Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mwenye MAUMIVU huwa na staili yake TOFAUTI ya kuongelea UTAMU!

>> Monday, February 08, 2010

Kama umsikilizaye akiongelea UTAMU ni yule mwenye UCHUNGU na MAUMIVU,...
....kumbuka labda anogewachonacho kwa kudai nikitamu wakati yuko KWENYE MAUMIVU chaweza kuwa kwako bado ni MAUMIVU.:-(




Kama umsikilizaye akiongelea MAUMIVU ni yule aliyekatikati ya KUSIKILIZIA UTAMU,...
.... kumbuka kwa neno MAUMIVU inawezekana kwake na kwako neno hilo MAUMIVU katika harakaharaka za kusikilizia utamu ALIYELITAMKA alimaanisha ``JAMANI hii kitu TAMU!´´.:-(




Swali:

  • Si unakumbuka MAUMIVU YAKO yanaweza KUPOFUA UWEZO WAKO wa  kusikilizia kilichowahi KUKUUMIZA kuwa kwa mkao fulani ni hichohicho CHAWEZA KUWA ni kianzilishi cha aina fulani nzuri tu ya UTAMU?

  • Si unajua kuna UWEZEKANO kila wakati MAISHANI MWA MTU kuna MAUMIVU na aina TU ya KIMUUMIZACHO mtu ndio hutofautisha MAUMIVU na ni nini kimuumizacho mtu leo?


  • SI kunauwezekano WAWEZA kutofautisha MASIKINI aongeleavyo MAUMIVU YA UMASIKINI ilivyotofauti na TAJIRI aongeleavyo MAUMIVU YA UMASIKINI?


NDIO,...
... labda MWENYE MAUMIVU anauhakika zaidi na staili yake ya kuongelea MAUMIVU,....

... na kuna uwezekano pia mkubwa tu kuwa KUNA UDHAIFU katika ASIYE  na  MAUMIVU aongeleavyo MAUMIVU.:-(



Swali:

  • KATIKA AINA ZA MAUMIVU si kuna mpaka mwenye NYAMA YA KUKU ambaye kimuumizacho sana LEO ni kukosa kwake MAHARAGE ya Mbeya?



NI HILO TU na ni wazo tu MHESHIMIWA!:-(


Hebu ECKHART TOLLE aongelee Pain body katika -Your Pain Body is very Seductive



Tudeku -Why Black men silently SUFFER






Au tu 2PAC arudie kuongelea-PAIN

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:49 am  

nanukuu swali hili:- "Si unajua kuna UWEZEKANO kila wakati MAISHANI MWA MTU kuna MAUMIVU na aina TU ya KIMUUMIZACHO mtu ndio hutofautiana MAUMIVU na ni nini kimuumizacho mtu leo?" Ni swali nzurikwa kila mmoja wetu kujiuliza" Ahsante Mt. Simon. Upendo Daima!!

MICHUZI BLOG 7:51 pm  

Mt. Simon nimekukubali kwa falsafa. Inabidi mtu ukae chini na kudurusu na kufahamu nini maana ya maumivu. hakika umefanya utafiti yakinifu. Hongera sana

Simon Kitururu 10:35 pm  

@Dada Yasinta: Upendo Daima!
@Mkuu Michuzi: Asante Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP