika dunia yenye  WENYE mabavu,...
.... kwa kawaida WABABE HUSENGENYWA kwa SIRI ili wasije kubwenga MTU bure  wakisutwa USO kwa USO,....

....na ASUTWAYE uso kwa uso ni ambaye inaaminika katika tukio  hana MABAVU na akileta za kuleta wakati anapandishiwa sketi a.k.a ANASUTWA hata  MBATA na KONZI anawezabwengwa  kama nyongeza juu ya MSUTO.:-(





Swali:

  • SI unakumbuka mara nyingi  HATA WEWE ufanikiwaye KUMSUTA uso kwa uso   KWA KAWAIDA ni YULE ambaye humuogopi VIZURI?

  • SI unakumbuka UMSENGENYAYE  na KUMTETA na MASHOGA ZAKO  hasa yule rafiki yako bado  ni ISHARA ya KUOGOPA KUZUNGUMZA NAYE UFIKIRIACHO  na ndio sababu INGAWA UNAMSENGENYA NA MASHOGA ZAKO WENGINE  bado KWA KUMUOGOPA una kahofu kakutotaka ajue ni wewe UMTETAYE  kisa  unajua ana mimba ya PADRE  na wala si ya HAUSIBOI kama walivyohisi   WAMBEYA wa nyumba ya jirani  waliovalia njuga ufala wa MUME wa rafikiyo kabla huja waongezea MSENGENYO kwa kuwa tonya ishu?

  • Si unakumbuka kuna WAPINZANI wengi wa Rais KIKWETE ambao ni mabingwa tu ya KUMSENGENYA na KUMTETA wakati hayupo lakini akitokea KIJIWENI kumsuta HAWAWEZI?



Kwa mtazamo huo usishangae mahusiano YA ASUTWAYE  na ASENGENYWAYE na KUTETWA yakiwa na MWALIKO uliokaa mkawai :

Njoo tumsute MLALAHOI,...
... kwa kuwa FISADI  inabitumsengenye tu na kumteta kwa siri kwa kuwa mpaka POLISI ni hawala zake.


Njoo tumsute, KUMTETA  na kumpiga makonzi MSENGE,...
... kwa kuwa NJEMBA RIJALI yenye wake wengi hata  kuisengenya tu kwa hilo KIMILA nyingi za KIAFRIKA bado haiwezekani.


Njoo  tumsengenye MAMA MWENYE NYUMBA na sio HAUSIGELI,...
..... si unajua  kumsuta MAMA MWENYE NYUMBA unaweza kuchochea kubwengwa na mpaka BABA MWENYE NYUMBA ingawa kwa kumsuta HAUSIGELI  yaweza kuonekana sawa TU  ingawa HAUSIGELI na wala sio MAMA MWENYE NYUMBA ndiye kiburudisho cha  Baba Watoto.




Swali:
  • Lakini si unakumbuka asengenywaye kama hastukii asengenywacho  MSENGENYAJI labda anapoteza tu MUDA?
  • Si ulishawahi kufikiria kuwa mara nyingi UMSUTAYE unaweza pia kumsengenya lakini si kila UMSENGENYAYE unaubavu wa kumsuta kwa kuwa kusuta mtu huhitaji umuangalie machoni?



Ndio,...
....labda hata katika  ya  VIONGOZI wako  MAFISADI kuna uwezekano yote uyasikiayo ni MISENGENYO na kuteta tu kwa wasio na MABAVU ,...
....kwa kuwa hakuna wa KUWASUTA uso kwa USO.:-(

CHA ajabu ni kwamba,...
....wengi waogopwao KUSUTWA uso kwa USO mabavu yao  MISINGI YAKE  inatokana na  kitu hicho hicho ``KUOGOPWA´´.:-(

Swali:
  • Unauhakika weye MTANZANIA  Rais Lowasa Mkapa akiwa mbele zako utaongelea Richmondi kama utetavyo kijiweni na washikaji?

Ni wazo tu DHAIFU HILI Mheshimiwa lakini pamoja na yote NI  WAZO!



Hebu FALLY IPUPA abadili kwa -Cadenas





au tu tulia na Awilo Longomba - Awa Imani - African Tonic katika- C'est pas Complique

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 6:51 am  

Mkuu umemaliza yote. Maana hivyo ndivyo tuishivyo mitaani. Mtu akiwepo mabaya yake hayasemwi. Asipokuwepo kila mtu alonga la kwake hata kama katika hao wasengenyaji kuna aliyewahi kuchojoa na msengenywaji faragha siku fulani.
Binadamu bwana!

Simon Kitururu 11:59 am  

@Askofu Fadhy:

Mtu akiwepo mabaya yake yanamumunywa hata na wale ambao unajua ni wapayukaji sehemu nyingine.

Na inasemekana kwa Tanzania afadhali sasa kwa kuwa enzi za Nyerere, wamkosoaye NYERERE WENGI yasemekana ilikuwa akitokea ndio wa kwanza kutamka zidumu fikira za Mwenyekiti, Ujamaa OYEE.

Akiondoka wanasononeka ulaji unawapita. Na siumeona watu walivyojitajirisha baada ya kuacha kuogopa ya NYERERE ambao wengi wao ni walewale wa zidumu FIKIRA za Mwenyekiti Ujamaa oyeee!?


Na kwa wachojoao faragha na kuwa mstari wa mbele katika msengenyo maeneo , hilo ndio kabisaa kama ni jipu linausaha.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP