Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa , ...KUWA na DHAMBI ni tofauti na JINSI ya kujisikia una DHAMBI!

>> Saturday, February 27, 2010

[ Tahadhari: JIHADHARI na WAZO hasa kama ULIVYO na unavyojisikia UNAFIKIRI  ni sawasawa!:-(]



Kuna UWEZEKANO  kabisaaa...
...kuwa  MASIKINI ni tajiri kama hujamfundisha MHUSIKA  jinsi ya kuusikilizia UMASIKINI!:-(


MATATIZO ya UMASIKINI ni MATATIZO tu kawaida  ,...
... na LABDA mpaka uyaoanishe tu na UMASIKINI ndio matatizo AMBAYO NI MATATIZO kutokunya KIKAWAIDA kwenye jedwali la MATATIZO  kuna ambayo utayaambatanisha na  SEKSHENI a.k.a kipengele cha MATATIZO yaletwayo na kibano cha UMASIKINI na kuyafanya kuwa MATATIZO HAYO ni MATATIZO YA UMASIKINI.:-(


Samahani,....

..... nimekumbuka , NIA na MADHUMUNI  ya taralila hii ni kuongelea DHAMBI.:-(



DHAMBI ,...
....ni FIKIRA aliyokuwanayo MTU  hasa baada ya TENDO,...

.... kwa kuwa DHAMBI inaweza ikawa ni TENDO LA NDOA  kabla HUJAFIKIRIA na kulioanisha kifikira na UZINZI.:-(


Kwahiyo ;...
...DHAMBI usiishangae kama  ni  tamu!


Na labda unajua  hata kama naheshimu kwamba HUTAKIRI,...

....  wala DHAMBI  hainauhusiano na UCHUNGU ingawa KIFIKIRA neno dhambi linamchezo wakufanya hata utamu wa ULICHODOKOA  ufikiriacho ni KISAFI  KIFISADI katika TAMU yake  YA MSHIKAKI  ukahisi KWAKE kunyunyiziwa chembechembe za kamasi la MPIGA CHAFYA ambalo husababisha utamu wa peremende usikilizwa kwa mikwaruzo ya ujuaji labda moja ya ifanyayo PEREMENDE tamu ni kamasi.:-(!


Swali:
  • AU?



Ndio,...
....DHAMBI ingekuwa MCHICHA,...
....kuna watu tungejaza TENGA!:-(


Ila kwa jinsi DHAMBiI ilivyokuwa NYOKO,...
.... ahubiriye DHAMBI mara karibu zote ndiye aliyekuwa na TAFSIRI FULANI  ya uhakika kwake YA DHAMBI ,...
....kitu kifanyacho awe miongoni mwa WATU ambao kwa uhakika wanajua wafanyavyo ni DHAMBI.:-(




Ndio ,...
...jinsi yako YA  kufanya DHAMBI  yaweza kuathiriwa na STAILI yako ya  unavyoisikilizia DHAMBI.

Na kwa kuifikiria dhambi,...
waweza kustukia  katika  dunia ya WENYE DHAMBI, watu wengi wanakustukia WEYE ni MWENYE DHAMBI kwa kuwa tu  NI KWELI  katika wafunikao kwa GWAGURO ,...
...WEYE unaikalia uchi na kuionyesha masharubu ya chini  DHAMBI .:-(



Tukiacha MZAHA ;....
Swali:

  • Unauhakika DHAMBI ni nini?
  • Unafikiri UMASIKINI USIKILIZIWAVYO kama tu DHAMBI  , unauhakika MASIKINI ni muda gani  HUWA anajisikia MASIKINI?
  • Unauhakika TAJIRI anajisikia tajiri wakati anakunya?
  • Unafikiri wewe kama ni MKRISTO ambaye  kwako ruksa ni kuonjeshwa kidude kimoja tu NA MKE WAKO  WA NDOA huwa unaelewaje na KUIGEUZA NI DHAMBI   ya MUISLAMU ambaye kwake SIO DHAMBI ,- ile ya KUONJESHWA VIDUDE VINNE  kutoka kwa WAKE WANNE WA NDOA  awawezao kuwapa huduma WAJISIKIE NI WAKE WA MTU  wapatao matekenyo yote ya NDOA   kwa maadili  ya KIISLAMU?
  • Unafikiri dhambi yako ya UZINZI  inafanana na dhambi ufikiriayo ni  HIYO HIYO kwa mwingine YULE aliyedakwa UGONI na wewe ambaye hafikirii kama WEWE?

  • Unafikiri kuna MTU anajisikia ana DHAMBI kama alivyo na DHAMBI?


NI HILO TU!
JARIBU TU  kukumbuka  ni TAFAKURI tu hii  MHESHIMIWA  na KUNAUWEZEKANO  kama WAZO HILI  limevalishwa chupi , basi chupi INATOBO!:-(


Hebu ANDREW SAMUEL alainishe na kubadili HALI YA HEWA KIJIWENI kwa ndude-Pinacolada



Maxi Priest abadili zaidi kwa ndude-Close to U



Au tu MAXI Priest amalizie tu kwa ndude-Just a little bit longer

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP