Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Faraja za kuumia kwa wengine za : ``Mkuki kwa KIRUKA NJIA, kwa malaya wa kiume MCHUNGU!´´

>> Saturday, February 06, 2010

Kuna FARAJA katika kulalamikia ya WENGINE ,....
....kwa kuwa KWA MUDA MFUPI huondoa kufikiria YAKO.:-(



NA UBAYA wa ya wengine,...
... ni kwamba kunauwezekano ni kweli hayo NI YA WENGINE na hayakuhusu na sio kwa kuwa tu si YAKO.:-(


Na wakati unanyege ya kulalamikia WENGINE,...

.....chunguza kwa kuangalia ZAIDI yako na waweza KUSTUKIA kikukeracho hasa KATIKA YA WENGINE labda NI UDHAIFU wa YAKO.:-(





Swali:

  • AU?

Wakati unahangaika na YAKO hata kabla HAYAJAKUSHINDA yako,...
... yaweza kukufanya UWE MKALI kweli kwa ya wengine wasio HUSIKA.:-(




Na wakati UNALENGWA na MTU kuhusu yako,...
... inawezekana kabisa AKULENGAYE yuko tu katika KUHANGAIKA NA YAMSHINDAYO YAKE kwa kuyavalia njuga YAKO na kifaraja ANAKABILI YAKE kwa kujaribu kujifanya katika yako ANAHUSIKA.:-(


Swali:

  • Unataka kusema hujastukia uwezekano wa MTU AKERWAVYO na YAKO atambulishavyo YAKE MAPUNGUFU?

Ndio ,..
...MKUKI kwa nguruwe,...
... kwa BINADAMU mchungu.



Ndio,....
...MKUKI kwa mmoja nguruwe ,....
.... labda kwa nguruwe wengine wala sio MCHUNGU ndio maana nguruwe unaweza kumlisha KITIMOTO.:-(


NI wazo tu hili Mheshimiwa MAMA Kisebengo na wala USIKONDE kuendelea nalo kwa kuwa nimelisitisha ghafla kabla ya KUKUNA KIPELE!





Hebu Frank Sinatra aseme- Somethin' Stupid




Au tu Louis Armstrong adai pamoja na kibanochote maishani-What a Wonderful World

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP