Tukiangalia HALI HALISI ,labda HALIHALISI NDIYO inamlazimisha MKULIMA kuwa MKULIMA!:-(
>> Saturday, February 06, 2010
Labda HATA nesi kawa nesi,....
...... kwa kuwa hali halisi imefanya ahitajike nesi.
Na labda Mkulima angekuwa TANDIBOI ,....
.... kama KIHALIHALISI kungekuwa na basi KWA WAKULIMA lihitajilo TANDOBOI.:-(
Swali:
- Unafikiri Ni wakulima wangapi wangekuwa na chaguo tofauti wangeamua kuwa wakulima?
- Unauhakika pamoja na KIRUKA NJIA kupigwa vita , HALI HALISI ya uwepo wa KIRUKA NJIA hailetwi na hitaji kubwa la kidude cha Kiruka NJIA ?
- Unafikiri ni kwanini Mtakatifu Simon Kitururu sio Mkulima?
- Unauhakika kama wewe sio malaya , wee SI MALAYA kwakuwa TU hali halisi haijaruhusu tu?
Hali halisi yaleta shughuli,....
... na shughuli yenyewe yawezakuwa inahitaji MZIBUA choo.
... na shughuli yenyewe yawezakuwa inahitaji MZIBUA choo.
Na ni HALI HALISI KUWA Mzibua choo KWA KAWAIDA anahitajika kwenye CHOO.:-(
NI HILO TU na NI WAZO TU hili Mheshimiwa Bulicheka!
Au tu turudi Kameruni Bebe Manga arudie-Mota Benamaa
Au tu Bebe Manga arudie tena na-Amio
Asanteni wadau wote hasa kwenye African Party mlionisaidia kwa muda fulani KUSAHAU kuwa DUNIA NYOKO , hii siku ambayo kwangu ilikuwa ni mara ya kwanza kula nyama ya Pundamilia ,- ambao baadhi mpo kwenye taswira zangu baadhi zifuatazo...
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kitururu unajipenda jamani mwee!!
@Da Mija: Nisipojipenda ntawezaje kumpenda jirani?
Si nasikia hushauriwa kuwa Mpende jirani kama ujipendavyo?
kwa kweli mkuu Simon umenishangaza kwa kutumia kisu na umma.
Naamini sote tulifundishwa kula kwa kutumia mikono.
Hehehe pamoja na Msosi wote huo,kisu umma na mazagazaga yote Bw Nyahbingi,Bw Kitururu hawezagi kula
@Rasta Luihamu: Kama hili nalo linakushangaza basi naogopa kutafakari ni mangapi yanakushangaza Mkuu.
Miye nilichojua mwenyewe ni kunyonya tu , na nasikia nilivyosogezewa chuchu tu nikakaa mkao wa kunyonya maziwa mpaka na lala hapohapo kifuani .
Kulia mkono , vijiti , kijiko, umma na kisu nimeigilizia tu WALIONITANGULIA kustukia MISOSI a.k.a NGUNA baada ya kufumbuka macho na kuanza kunyimwa nyonyo na mama.:-(
Lakini bado mtazamo wangu ni :
... Umuhimu wa chakula ni kuliwa na sio jinsi au staili ya unavyoliwa.
Na kulia mikono ni luxury tu za wenye mikono kwa kuwa asiye na mikono hata kwa miguu ni bonge tu la staili ya kufikisha chakula mdomoni ili NGUNA a.k.a MSOSI ugwidwe.:-(
@Altunes: :-)
Post a Comment