Labda umuhimu wa MTOTO kwa baadhi ni TUMIZI la MTOTO,.....
>> Thursday, February 18, 2010
.....katika ajenda za WAKUBWA waliozaa kujisikia kuna kitu ANGALAU KIMOJA TU wamefanikiwa kufanya KATIKA ya DUNIANI !:-(
NA labda sio utani ,...
... kuwa umuhimu wa MTOTO kwa binadamu waliozaa ni tumizi la ya mtoto LIZIBALO na KUJAZIA kizibwacho na hisia na shughuli zitokanazo na kuwa na MTOTO DUNIANI ambazo huanzia tokea mzazi ajue atapata MTOTO.:-(
Labda si utani ,...
...MTOTO kama tumizi kuna walikabilio kama ni SHUGHULI tu mojawapo iwasaidiayo WENYE MTOTO kujisikia tu kuwa pamoja na matatizo yote ni kweli WAKO HAI na kithibitisho ni hata mwenye utapiamlo MTOTO.:-(Labda sio utani,...
... mtoto ni MTAJI wa baadaye , wakati MKE ni trekta la sasa HIVI kama UNA SHAMBA kubwa na pembejeo ni JEMBE shambani katika shughuli ya kilimo isiyo ya KITOTO.:-(Swali:
- MTOTO wako ni wa nini wakati kwa MTAKA WAJUKUU anaweza zaa mtoto atakaye kuwa PADRE wa KATOLIKI asiyeruhusiwa kuoa au kuzini kwa ruksa iletwayo kwa ndoa?
- MTOTO wako ni wanini wakati kwa MTAKA WAJUKUU anaweza kuzaa mtoto tasa?
Na kuna wenye WATOTO,...
... kwa kuwa katika kuhusudu URODA mtoto ni ajali kazini.
Kuna wenye MTOTO,...
... kwa sababu KUWA NA mtoto kwawasaidia tu KUWALETEA maana ya maisha hapa duniani.
Na kuna wahitajio MTOTO,...
.... kama msaada wa MAISHA uzeeni.
Swali:
- Unauhakika ni wangapi wana watoto na hata siku moja hawakufikiri ni kwanini wana watoto?
- Katika watoto waitwao wa mtaani duniani unafikiri ni wangapi wamezaliwa kutokana na wazazi wao kutofikiria yahusianayo na MTOTO kabla ya kuzaa mtoto?
- Unafikiri matajiri kama akina OPRAH wenye mabiloni si kufuru kutokuwa na MTOTO au akina Rais Clinton kuwa na mtoto mmoja tu si kitendo cha upotezaji wa mbegu na mayai yashughulikiayo mafanikio ya MMIMBISHO?
- Hivi MTOTO kwako ni wa nini?
Na kwa wengine ,...
.. LABDA mtoto UMUHIMU WAKE ni kama tu MWANASESERE kwa kuwa,....
..... SI MAMA YAKE YUPO atakaye mshughulikia ambaye yeye ni VIGUMU kumkimbia bila nyonyo kuvuja MTINDI akilia?
Swali:
- Unauhakika ni kweli unahitaji WATOTO au hata ndoa ukizingatia maisha yako ukiyatafutia MAANA kivingine yanaweza kuleta tu maana kama ya MASISTA wa KIKATOLIKI ambayo bila ZE TOTOZ yanalipa tu na hutabadili nepi rojo?
NI tafakari tu hii MHESHIMIWA wakati tunajua MAZOEZI ya kitendo yanaendelea DUNIANI na kwa kitendo KUNA mtu kammegea MTU mahali fulani MIMBA !:-(
Au hebu THE LAST POETS wabadili zaidi kwa tafsiri yao ya - Black is
Au tu The LAST POETS wabadili tena mtazamo wao kuwa -NIGGERS are SCARED of REVOLUTION
Au tu The Last Poets wamalizie kwa - When The Revolution Comes
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment